SEKONDARI YA AMALI YA NYAMRANDIRIRA YAZINDULIWA

Jimbo la Musoma Vijijini limekuwa miongoni mwa majimbo ambayo Halmashauri zake zimeanza kujengewa Sekondari za Amali

Jana, Mgeni Rasmi, Mhe DC Juma Chikoka alizindua sekondari ya mali ya uhandisi inayojengwa Kijijini Kasoma, Kata ya Nyamrandirira.

Kata hii yenye vijiji vitano (5) inazo Sekondari tatu (3) na High School moja (1)

Wanavijiji wa Kata hii wakiongozwa na Madiwani wao mahiri, Mwl Wanjara Nyeoja (Diwani wa Kata) na Mwl Nyachiro Makweba (Diwani Viti Maalum) wameshiriki na kuchangia ipasavyo ujenzi wa sekondari hii.

Matukio makuu muhimu ya sherehe hiyo:

*Mgeni Rasmi kukata utepe wa kuzindua shule mpya

*Wimbo maalumu wa kuelezea umuhimu wa Elimu ya Amali nchini mwetu

*Chakula kwa wote kilichoandaliwa na Mbunge wa Jimbo

*Mbunge wa Jimbo kugawa bure vitabu viwili viwili vya rangi (Volumes V & VI) vinavyoelezea mafanikio ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025

Viambatanisho vya hapa:
(i) Picha ya ukataji utepe
(ii) Wimbo maalumu wa umuhimu wa Elimu ya Amali kutoka S/M Nyamrandirira

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumapili, 8 Juni 2025