JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Prof. Sospeter Muhongo

Mh. Mbunge, Prof. Sospeter Muhongo (CV1)AND (CV2)

"Tovuti Rasmi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo, Kwaajili ya Kuwasiliana na Wananchi Jimboni "

MBUNGE WETU MH. PROF. SOSPETER MUHONGO ANATUHAMASISHA KUTEMBELEA WEBSITE HII KILA MARA, KWA MAENDELEO YETU SOTE.

A CONCISE PROFESSIONAL CV OF PROF. SOSPETER MWIJARUBI MUHONGO

(1) Fellowships in the topmost Science Societies/Academies of the World

*Honorary Fellow of the Geological Society of London, (est. 1807), HonFGS

*Honorary Fellow of the Geological Society of America (est. 1888), HonFGSA

*Honorary Research Fellow of the Chinese Academy of Geological Sciences (est. 1956), HonRFCAGS

*Fellow of The World Academy of Sciences, FTWAS

*Fellow of the African Academy of Sciences, FAAS

*Fellow and Life Member of the Geological Society of Africa, FGSAf

*Member of the Academy of Science of South Africa, MASSAf

(2) World's Top Science Leadership

*Former Vice President of the Commission of the Geological Map of the World (CGMW)

*Former Chair of the Science Programme Committee of the UN-proclaimed International Year of Planet Earth (UN-IYPE)

*Former Chair of UNESCO-IUGS-IGCP Scientific Board of the International Geoscience Programme

*Former President of the Geological Society of Africa (GSAf)

*Former Regional Director (Africa) for the International Council of Scientific Unions (ICSU-ROA)

(3) Preparation & Publication of Geological Maps

*Co-Author of Geology & Mineral Maps of Africa, East Africa, and Tanzania

*Co-Supervision for the publications of the geological maps of the world

(4) Publication of Science Books

*Senior Author of a Book (2009) on Science, Technology and Innovation for Socio-Economic Development: Success Stories from Africa

(5) Publication of Science Policy Booklets

*Cordinator for the preparation and publication of 4 Science Plans for sub-Saharan Africa (2007, ICSU ROA). They are on:
+Sustainable Energy
+Health and Human Well-being
+Global Environmental Change
+Natural and Human-induced Hazards and
Disasters

(6) Science Journal Publications

*More than 200 publications in international learned journals of high to moderate Impact Factors (IFs)

*Editor-in-Chief Emeritus of the Journal of African Earth Sciences (JAES), published by Elsevier, Amsterdam

*Editorial Board Member of the Precambrian Research Journal, published by Elsevier, Amsterdam

(7) Keynote Speaker

*Invited Keynote Speaker to over 500 national and international conferences

(8) Convener of Conferences for high-level science experts

*Co-Organizer/Convener of over 100 Science Experts' Conferences around the World

(9) Major International & National Awards
Many scholarly, professional, and research awards and scholarships, including:

*Officier, The Ordre des Palmes académiques. An academic decoration introduced by Emperor Napoleon in 1808

*The Prof Robert Shackleton Award for Outstanding Research on the Precambrian Geology of Africa

*The Nigerian Mining and Geosciences Society (NMGS)/AMNI Petroleum Award of Prof.M.O. Oyawaye

*The National Award for Research in Science and Technology (NARST), Tanzania.

*The Best First Year Student in the Faculty of Science of the University of Dar es Salaam (1976/1977)

*The 1971 Best Debating Student at Mara Secondary School, Musoma, Tanzania. He was in Form III.

(10) University Education

*Dr.rer.nat. graduate of the Technical University of Berlin (TU-Berlin), Germany

*MSc Research Student of the University of Góttingen, Germany

*MSc, BSc (Hons) (Geology) graduate of the University of Dar es Salaam, Tanzania

Prof Sospeter Mwijarubi Muhongo is a very distinguished world-class scholar, a Chartered and a European geologist. He is a retired Full Professor of Geology. He writes and speaks fluent Kiswahili, English, and German languages. His French is basic.

Prof Dr.rer.nat. Sospeter M Muhongo
Officer, Ordre Palmes Academìques
(FGSAf, FAAS, MASSAf, FASI, FASSAf, FTAAS, FGIGE, FTWAS, HonRFCAGS, HonFGSA, HonFGS, CGeol, EurGeol)

Homepage:
www.musomavijijini.or.tz

Telephone:
+255 754 400 800

Date:
Tuesday, 14.11.2022

 

 

Matukio katika picha - (Toa Maoni Hapa)

Habari Mpya Toka Jimboni

TAARIFA MPYA JUU YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO JIMBONI MWETU --MPYA--

(1) BARABARA
1a. Musoma-Makojo-Busekera
*TANROADS wako kwenye utaratibu wa manunuzi kwa ajili ya uwekaji lami kwenye barabara hili ambalo Serikali imeamua kulijenga kwa awali mbili.

*Nimewasisitizia (Mbunge wa Jimbo) kwamba ujenzi unaotafutiwa Mkandarasi uwe wa kuendeleza ujenzi wa Lot 2 (Kusenyi-Makojo-Busekera) ambapo kilomita 5 za lami zilijengwa kwa miaka minne (4)!

1b. Utengenezaji wa barabara la Musoma-Mugango-Makojo-Busekera
*TANROADS Mkoa wameanza matengenezo ya uboreshaji wa barabara hili kwa kipande cha Musoma-Mugango

(2) KILIMO CHA UMWAGILIAJI
2a. BONDE LA BUGWEMA
*"Consultant" ameanza kufanya "feasibility study" (tarehe 17.9.2023 - 16.10.2023). Nimempa taarifa kwamba nitawatembelea wakiwa kazini Bugwema.

*Mazao makuu yatakayoliwa kwa umwagiliaji ni: mahindi, mpunga, alizeti, dengu, pamba na mboga mboga

2b. BONDE LA SUGUTI
*"Consultant" atafanya "feasibility study" baada ya kukamilisha kazi kwenye Bonde la Bugwema

3. ELIMU
3a. ELIMU YA SEKONDARI - MAABARA
*Tunaendelea na ujenzi wa maabara 3 (Physics, Chemistry & Biology) kwa kila Sekondari. Tuendelee kuchangia ujenzi huu na tunashukuru kila mara Serikali inapotuunga mkono kwa michango yake mikubwa

*Halmashauri yetu (Musoma DC) iendelee kukumbushwa kuchangia ujenzi wa maabara 3 kwenye kila Sekondari yetu ya Kata (kwa saa tunazo 25 na tunajenga mpya 5. Sekondari za Binafsi ni 2)

3b. SCIENCE HIGH SCHOOLS
*Tunaendelea kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu muhimu inayotakiwa kwenye uanzishwaji wa science high schools.

*Vinavyohitajika kwa uanzishwaji wa "science high school" ni: maji ya bomba, umeme, maabara 3, bweni, na bwalo la chakula.

*Lengo letu ni mwakani, 2024, Jimbo letu liwe na angalau HIGH SCHOOLS 2-3 za masomo ya sayansi. Ile ya Kasoma ni ya masomo ya "arts."

3c. ELIMU YA MSINGI - MRADI WA BOOST
*Shule za Msingi tisa (9) zimepewa jumla Tsh bilioni 1.35 kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu kwenye shule hizo.

*Wananchi, Mbunge wa Jimbo na Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya waendelee kufuatilia mradi huu kwa ukaribu sana.

*Shule za Msingi zilizopewa fedha ni: Bugoji, Buira, Bulinga B, Kanyega, Kataryo B, Kigera B, Mabuimerafuru B, Masinono na Nyambono B

4. MAJI YA BOMBA KUTOKA ZIWA VICTORIA
4a. Maji ya MUWASA kupelekwa kwenye Kata za Etaro, Nyegina, Nyakatende na Ifulifu

*MUWASA inaendelea kukusanya baadhi ya vifaa hitajika kwa kutumia vyanzo vyake vya fedha.

*Vilevile, MUWASA imewasilisha Serikalini Bajeti ya kutekeleza mradi huu

*MUWASA imeishaanza kusambaza maji ya bomba kwa baadhi ya maeneo ya kata hizi

*Kijiji cha Nyasaungu cha Kata ya Ifulifu kimeanza kupata maji ya bomba kutoka kwenye bomba la zamani la Mugango-Kiabakari-Butiama

4b. Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama
*Ujenzi umekamilika kwa asilimia 92 (92%) na ifikapo Disemba 2023 kazi zote muhimu zitakuwa zimekamilishwa

4c. MIUNDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI NDANI YA KATA YA TEGERUKA
*Maji ya bomba kwenye Kata hii yatatoka kwenye Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama

*Mabomba yametandazwa ndani ya vijiji vyote vitatu vya Kata hii, ambavyo ni Kataryo, Mayani na Tegeruka

*Tenki la ujazo wa LITA 135,000 tayari linakamilishwa ujenzi kijijini Mayani

4d. MIUNDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI NDANI YA KATA YA MUGANGO
*Kata hii nayo itapata maji ya bomba kutoka kwenye Bomba la Mugango- Kiabakari-Butiama

*Mabomba yamesambazwa kwenye vijiji vyote vitatu vya Kata hii, ambavyo ni Kwibara, Kurwaki na Nyang'oma.

*Tenki la ujazo wa LITA 500,000
limejengwa kwenye Mlima Kong'u kijijini Nyang'oma

4e. MINDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI KWENYE KATA ZA BUSAMBARA NA KIRIBA
*Maji ya bomba ya Kata hizi mbili yatatoka kwenye Tenki ya LITA 500,000 liliojengwa Mlimani Kong'u. Maji yake yatatoka kwenye Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama

*RUWASA imepata vibali vyote hitajika kutoka Serikalini, na ndani ya miezi miwili miundombinu ya usambazaji maji ya bomba ndani ya Kata hizi itaanza kujengwa.

4f. MINDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI KWENYE KATA YA BWASI
*Vijiji vyote vitatu vya Kiti hii, yaani Bwasi, Bugunda na Kome vinatandaziwa mabomba ya maji

*Ujenzi wa Tenki la ujazo wa LITA 150,000 tayari limekamilishwa Kijijini Bwasi

4g. MINDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI YA BOMBA KWENYE VIJIJI VYA CHUMWI & MABUIMERAFURU
*Ujenzi wa Tenki la ujazo wa LITA 300,OOO umekamilika kijijini Mabuimerafuru

*Mabomba yanaelendelea kutandazwa

*Maji kutoka kwenye Tenki hili yatasambazwa kwenye vijiji vya Masinono na Bugwema (Kata jirani ya Bugwema)

4h: MAJI YA KISIMA CHA RUSOLI SEKONDARI
*Tunaendelea kuwashukuru baadhi ya WAZALIWA wa RUSOLI kwa ufadhili wa uchimbaji wa kisima hiki.

*RUWASA imekamilisha ujenzi wa Tenki la LITA 75,000 kwa ajili ya usambazaji wa maji kijijini hapo.

5. AFYA
5a. HOSPITALI ya Halmashauri yetu yenye hadhi ya Hospital ya Wilaya imeanza kutoa HUDUMA za AFYA hapo ilipojengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijijini Suguti.

*Hospitali hii inavyo vifaa tiba vya kisasa sana, ikiwemo Digital X-ray, Ultrasound, Vifaa vya Upasauji, Mitambo ya kutengeneza Oxygen.

5b. VITUO VYA AFYA
*Kwa sasa tuna jumla ya Vituo vya Afya sita (6) ambavyo ni: (i) Murangi, (ii) Makojo (mpya), (iii) Kiriba (mpya), (iv) Kisiwa cha Rukuba (Zahanati yake imepanuliwa), (v) Mugango (Zahanati yake imepanuliwa), na (vi) Bugwema (ilikuwa Zahanati ya Masinono, imepanuliwa)

5c. ZAHANATI
*Tuna jumla ya Zahanati 42
*Zahanati 24 zinatoa Huduma za Afya vijijini mwetu
*Zahanati 14 zinaendelea kujengwa na baadhi karibu zitakamilishwa ujenzi.
*Zahanati 4 za Binafsi zinatoa Huduma za Afya vijijini mwetu.

5d. MAGARI YA WAGONJWA (AMBULANCES)
*Tunayo magari ya kusafirishia wagonjwa (ambulances) matano (5). Mbunge wa Jimbo ndiye aliyefanikisha upatikaji wa ambulances hizi.

*Ambulance iliyoko Kituo cha Afya cha Murangi ni ya kisasa ambayo upasuaji unaweza kufanyika wakati mgonjwa akiwa anasafirishwa. Serikali ya Japan ilimpatia Mbunge wa Jimbo ambulance hii.

*Ambulance nyingine nne (4) zilinunuliwa na Mbunge wa Jimbo akishirikiana na rafiki zake.

*Tunaendelea kufuatilia miradi ya usambazaji UMEME vijijini mwetu (REA & TANESCO). Miradi ya REA itaanza hivi karibuni

*Tunaendelea kufuatilia miradi ya ujenzi na uboreshaji wa barabara zetu vijijini (TARURA & TANROADS)

*Tunaendelea kufuatilia uboreshaji wa miundombinu ya usambazaji maji ya bomba vijijini mwetu (RUWASA & MUWASA)

Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz

SHUKRANI
Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na WADAU wengine wa uchangiaji wa Maendeleo na Ustawi wa Jimbo letu wanapewa shukrani nyingi sana - tafadhali endeleeni kutuunga mkono.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 20.9.2023

TAARIFA ZA MIRADI MBALIMBALI YA MUSOMA VIJIJINI

1. Barabara ya Musoma-Makojo-Busekera (km 92)

*Ujenzi wa kilomita 5 (Kusenyi hadi Suguti, Kwikonero) umekamilika wiki jana

*Ujenzi wa kilomita 87 zilizosalia:

Ombi liko ndani ya Wizara la kushawishi Mradi huu wa KM 87 uwekwe wote kwenye Bajeti ya Mwaka unaoanza tarehe 1.7.2023, yaani, Mwaka wa Fedha 2023/2024

2. Maombi ya Mikopo ya UVUVI

*Tulituma jumla ya maombi 10 yakiwa ya: (i) boti za uvuvi na (ii) vizimba vya uvuvi.

*Taarifa niliyopewa (Mbunge) ni kwamba sehemu kubwa ya maombi yetu imekubalika.

*Wapo watakaopata mikopo ya boti yenye thamani ya kati ya Tsh Milioni 16 na 72

*Wapo watakaokopeshwa vizimba 8 vyenye thamani ya Tsh Milioni 130

*Orodha na maelekezo ya upokeaji wa mikopo hiyo utatolewa hivi karibuni na Wizara husika.

3. Ujenzi wa VETA Musoma Vijijini

*Serikali imeamua kujenga VETA moja kwa kila Wilaya

*Sisi Wilaya yetu inayo VETA hapo Mwisenge, Musoma Mjini. Hii ilikuwa VETA ya Mkoa wa Mara, sasa inakuwa VETA ya Wilaya ya Musoma.

*Wizara imeshawishiwa na kuona umuhimu wa Musoma Vijijini kupata VETA yake.

Tumeombwa tukabidhi VETA MAKAO MAKUU eneo lililoainishwa kwa ajili ya ujenzi wa VETA tunayoiomba.

Mbali ya ufinyu wa Bajeti, Wizara itajitahidi kutafuta fedha za ujenzi wa VETA ya Musoma Vijijini. Halmashauri itekeleze hili!

4. Minara mipya ya Mawasiliano

Ombi letu linafanyiwa kazi, pamoja na maombi mengine ya nchini kote. Tutajulishwa.

5. Ujenzi wa Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba

*Taarifa ya uamuzi wa Wakazi wa Rukuba kuwa na Sekondari yao hapo Kisiwani imefikishwa kwa Wahusika TAMISEMI, na hakuna kuzuizi cho chote kilichopo.

*Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba waanze matayarisho ya mradi huu. Mbunge wa Jimbo ataenda huko kupiga Harambee ya ujenzi wa Rukuba Sekondari.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Alhamisi, 9.2.2023

Kalamu ya Mh. Mbunge, Prof. Sospeter Muhongo

BUNGENI

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, ameelezea umuhimu wa Tanzania kuzalisha umeme mwingi kutoka vyanzo vingine na ametoa mifano ya umeme mwingi kutoka: umemejua (solar), upepo (wind) na jotoardhi (geothermal).

Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumatano, 24.4.2024

ALAT MKOA WA MARA WASHUHUDIA USHIRIKIANO MZURI KATI YA WANANCHI NA SERIKALI YETU KWENYE UJENZI WA KIGERA SEKONDARI

Jana, Jumatano, 17.4.2024, Viongozi wa ALAT Mkoa wa Mara walitembelea Kigera Sekondari iliyojengwa Kijijini Kigera (Etuma), Kata ya Nyakatende.

Sekondari hii ambayo ni ya pili ya Kata ya Nyakatende, ilianza kujengwa Mwaka 2020 kwa nguvu za Wananchi wa Vijiji viwili vya Kigera (Etuma) na Kakisheri, na Mbunge wao wa Jimbo la Musoma Vijijini.

Baadae, Serikali ilichangia na inaendelea kuchangia ustawi wa shule hii. Miumbombinu ya Elimu ya Sekondari hii imejengwa kwa ubora mkubwa - ALAT imedhibitisha ubora huu!

Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa - Wananchi wanashukuru sana juhudi za Serikali yetu.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Alhamisi, 18.4.2024

MAJI YA BOMBA MUSOMA VIJIJINI - MAKABIDHIANO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA USAMBAZAJI WA MAJI YA BOMBA YAFANYIKA KIJIJINI KWIKUBA

Kata za Busambara (vijiji: Kwikuba, Maneke na Mwiringo) na Kiriba (vijiji: Bwai Kumsoma, Bwai Kwitururu na Kiriba) zimeshuhudia Mkataba wa kusambaziwa maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria ukitiwa saini Kijijini Kwikuba.

Makabiadhiano hayo kati ya RUWASA na MKANDARASI (Otonde Construction & General Supplies Ltd) yalifanyika siku ya Jumatano asubuhi, 20.3.2024.

Walioshuhudia utiaji wa saini za Mkataba huo ni: wananchi kutoka Kata hizo mbili, viongozi kadhaa wa Chama (CCM) na Serikali, DAS Wilaya ya Musoma, na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

RUWASA inasifiwa sana kwa kufanya kazi nzuri Musoma Vijijini - hongereni sana RUWASA!

Gharama za Mradi huu:
Jumla ni: Tsh bilioni 4.42
Kazi za awali zitatumia: Tsh bilioni 1.44

Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumanne, 26.3.2024

MABADILIKO YA RATIBA YA KAZI ZA MBUNGE WA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Jumanne, 19.3.2024
*Kushiriki kwenye Kampeni za CCM za Uchaguzi wa Diwani wa Kata ya Mshikamano, Musoma Mjini

Jumatano, 20.3.2024
Saa 5 asubuhi: Kata ya Suguti
*Upandaji wa miche ya miti kwenye Sekondari ya Suguti

*Ugawaji wa Vitabu 2 vinavyoelezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Jimboni mwetu. Viongozi wa CCM wa Kata ya Suguti na Matawi yake wataanza kugawiwa

Jumatano, 20.3.2024
Saa 8 mchana: Kata ya Musanja
*Mkutano na wananchi - kutatua kero za wananchi

Harambee ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mabuimerafuru

*Ugawaji wa Vitabu 2 vinavyoelezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Jimboni mwetu. Viongozi wa CCM wa Kata ya Musanja na Matawi yake wataanza kugawiwa.

WOTE MNAKARIBISHWA

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatatu, 18.3.2024

FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO: VIFAA VYA UJENZI VINAANZA KUGAWIWA JUMANNE, 12.3.2024

Fedha: Tsh 75,769,000 (ca. Tsh 75.8m)

Vifaa vilivyonunuliwa:
(1) Saruji, Twiga Plus: Mifuko 2,010
(2) Nondo, 12mm: 311
(3) Mabati ya rangi: 344

Kipaumbele cha matumizi ya vifaa hivi:
Ukamilishaj wa ujenzi wa Maabara 3 (Physics, Chemistry & Biology) kwa kila Sekondari ya Kata ndani ya Jimbo letu.

Sekondari zilizotuma maombi ya saruji na kilichopatikana:
Makojo imepata mifuko ya saruji 150, Nyasaungu 50 (mpya), Rukuba Kisiwa 205 (mpya), Kigera 100, Nyanja 100, Bulinga 100, Bukwaya 150, Muhoji 50 (mpya), Rusoli 100, Busambara 150, Nyambono 150, Mtiro 150, Suguti 100, Etaro 100, Seka 150 na David Massamba Memorial 205 (mpya)

Uchache wa mabati yaliyonunuliwa:
Uchache wa mabati ya rangi yaliyonunuliwa, umelazimisha mgao uende kwenye Sekondari zenye maboma ya kukamilisha ujenzi wa maabara zao, ambazo ni:
Etaro (mabati 120), Mabuimerafuru(105) na Mtiro (139)

Usafirishaji wa vifaa vitakavyogawiwa:
Kila Sekondari itajitegemea kusafirisha vifaa vya ujenzi walivyogawiwa kutoka kwenye Bohari ya Halmashauri yetu iliyoko Musoma Mjini.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatatu, 11.3.2024

WANANCHI WA MUSOMA VIJIJINI WAMEAMUA KUACHANA NA UVUVI HARAMU

Ziara ya tarehe 29.2.2024 ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa aliyoifanya Musoma Vijijini imetoa hamasa na ushawishi mkubwa kwa wavuvi wetu kuachana na uvuvi haramu!

Wadau wa Maendeleo wa Jimbo la Musoma Vijijini wanashirikiana na Serikali yetu kutokomeza uvuvi haramu ndani ya Ziwa Victoria. Mmoja wa wadau hao ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Wilaya ya Musoma Vijijini, Ndugu Jackson Nyakia Kikomati.

Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa - uvuvi haramu unashughulikiwa ipasavyo.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 6.3.2024

Vipaumbele vya Mh. Mbunge

Elimu
Kila mtoto aliyefikia umri wa kwenda shule, awe shuleni na kuinua kiwango cha ufaulu
Afya
Kusogeza huduma bora za afya zinazokidhi uhitaji kwa wananchi
Kilimo
Kilimo cha kisasa, endelevu na chenye uzalishaji mkubwa kwa eneo
Maji
Gharama nafuu katika upatikanaji wa maji safi na salama kwa kila kaya