
RC MTAMBI AZINDUA SEKONDARI ILIYOANZA KUJENGWA KWA NGUVU ZA WANANCHI
Mgeni Rasmi: RC Mhe Col Evans Mtambi
Leo, Mkuu wa wa Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Col Evans Mtambi amezindua Muhoji Sekondari ya Kijijini Muhoji, Kata ya Bugwema
Hii ni sekondari ya pili ya Kata hii yenye vijiji vinne (Bugwema, Kinyang'erere, Masinono na Muhoji)
Mgeni Rasmi huyo amewaeleza wananchi wa Kata ya Bugwema dhamira nzuri na yenye manufaa makubwa ya Mheshimiwa Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan ya uwekezaji mkubwa anaoufanya kwenye Sekta ya Elimu.
Wananchi wa Kata ya Bugwema na viongozi wao wamemthibitishia Mkuu wa Mkoa huyo kwamba Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ndie chaguo lao pekee la nafasi ya U-Rais wa Taifa letu.
Ujenzi wa Muhoji Sekondari:
Ujenzi ulianza Disemba 2022 kwa kutumia michango ya fedha iliyopatikana kwenye Harambee ya Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo.
Gharama za ujenzi kwa hatua iliyofikiwa:
Tsh 175, 346,955
Wachangia wakuu wa ujenzi wa sekondari hii ni:
(i) Serikali Kuu: Tsh 75 milioni
(ii) Mfuko wa Jimbo: 24.4 milioni
(iii) Wanakijiji: fedha na nguvukazi
(iv) Halmashauri (Musoma DC)
(v) Wazaliwa wa Kijiji cha Muhoji
(vi) Wadau wa Maendeleo
(vii) Mbunge wa Jimbo
Ujenzi unaendelea:
Miundombinu iliyopo ni: vyumba vya madarasa vinne (4), ofisi moja (1) ya walimu, matundu 17 ya vyoo vya wanafunzi na walimu
Miundombinu ya elimu iliyopangwa kuendelea kujengwa ni: vyumba vya madarasa, maabara za masomo ya sayansi, maktaba, chumba cha TEHAMA, Jengo la utawala na nyumba za kuishi walimu
Umeme na Maji ya bomba:
Shule tayari imefungiwa umeme na iko kwenye mradi wa kufungiwa maji ya bomba
Vitabu vya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025:
Vitabu hivyo viwili viwili (Volumes V & VI) vimegawawiwa kwa wananchi na viongozi walioshiriki sherehe hizo.
Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:
Matukio mbalimbali ya uzinduzi wa Muhoji yakiwemo:
(i) RC Mhe Col Evans Mtambi akikata utepe
(ii) Ngoma maarufu ya Liranda ya Kijijini Muhoji
ELIMU NI UHAI WA KILA TAIFA
ELIMU NI UCHUMI WA KILA TAIFA
ELIMU NI USTAWI WA KILA TAIFA
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumatatu, 9 Juni 2025