KISIWA CHA RUKUBA CHAIKUBALI ILANI MPYA YA CCM NA KUAMUA KUJENGA KITUO CHA AFYA
ILANI MPYA YA CCM IMEBEBA VIPAUMBELE VYA MAENDELEO YA KATA YA TEGERUKA
ARI KUBWA YA WANAVIJIJI KUCHANGIA MAENDELEO YAO WAIWEKA PAZURI KATA YA MUGANGO – WANAANZA UJENZI WA MABWENI WAWE NA “HIGH SCHOOL” MWAKANI
ILANI MPYA YA CCM INATOA MAJIBU YA KERO & VIPAUMBELE VYA WANANCHI WA KATA YA NYAMRANDIRIRA
MIKUTANO 3 YA KAMPENI NDANI YA KATA YA NYAMBONO YAMKUBALI SANA DKT MAGUFULI
Leo, Jumanne, 6.10.2020 MGOMBEA UBUNGE wa CCM wa Jimbo la Musoma Vijijini, PROF MUHONGO ameenda Kijijini Nyambono, Kijijini Saragana na kwenye Kitongoji cha Nyabherango KUOMBA KURA za WAGOMBEA wa CCM wa nafasi za Urais, Ubunge na Udiwani.
DKT MAGUFULI anakubalika kwa Asilimia Miamoja (100%). SABABU KUU zikiwa:
(i) MAJI ya ZIWA VICTORIA
Vijiji 2 vya Kata ya Nyambono (Saragana & Nyambono) viko mbali na Ziwa Victoria na hivi karibuni vitapata MAJI ya Ziwa hilo kupitia MRADI wa BOMBA la MAJI wa Suguti-Wanyere/Chirorwe ambapo BOMBA hilo litapaleka MAJI kwenye Vijiji hivyo. Ujenzi wa TENKI kubwa la MAJI kwenye Mlima Nyabherango utaanza hivi karibuni (Bajeti ya Mwaka huu).
(ii) UMEME wa REA:
Vitongoji vya Kata hiyo vilivyosalia vitapewa umeme – ILANI MPYA ya CCM (2020-2025) imebainisha hivyo.
VIPAUMBELE MAALUM
* KIJIJI CHA NYAMBONO
WANANCHI wa Kijiji hiki WAMEAMUA kwa KAULI moja kwamba kwa MIAKA 5 ya UTEKELEZAJI wa ILANI ya CCM (2020-2025) watajenga SEKONDARI yao. Kwa sasa WATOTO wao wanatembea umbali wa zaidi ya KILOMITA 6 kwenda masomoni kwenye SEKONDARI ya NYAMBONO iliyoko Kijijini Saragana.
Vilevile, WANANCHI hawa na WADAU wao wa MAENDELEO watakamilisha ujenzi wa ZAHANATI ya Kijiji chao.
WATOTO wa Kitongoji cha Nyabherango wanaenda masomoni kwenye SHULE za MSINGI za mbali na kwao (zaidi ya kilomita 5). Kitongoji hicho kinatafuta ardhi kianze kujenga SHULE SHIKIZI.
* KIJIJI CHA SARAGANA
Kitongoji cha Kabise kitajenga SHULE SHIKIZI kutatua tatizo sugu la mwendo mrefu ambao WATOTO wao wanatembea kwenda masomoni kwenye SHULE za MSINGI za Vitongoji vingine.
* MIRADI MINGINE ni kama ilivyoainishwa kwenye ILANI MPYA ya CCM ya 2020-2025.
“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA”
Sospeter Muhongo
Jimbo la Musoma Vijijini
6 Oktoba 2020
KAMPENI ZA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI NI KAMPENI ZA UCHUMI & MAENDELEO – KATA YA BUGWEMA ITAENDELEA KUPANUA KILIMO CHA ALIZETI
KATA ya BUGWEMA yenye VIJIJI 4 (Bugwema, Masinono, Muhoji na Kinyang’erere) ndiyo inayoongoza kwenye KILIMO cha MAZAO MCHANGANYIKO (alizeti, pamba, mahindi, mihogo, mpunga, mtama, dengu, vitunguu, nyanya, viazi, n.k.) ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
Jana, wakati wa KAMPENI za CCM kwenye Vijiji vya Bugwema na Masinono, KILIMO kiliwekewa mkazo sana.
Matayarisho ya MRADI mkubwa wa KILIMO cha UMWAGILIAJI kwenye BONDE LA BUGWEMA unaendelea ndani ya SERIKALI yetu.
ELIMU & MAFUNZO ni KIPAUMBELE kingine cha Kata hii ambayo VIJIJI vyake 4 viko mbalimbali. Kwa mfano, kutoka Muhoji hadi Masinono (kwenye SEKONDARI yao ya Kata) ni mwendo usiopungua kilomita 11. Kwa hiyo, SEKONDARI MOJA haitoshi. WANANCHI wamependekeza SEKONDARI 2 MPYA zijengwe kwenye VIJIJI vya Muhoji na Bugwema ndani ya MIAKA 5 ya UTEKELEZAJI wa ILANI MPYA ya CCM (2020-2025).
BARAZA LA MADIWANI liliishaamua kupanua BUGWEMA SEKONDARI na kuwa na “HIGH SCHOOL” ya Wasichana (Bugwema Girls High School). Uamuzi huu UTATEKELEZWA ndani ya MIAKA 5 ya UTEKELEZAJI wa ILANI MPYA ya CCM.
WANANCHI wanayo imani kubwa na SERIKALI ya CCM kuendelea kusambaza UMEME kwenye Vitongoji vilivyosalia.
Ndani ya MIAKA 5 (2020-2025), RUWASA imeahaidi kusambaza MAJI kutoka Ziwa Victoria kwenda kwenye VIJIJI 4 vya Kata hii.
ZAHANATI ya Masinono, yenye GARI la WAGONJWA (Ambulance) walilopewa na Prof Muhongo, IMEPOKEA Tsh MILIONI 400 kutoka SERIKALINI kwa ajili ya upanuzi wake wa kuwa KITUO cha AFYA – KURA za DKT MAGUFULI ni NYINGI kweli kweli!
MASUALA ya UKABILA yamekewa sana na WANANCHI wa KATA ya BUGWEMA wamehaidi kutoa KURA zaidi ya 98% kwa WAGOMBEA wa CCM kwenye nafasi za URAIS (Dkt Magufuli), UBUNGE (Prof Muhongo) na UDIWANI (Ndugu Clifford Machumu).
UTAMADUNI, MICHEZO & SANAA – ILANI MPYA CCM – Kata ya Bugwema iko tayari kwenye UTEKELEZAJI wake
“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA”
Sospeter Muhongo
Jimbo la Musoma Vijijini
4 Oktoba 2020
WANANCHI WA KATA YA MUSANJA WATOA VIPAUMBELE VYAO KWA MIAKA 5 YA UTEKELEZAJI WA ILANI MPYA YA CCM (2020-2025)
Ijumaa, tarehe 2.10.2020, KATA ya MUSANJA yenye VIJIJI 3 (Mabui Merafuru, Musanja na Nyabaengere) ilikuwa kwenye KAMPENI za UCHAGUZI za Chama cha Mapinduzi (CCM)
WAGOMBEA UBUNGE (Prof Muhongo) na UDIWANI (Ndugu Mwira) wa CCM walinadi SERA na MIRADI ya MAENDELEO iliyoko kwenye ILANI MPYA (2020-2025) ya Chama chao.
MIKUTANO 2 ya KAMPENI ilifanywa kwenye VIJIJI 2 (Musanja & Mabui Merafuru).
WANANCHI WALIVUTIWA SANA na SERA za CCM na kuahidi kutoa KURA ZOTE kwa WAGOMBEA wa CCM kwa nafasi ya URAIS (Dkt Magufuli), UBUNGE (Prof Muhongo) na UDIWANI (Ndg Ernest John Mwira).
MIRADI ya KIPAUMBELE ya KATA ya MUSANJA ni:
*Kukamilishwa kwa usambazaji wa UMEME kwenye Vitongoji vilivyosalia
*Kuanza kwa utekelezaji wa Mradi wa MAJI ya kutoka Ziwa Victoria (Chumwi, Kata ya Nyamrandirira) hadi Mabui Merafuru (Kata ya Musanja). Wataalamu walishakamilisha USANIFU wa Mradi huu.
*Ukamilishaji wa ujenzi wa SHULE Shikizi Gomora na kuipanua iwe Shule ya Msingi inayojitegemea.
*Kujenga ZAHANATI 1 kwenye Kijiji 1 kati ya Vijiji 3. Kwa sasa Kata ya Musanja inatumia Kituo cha Afya ya Murangi.
*SEKONDARI kwenye Kijiji cha Musanja ambacho kiko mbali na Sekondari ya Kata iliyoko Kijiji cha Mabui Merafuru
*VITENDO KWANZA
*MAENDELEO KWANZA
VIAMBATANISHO vya hapa:
*Kwaya ya Musanja
*Matukio mengine ya Kampeni
“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE KWA PAMOJA”
Sospeter Muhongo
Jimbo la Musoma Vijijini
3 Oktoba 2020
MIRADI YA UJENZI WA SEKONDARI MPYA TISA (9) ZA KATA ITAKAMILISHWA NA WANANCHI WAKISHIRIKIANA NA SERIKALI YA CCM
Jimbo la Musoma Vijijini lina JUMLA ya SEKONDARI 20 za KATA. Sekondari zote hizi ziko kwenye UJENZI wa MAABARA, MAKTABA, VYUMBA VIPYA VYA MADARASA, OFISI & NYUMBA ZA WALIMU, n.k.
Jimbo la Musoma Vijijini lina UJENZI wa SEKONDARI MPYA TANO (5) za Kata zilizopangwa zifunguliwe mwakani (Januari 2021). SEKONDARI MPYA hizo ni:
(i) Kigera, Kata ya Nyakatende,
(ii) Nyasaungu, Kata ya Ifulifu,
(iii) Ifulifu (inajengwa Kijijini Kabegi), Kata ya Ifulifu,
(iv) Seka, Kata ya Nyamrandirira, na
(v) Bukwaya, Kata ya Nyegina.
Kata hizo 5 zitakuwa na SEKONDARI zaidi ya MOJA ndani ya Kata zao.
*VITENDO KWANZA*
Kata nyingine za Jimbo la Musoma Vijijini nazo zimepanga kuwa na SEKONDARI zaidi ya MOJA ndani ya Kata zao. Kwa hiyo, zimeishafanya maamuzi ya kuanza kujenga SEKONDARI MPYA. Kata hizo ni:
(vi) Suguti, itajenga Sekondari mpya Kijijini Wanyere,
(vii) Tegeruka, Sekondari mpya itajengwa katikati ya Vijiji vya Kataryo na Mayani,
(viii) Etaro, itajenga Sekondari mpya Kijijini Busamba, na
(ix) Mugango, Sekondari mpya itajengwa katikati ya Vijiji vya Kurwaki na Nyang’oma
Ifikapo MWAKA 2025, Jimbo la Musoma Vijijini, lenye Kata 21 litakuwa na:
* SEKONDARI 29 za Kata (Serikali)
* SEKONDARI 2 za Binafsi (SDA & KATOLIKI)
* VETA 1 – maombi yameishapelekwa Serikalini
*MAENDELEO KWANZA*
*CHAGUENI CCM TUKAMILISHE MIRADI YETU
*CHAGUENI DKT MAGUFULI ili TUKAMILISHE MIRADI YETU*
* CHAGUENI PROF MUHONGO & MADIWANI 21 WA CCM wa KATA 21 za Jimbo letu ili TUKAMILISHE MIRADI YETU
PICHA zilizopo hapa zinaonesha ujenzi unaoendelea kwa baadhi ya SEKONDARI MPYA za KATA za Jimbo la Musoma Vijijini.
“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA”
Sospeter Muhongo
Jimbo la Musoma Vijijini
29 Sept 2020
SHULE MPYA 11 ZA MSINGI KUKAMILISHWA NDANI YA MIAKA 5 (2020-2025) – CHAGUA CCM, CHAGUA DKT MAGUFULI MIRADI IKAMILIKE
MWAKA jana (2019) SHULE za MSINGI za Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC), yenye Jimbo la Musoma Vijijini, ziliongoza (NAMBA MOJA) Mkoa wa Mara kwenye MITIHANI ya Darasa la Nne (Std IV).
WANANCHI wa VIJIJI 11 ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini WAMEAMUA kujenga SHULE MPYA 11 za MSINGI kwa madhumuni ya kuongeza UBORA wa ELIMU itolewayo kwenye SHULE za MSINGI za maeneo yao.
Baadhi ya WANAFUNZI wa Shule za Msingi wanatembea umbali mrefu (kati ya kilomita 2 na 5) kwenda masomoni, na kwenye baadhi ya SHULE za MSINGI kuna MIRUNDIKANO mikubwa MADARASANI.
Kwa hiyo, WANANCHI, kwa kutumia NGUVUKAZI zao na kwa KUSHIRIKIANA na SERIKALI ya CCM, wameamua kutatua matatizo haya!
SHULE SHIKIZI 11 zinajengwa kwenye VIJIJI 11 vya Jimbo hili. Baadhi ya SHULE hizi tayari zina MADARASA ya AWALI na zimeanza kutoa MASOMO ya Darasa la Kwanza na Pili (Std I & II).
Ndani ya MIAKA 5 ya UTEKELEZAJI wa ILANI ya CCM (2020-2025), SHULE hizi 11 zitaendelea kujengwa na kukamilishwa, yaani kuwa SHULE za MSINGI kamili.
*CHAGUA CCM,
*CHAGUA MAENDELEO KWA VITENDO
ORODHA YA SHULE SHIKIZI ZINAZOJENGWA:
(1) Binyango: Kijijini Kabegi, Kata ya Ifulifu
(2) Buanga: Kijijini Buanga, Kata ya Rusoli
(3) Buraga Mwaloni: Kijijini Buraga, Kata ya Bukumi
(4) Egenge: Kijijini Busamba, Kata ya Etaro
(5) Gomora: Kijijini Musanja, Kata ya Musanja
(6) Kaguru: Kijijini Bugwema, Kata ya Bugwema
(7) Karusenyi: Kijijini Mikuyu, Kata ya Nyamradirira
(8) Rwanga: Kijijini Kasoma, Kata ya Nyamradirira
(9) Mwikoko: Kijijini Chitare, Kata ya Makojo
(10) Kihunda: Kijijini Kamguruki, Kata ya Nyakatende
(11) Ziwa: Kijijini Mwiringo, Kata ya Busambara
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, PROF MUHONGO ni sehemu ya MAFANIKIO ya UJENZI wa SHULE SHIKIZI hizi. Baada ya UCHAGUZI ataendelea KUSHIRIKIANA na WANANCHI na SERIKALI ya CCM kukamilisha ujenzi wa SHULE hizi.
PICHA zilizoko hapa zinaonyesha baadhi ya SHULE SHIKIZI zinazojengwa ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA.”
Sospeter Muhongo
Jimbo la Musoma Vijijini
ELIMU & MAFUNZO – MAKTABA ZAJENGWA KWENYE SHULE ZA MSINGI ZA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI
JIMBO la Musoma Vijijini tayari linatekeleza ILANI MPYA ya CCM (2020-2025) kwa SHULE za MSINGI kujenga MAKTABA zao.
(1) SHULE YA MSINGI RUKUBA
Hii iko Kata ya Etaro. MAKTABA imekamilika na inatumika. Ujenzi wake ni mafanikio ya USHIRIKIANO wa WANANCHI, PCI (USA – vifaa vingi vya ujenzi), PROF MUHONGO (Saruji Mifuko 50) na UONGOZI wa SHULE. VITABU vya Maktaba vilitolewa na Prof Muhongo.
VIAMBATANISHO – Picha za Jengo lenye Mabati Meupe (Maktaba) baadhi ya vitabu vimeshakabidhiwa
(2) SHULE YA MSINGI BUTATA
Hii iko Kata ya Bukima. Ujenzi wake ni mafanikio ya USHIRIKIANO wa MiCHANGO ya WANANCHI, PCI (USA – vifaa vingi vya ujenzi), PROF MUHONGO (Saruji Mifuko 50) na UONGOZI wa SHULE. VITABU vya Maktaba vitatolewa na Prof Muhongo na PCI (USA).
(3) SHULE YA MSINGI BUSAMBA
Hii iko Kata ya Etaro na inajengwa kwa USHIRIKIANO wa WANANCHI, PROF MUHONGO (Saruji Mifuko 60) na UONGOZI wa SHULE
(4) SHULE YA MSINGI BURAGA
Hii iko Kata ya Bukumi. WANANCHI wamemuomba MGOMBEA UBUNGE wa CCM (Prof Muhongo) achangie ujenzi wake baada ya Uchaguzi wa tarehe 28.10.2020. Amepokea OMBI hilo na kukubali kushirikiana na Wananchi hao.
(5) SHULE YA MSINGI BUIRA
Hii iko Kata ya Bukumi. Ujenzi wake unafanana na ule wa S/M BURAGA (soma hapo juu).
(6) AGAPE PRIMARY SCHOOL
Hii ni SHULE ya PRIVATE (Binafsi) iliyoko kwenye Kata ya Bukima na inajenga JENGO la TEHAMA (angalia Kiambatanisho – Picha za Jengo lenye mabati ya rangi ya kijani).
PROF MUHONGO alishachangia VITABU vya MAKTABA na Saruji Mifuko 50 ya ujenzi wa Jengo la Tehama la Shule hii, na alihaidi kuchangia COMPUTERS.
SHULE NYINGINE za MSINGI za JIMBO la Musoma Vijijini zimeweka MIPANGO ya ujenzi wa MAKTABA zao.
PROF MUHONGO aligawa VITABU vingi vya MAKTABA kwenye SHULE zote za MSINGI za JIMBO hili (111 za Serikali & Agape ya Binafsi).
ILANI MPYA CCM (Elimu & Mafunzo) TAYARI INATEKELEZWA ndani ya JIMBO la Musoma Vijijini
*VITENDO KWANZA
*MAENDELEO KWANZA
Sospeter Muhongo
Jimbo la Musoma Vijijini
27 Sept 2020
CHAGUENI CCM NCHI IZIDI KUNG’ARA – SHAIRI KUTOKA KIJIJI CHA KASOMA
WANANCHI wa Kata ya Nyamrandirira yenye VIJIJI 5 wamewaomba Prof SOSPETER MUHONGO (Mgombea Ubunge) na Mwl NYEOJA WANJARA (Mgombea Udiwani) waungane nao tarehe 5 Novemba 2020 kukamilisha MAJENGO ya AWALI yanayohitajika ili SEKA SEKONDARI ifungiliwe Januari 2021.
VIJIJI 5 (Chumwi, Kaboni, Kasoma, Mikuyu na Seka) vya Kata ya Nyamrandirira vinayo SEKONDARI MOJA (Kasoma Secondary School) ambayo kwa sasa imeelemewa na WINGI wa WANAFUNZI kutoka kwenye vijiji hivyo. WANAFUNZI wengine wanatembea mwendo wa zaidi ya kilomita 10 kwenda masomoni Kasoma Sekondari.
Kwa hiyo, KATA hiyo imeamua kuanza KUTEKELEZA ILANI MPYA YA CCM (2020-2025) kwa KUKAMILISHA UJENZI wa MIUNDOMBINU INAYOHITAJIKA kwa ufunguzi wa SEKONDARI yao mpya (Seka Secondary School) inayojengwa Kijijini Seka.
Sospeter Muhongo
Jimbo la Musoma Vijijini
25.9.2020
MIRADI YA MAENDELEO YA KATA YA NYAKATENDE ITAKAMILISHWA NA CCM
CCM YAENDELEA KUNG’ARA NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI
JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI – ILANI MPYA YA UCHAGUZI YA CCM (2020-2025) KUANZA KUTEKELEZWA TAREHE 1 NOVEMBA 2020
JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI – USAMBAZAJI WA MABANGO, VIPEPERUSHI & VITABU VYA TAARIFA ZA UTEKELEZAJI WA ILANI ILIYOPITA
PROF. MUHONGO ARUDISHA FOMU ZA MAOMBI YA KUGOMBEA NAFASI YA UBUNGE WA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI
PROF MUHONGO ACHUKUA FOMU YA KUWANIA UTEUZI WA CCM KWA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI
PLAU NYINGINE 50 KUGAWIWA KWA VIKUNDI VINGINE 50 VYA WAKULIMA WA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI
WATOTO CHINI YA MIAKA 6 WAJENGEWA SHULE VIJIJINI MWAO
SEKONDARI MPYA ZINADAIWA VYUMBA VIPYA VYA MADARASA KWA AJILI YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA CHA MWAKANI (2021)
UJENZI WA WODI YA MAMA NA MTOTO KISIWANI RUKUBA
WANANCHI KISIWANI RUKUBA WAJENGA MSINGI WA JENGO LA WODI YA MAMA NA MTOTO LENYE VYUMBA 13 KWA MUDA WA WIKI MOJA
UBORESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA VIJIJINI UNAFANYWA KWA USHIRIKIANO MZURI WA SERIKALI NA WANAVIJIJI
SERIKALI YATOA SHILINGI MILIONI 400 KUJENGA KITUO CHA AFYA NA WANANCHI WAJIONGEZA ILI KUPATA MIUNDOMBINU ZAIDI
ZAWADI YA EID AL FITR: PLAU 40 KWA VIKUNDI 40

Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo akitoa ZAWADI yake ya Eid al Fitr ya PLAU 40 kwa VIKUNDI 40 vya Jimbo la Musoma Vijijini. Katibu wa CCM Wilaya ya Musoma Vijijini, Ndugu Peter Francis Mashenji aliambatana na Mbunge huyo kwenye zoezi hilo la kugawa PLAU hizo lilofanyika jana (24.5.2020) Vijijini Kusenyi (Kata ya Suguti), Kwibara (Kata ya Mugango) na Mkirira (Kata ya Nyegina).
UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM (2015-2020) NA UJENZI WA OFISI YA CCM WILAYA YA MUSOMA VIJIJINI
WANAVIJIJI WAAMUA KUJENGA VYUMBA VIPYA 5 VYA MADARASA NA SERIKALI YACHANGIA UJENZI HUO
KATA YA BWASI YAENDELEA KUBORESHA KILIMO CHA UMWAGILIAJI
WANAKIJIJI WANAJENGA MAKTABA, VYUMBA VIPYA VYA MADARASA NA OFISI YA WALIMU KWA WAKATI MMOJA
UJENZI WA SHULE MPYA SHIKIZI KUTATUA MATATIZO YA UMBALI MREFU WA KUTEMBEA NA MIRUNDIKANO MADARASANI
WANAVIJIJI WAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI, PCI NA CRDB KUBORESHA MIUNDOMBINU YA SHULE ILIYOFUNGULIWA MWAKA 1956
UTUMIAJI WA MAJEMBE YA KUKOKOTWA NA NG’OMBE (PLAU) WAONGEZA UFANISI KWENYE KILIMO VIJIJINI
SHULE YENYE WANAFUNZI 187 KWENYE CHUMBA KIMOJA CHA DARASA YACHANGIWA KUJENGA VYUMBA VIPYA VYA MADARASA
SHULE ZA MSINGI ZA MUSOMA VIJIJINI ZAANZA KUJENGA MAKTABA
SEKONDARI MPYA ILIYOFUNGULIWA MWAKA HUU (2020) YAJITAYARISHA KUPOKEA WANAFUNZI WAPYA MWAKANI (2021)
MATATIZO SUGU YA MIRUNDIKANO MADARASANI NA UMBALI MREFU WA KUTEMBEA YAENDELEA KUTATULIWA MUSOMA VIJIJINI
PROGRAMU YA KUBORESHA KILIMO NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI
BENKI YA CRDB YACHANGIA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA S/M MURUNYIGO
WANAFUNZI 157 WA KIDATO CHA KWANZA HAWATARUNDIKANA MADARASANI
ZAHANATI KWA KILA KIJIJI – KATA YA NYEGINA YATEKELEZA ILANI YA CCM
WALEMAVU KWIKUBA GROUP WAPOKEA MKOPO USIOKUWA NA RIBA KUTOKA HALMASHAURI YAO
SHULE YA MSINGI MURANGI B YAKARIBIA KUACHANA NA DARASA NA OFISI CHINI YA MITI
MATATIZO YA UMBALI MREFU WA KUTEMBEA NA MIRUNDIKANO YA WANAFUNZI MADARASANI YAENDELEA KUTATULIWA
OFISI YA CCM YA WILAYA YA MUSOMA YAANZA KUJENGWA
SHULE YA MSINGI MKAPA YA KIJIJINI KASTAM IMEAMUA KUTATUA TATIZO LA MIRUNDIKANO MADARASANI
KIJIJI CHA ETARO CHAJIWEKA SAWA KUMALIZA TATIZO LA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA
UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA UBORESHAJI WA KIWANGO CHA ELIMU NDANI YA MKOA WA MARA
SIKU YA WANAWAKE DUNIANI: MIKOPO ISIYOKUWA NA RIBA YAENDELEA KUTOLEWA
HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA YASHIRIKIANA NA PCI KUSHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
MAAZIMIO YA KONGAMANO (23.3.2020) LA UBORESHAJI WA KIWANGO CHA ELIMU NDANI YA MKOA WA MARA
WATOTO WADOGO WA KIJIJI CHA BURAGA KUEPUKA KUTEMBEA KILOMITA 4-5 KWENDA MASOMONI
WANAVIJIJI WAAMUA SEKONDARI MPYA INAYOJENGWA IWE NA MIUNDOMBINU YA AWALI IFIKAPO TAREHE 1 MEI 2020
WADI YA MAMA NA MTOTO YACHANGIWA SARUJI MIFUKO 200
MBUNGE WA JIMBO AENDELEA KUKAGUA UJENZI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU KWENYE SEKONDARI ZA KATA
SEKONDARI MPYA JIMBONI KUONGEZA KASI KWENYE UJENZI WA MIUNDOMBINU MIPYA
ZAHANATI YA KIJIJI CHA MASINONO KUPANULIWA NA KUWA KITUO CHA AFYA CHA KATA YA BUGWEMA
SHEREHE ZA UZINDUZI WA BUSAMBARA SECONDARY SCHOOL ZAFANA SANA
KIRIBA SEKONDARI – UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA KUTATULIWA KWA USHIRIKIANO WA WANANCHI NA SERIKALI
MADARASA CHINI YA MITI LAZIMA YATOWEKE – KIJIJI CHA BWASI KIMEAMUA
KATA YENYE VIJIJI 4 YAAMUA KUJENGA SEKONDARI YA PILI
WANAVIJIJI WADHAMIRIA KUACHANA NA JEMBE LA MKONO
VYUMBA VIPYA VYA MADARASA VINAVYOJENGWA VITAWATOA WANAFUNZI CHINI YA MITI
KIJIJI CHA BUTATA CHAENDELEA KUTEKELEZA ILANI YA CCM – ZAHANATI MOJA KILA KIJIJI
SEKONDARI MPYA ZAENDELEA KUJENGWA JIMBONI MWETU
SHULE YA MSINGI ILIYOFUNGULIWA MWAKA 1942 YAOMBA MICHANGO ZAIDI KUTOKA KWA MBUNGE WA JIMBO
MRADI WA BMZ (UJERUMANI) WASAIDIA WATOTO WENYE ULEMAVU KWENYE KATA 10 ZA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI
WANAVIJIJI WAITIKIA MWITO WA KUTATUA TATIZO LA MIRUNDIKANO MADARASANI
WANAFUNZI WENGINE NAO WAEPUKA KUTEMBEA UMBALI UNAOZIDI KM 10 KWENDA MASOMONI KATA YA JIRANI
SEKONDARI MPYA ZAONYESHA UBORA WA MIUNDOMBINU YA ELIMU VIJIJINI MWETU
WANAVIJIJI WA KATA YA BULINGA WAKUBALI KUTATUA TATIZO LA MRUNDIKANO WA WANAFUNZI MADARASANI
PROF MUHONGO AWEZESHA UWEKAJI WA UMEME KWENYE JENGO LA CCM LA WILAYA YA MUSOMA VIJIJINI
VIJIJI VYAGAWANA KAZI KUHARAKISHA UJENZI WA VYUMBA VIPYA VYA MADARASA NA OFISI ZA WALIMU
KATA YA NYAMRANDIRIRA YAAMUA KUJENGA SEKONDARI YAKE YA KATA
WASAGA FC YAENDELEZA MATUMAINI YA KUWA MABINGWA WA MKOA
MBUNGE WA JIMBO AIWEZESHA TIMU YA KIJIJI CHA KASOMA KUSHIRIKI LIGI DARAJA LA 3
KIKUNDI CHA WAZALIWA WA KIJIJI CHA RUSOLI CHAENDELEA KUBORESHA UBORA WA SHULE ZA KIJIJINI MWAO
MZALIWA WA KIJIJI CHA BUKIMA AANZISHA SHULE YA MSINGI KIJIJINI MWAO – YAZINDULIWA RASMI LEO
HAYUPO MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2020 (wamechaguliwa 3,502) ATAKAYEBAKI NYUMBANI
MICHEZO JIMBONI – UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM YA 2015-2020
MASHINDANO YA KUPIGA KASIA 2019 (THE ANNUAL BOAT RACE)
Jumapili, 29.12.2019
Jimbo la Musoma Vijijini
KIPAUMBELE Na. 5 (Michezo na Utamaduni) cha Jimbo la Musoma Vijijini kinaendelea kutekelezwa na kesho, Jumatatu, 30.12.2019 kuna MASHINDANO YA KUPIGA KASIA Kijijini Bukima, Kata ya Bukima.
MASHINDANO hayo, kama yalivyo ya KWAYA (Nyimbo), NGOMA za ASILI na MPIRA wa MIGUU ni sehemu ya UTEKELEZAJI wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020, ndani ya Jimbo letu (Rejea Kitabu cha Kurasa 110 cha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani hiyo: Januari 2016 – Juni 2019, Jimbo la Musoma Vijijini).
Matayarisho ya MASHINDANO hayo yamekamilika.
MAHALI:
Mwalo (Ufukwe) wa Kijiji cha Bukima
SIKU:
Jumatatu, 30.12.2019
MUDA:
Timu zinazoshindana zitawasili MWALONI (ufukweni) Bukima Saa 2.30 Asubuhi
UKUBWA WA TIMU:
Wapiga kasia 5 kwa kila MTUMBWI (Timu)
USALAMA:
Taratibu za usalama majini (ziwani) zitazingatiwa.
KATA ZILIZOJIANDIKISHA kushiriki kwa ridhaa zao:
(1) Bugwema, (2) Bukima, (3) Bukumi, (4) Bwasi, (5) Etaro, (6) Mugango, (7) Murangi, (8) Musanja, (9) Nyakatende, (10) Rusoli na (11) Suguti
ZAWADI KWA WASHINDI
*Mshindi wa 1
Tsh Milioni 1 & Kikombe
*Mshindi wa 2
Tsh 700,000 & Kikombe
*Mshindi wa 3
Tsh 400,000 & Kikombe
*Kifuta jasho kwa WASHIRIKI ambao hawatashinda: Tsh 50,000 kwa Timu.


















































































































































































































