JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Mh. Mbunge, Prof. Sospeter Muhongo
"Tovuti Rasmi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo, Kwaajili ya Kuwasiliana na Wananchi Jimboni "
UCHUNGUZI NA MJADALA WA HALI YA ELIMU NA MAPENDEKEZO
YA UBORESHAJI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA
TAARIFA YA AWALI
A CONCISE PROFESSIONAL CV OF PROF. SOSPETER MWIJARUBI MUHONGO
CONCISE CV:
Prof Dr. rer. nat. Sospeter Mwijarubi Muhongo
He is a very distinguished world-class scholar, a Chartered and a European earth scientist. He
writes and speaks fluent Kiswahili, English, and German languages. His French is basic.
Recognition by the world's topmost learned professional societies:
*Honorary Fellow, Geological Society of London (est. 1807), HonFGS
*Honorary Fellow, Geological Society of America (est.1888), HonFGSA
*Honorary Research Fellow, Chinese Academy of Geological Sciences (est. 1956),
HonRFCAGS
Top international professional services & leadership:
*Former Vice President of the Commission of the Geological Map of the World (CGMW)
*Former Chair of the Science Programme of the UN-proclaimed International Year of Planet
Earth (UN-IYPE)
*Former Chair of UNESCO-IUGS-IGCP Scientific Board of International Geoscience
Programme
*Former President of the Geological Society of Africa (GSAf)
*Former Regional Director (Africa) for the International Council of Scientific Unions (ICSUROA)
*Editor-in-Chief Emeritus, JAES, Elsevier
*Selecting Expert: UNESCO & TWAS international science awards
Top National Leadership:
*Member of Parliament of the Musoma Rural Constituency
*Former Minister for Energy and Minerals
*Former Chair of the State Mining Corporation (STAMICO) Board of Directors
*Former Head of the Department of Geology of the University of Dar es Salaam
Fellowships & Recognitions in abbreviation:
Prof Dr.rer.nat. Sospeter M Muhongo
Officer, Ordre Palmes Academìques
FGSAf, FAAS, MASSAf, FASI, FASSAf, FTAAS, FGIGE, FTWAS, HonRFCAGS, HonFGSA,
HonFGS, CGeol, EurGeol
For additional information:
www.musomavijijini.or.tz
Date:
Thursday, 10 April 2025
MSIKILIZE PROF. SOSPETER MWIJARUBI MUHONGO

JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI: VITABU VIPYA VYA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM
Vitabu vipya viwili vya rangi vya Jimbo la Musoma Vijijini vinavyoelezea Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025 vinachapishwa na vitaanza kugawiwa bure kuanzia tarehe 30.5.2025
Vitabu hivyo ni:
*Volume VI (Mwaka wa Fedha 2023/2024), 102pp
*Volume V (Mwaka wa Fedha 2022/2023), 86pp
Kitabu cha Mwaka wa Fedha 2024/2025 (Volume VII) kitachapishwa baada ya tarehe 30.6.2025
Vitabu vingine vya Jimbo hili ambavyo vimechapishwa na kugawiwa bure ni: Volumes I, II, III na IV.
Vitabu vyote hivi vinaelezea miradi inayobuniwa na kuanza kutekelezwa na wanavijiji na Mbunge wao, na baadae Serikali huchangia ukamilishaji wa miradi ambayo ni ya wanavijiji.
Orodha ya wachangiaji wa kila mradi imetolewa, na imetunzwa na kila serikali ya kijiji yenye mradi unaotekelezwa
Vilevile, miradi inayotekelezwa kwa asilimia 100 (100%) na Serikali nayo imeelezwa.
Tovuti ya Jimbo:
Vitabu vyote hivyo na taarifa nyingine muhimu za maendeleo na ustawi wa Jimbo la Musoma Vijijini vinapatikana kwenye Tovuti hiyo ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz
Picha iliyoambatanishwa hapa inaonesha:
Vitabu 2 vipya vya Utekelezaji wa Ilani ya CCM ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini vitakavyoanza kugawiwa bure tarehe 30.5.2025
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumapili, 18 May 2025
Matukio katika picha - (Toa Maoni Hapa)
Habari Mpya Toka Jimboni
TAARIFA MPYA JUU YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO JIMBONI MWETU --MPYA--
(1) BARABARA
1a. Musoma-Makojo-Busekera
*TANROADS wako kwenye utaratibu wa manunuzi kwa ajili ya uwekaji lami kwenye barabara hili ambalo Serikali imeamua kulijenga kwa awali mbili.
*Nimewasisitizia (Mbunge wa Jimbo) kwamba ujenzi unaotafutiwa Mkandarasi uwe wa kuendeleza ujenzi wa Lot 2 (Kusenyi-Makojo-Busekera) ambapo kilomita 5 za lami zilijengwa kwa miaka minne (4)!
1b. Utengenezaji wa barabara la Musoma-Mugango-Makojo-Busekera
*TANROADS Mkoa wameanza matengenezo ya uboreshaji wa barabara hili kwa kipande cha Musoma-Mugango
(2) KILIMO CHA UMWAGILIAJI
2a. BONDE LA BUGWEMA
*"Consultant" ameanza kufanya "feasibility study" (tarehe 17.9.2023 - 16.10.2023). Nimempa taarifa kwamba nitawatembelea wakiwa kazini Bugwema.
*Mazao makuu yatakayoliwa kwa umwagiliaji ni: mahindi, mpunga, alizeti, dengu, pamba na mboga mboga
2b. BONDE LA SUGUTI
*"Consultant" atafanya "feasibility study" baada ya kukamilisha kazi kwenye Bonde la Bugwema
3. ELIMU
3a. ELIMU YA SEKONDARI - MAABARA
*Tunaendelea na ujenzi wa maabara 3 (Physics, Chemistry & Biology) kwa kila Sekondari. Tuendelee kuchangia ujenzi huu na tunashukuru kila mara Serikali inapotuunga mkono kwa michango yake mikubwa
*Halmashauri yetu (Musoma DC) iendelee kukumbushwa kuchangia ujenzi wa maabara 3 kwenye kila Sekondari yetu ya Kata (kwa saa tunazo 25 na tunajenga mpya 5. Sekondari za Binafsi ni 2)
3b. SCIENCE HIGH SCHOOLS
*Tunaendelea kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu muhimu inayotakiwa kwenye uanzishwaji wa science high schools.
*Vinavyohitajika kwa uanzishwaji wa "science high school" ni: maji ya bomba, umeme, maabara 3, bweni, na bwalo la chakula.
*Lengo letu ni mwakani, 2024, Jimbo letu liwe na angalau HIGH SCHOOLS 2-3 za masomo ya sayansi. Ile ya Kasoma ni ya masomo ya "arts."
3c. ELIMU YA MSINGI - MRADI WA BOOST
*Shule za Msingi tisa (9) zimepewa jumla Tsh bilioni 1.35 kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu kwenye shule hizo.
*Wananchi, Mbunge wa Jimbo na Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya waendelee kufuatilia mradi huu kwa ukaribu sana.
*Shule za Msingi zilizopewa fedha ni: Bugoji, Buira, Bulinga B, Kanyega, Kataryo B, Kigera B, Mabuimerafuru B, Masinono na Nyambono B
4. MAJI YA BOMBA KUTOKA ZIWA VICTORIA
4a. Maji ya MUWASA kupelekwa kwenye Kata za Etaro, Nyegina, Nyakatende na Ifulifu
*MUWASA inaendelea kukusanya baadhi ya vifaa hitajika kwa kutumia vyanzo vyake vya fedha.
*Vilevile, MUWASA imewasilisha Serikalini Bajeti ya kutekeleza mradi huu
*MUWASA imeishaanza kusambaza maji ya bomba kwa baadhi ya maeneo ya kata hizi
*Kijiji cha Nyasaungu cha Kata ya Ifulifu kimeanza kupata maji ya bomba kutoka kwenye bomba la zamani la Mugango-Kiabakari-Butiama
4b. Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama
*Ujenzi umekamilika kwa asilimia 92 (92%) na ifikapo Disemba 2023 kazi zote muhimu zitakuwa zimekamilishwa
4c. MIUNDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI NDANI YA KATA YA TEGERUKA
*Maji ya bomba kwenye Kata hii yatatoka kwenye Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama
*Mabomba yametandazwa ndani ya vijiji vyote vitatu vya Kata hii, ambavyo ni Kataryo, Mayani na Tegeruka
*Tenki la ujazo wa LITA 135,000 tayari linakamilishwa ujenzi kijijini Mayani
4d. MIUNDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI NDANI YA KATA YA MUGANGO
*Kata hii nayo itapata maji ya bomba kutoka kwenye Bomba la Mugango- Kiabakari-Butiama
*Mabomba yamesambazwa kwenye vijiji vyote vitatu vya Kata hii, ambavyo ni Kwibara, Kurwaki na Nyang'oma.
*Tenki la ujazo wa LITA 500,000
limejengwa kwenye Mlima Kong'u kijijini Nyang'oma
4e. MINDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI KWENYE KATA ZA BUSAMBARA NA KIRIBA
*Maji ya bomba ya Kata hizi mbili yatatoka kwenye Tenki ya LITA 500,000 liliojengwa Mlimani Kong'u. Maji yake yatatoka kwenye Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama
*RUWASA imepata vibali vyote hitajika kutoka Serikalini, na ndani ya miezi miwili miundombinu ya usambazaji maji ya bomba ndani ya Kata hizi itaanza kujengwa.
4f. MINDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI KWENYE KATA YA BWASI
*Vijiji vyote vitatu vya Kiti hii, yaani Bwasi, Bugunda na Kome vinatandaziwa mabomba ya maji
*Ujenzi wa Tenki la ujazo wa LITA 150,000 tayari limekamilishwa Kijijini Bwasi
4g. MINDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI YA BOMBA KWENYE VIJIJI VYA CHUMWI & MABUIMERAFURU
*Ujenzi wa Tenki la ujazo wa LITA 300,OOO umekamilika kijijini Mabuimerafuru
*Mabomba yanaelendelea kutandazwa
*Maji kutoka kwenye Tenki hili yatasambazwa kwenye vijiji vya Masinono na Bugwema (Kata jirani ya Bugwema)
4h: MAJI YA KISIMA CHA RUSOLI SEKONDARI
*Tunaendelea kuwashukuru baadhi ya WAZALIWA wa RUSOLI kwa ufadhili wa uchimbaji wa kisima hiki.
*RUWASA imekamilisha ujenzi wa Tenki la LITA 75,000 kwa ajili ya usambazaji wa maji kijijini hapo.
5. AFYA
5a. HOSPITALI ya Halmashauri yetu yenye hadhi ya Hospital ya Wilaya imeanza kutoa HUDUMA za AFYA hapo ilipojengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijijini Suguti.
*Hospitali hii inavyo vifaa tiba vya kisasa sana, ikiwemo Digital X-ray, Ultrasound, Vifaa vya Upasauji, Mitambo ya kutengeneza Oxygen.
5b. VITUO VYA AFYA
*Kwa sasa tuna jumla ya Vituo vya Afya sita (6) ambavyo ni: (i) Murangi, (ii) Makojo (mpya), (iii) Kiriba (mpya), (iv) Kisiwa cha Rukuba (Zahanati yake imepanuliwa), (v) Mugango (Zahanati yake imepanuliwa), na (vi) Bugwema (ilikuwa Zahanati ya Masinono, imepanuliwa)
5c. ZAHANATI
*Tuna jumla ya Zahanati 42
*Zahanati 24 zinatoa Huduma za Afya vijijini mwetu
*Zahanati 14 zinaendelea kujengwa na baadhi karibu zitakamilishwa ujenzi.
*Zahanati 4 za Binafsi zinatoa Huduma za Afya vijijini mwetu.
5d. MAGARI YA WAGONJWA (AMBULANCES)
*Tunayo magari ya kusafirishia wagonjwa (ambulances) matano (5). Mbunge wa Jimbo ndiye aliyefanikisha upatikaji wa ambulances hizi.
*Ambulance iliyoko Kituo cha Afya cha Murangi ni ya kisasa ambayo upasuaji unaweza kufanyika wakati mgonjwa akiwa anasafirishwa. Serikali ya Japan ilimpatia Mbunge wa Jimbo ambulance hii.
*Ambulance nyingine nne (4) zilinunuliwa na Mbunge wa Jimbo akishirikiana na rafiki zake.
*Tunaendelea kufuatilia miradi ya usambazaji UMEME vijijini mwetu (REA & TANESCO). Miradi ya REA itaanza hivi karibuni
*Tunaendelea kufuatilia miradi ya ujenzi na uboreshaji wa barabara zetu vijijini (TARURA & TANROADS)
*Tunaendelea kufuatilia uboreshaji wa miundombinu ya usambazaji maji ya bomba vijijini mwetu (RUWASA & MUWASA)
Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz
SHUKRANI
Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na WADAU wengine wa uchangiaji wa Maendeleo na Ustawi wa Jimbo letu wanapewa shukrani nyingi sana - tafadhali endeleeni kutuunga mkono.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumatano, 20.9.2023
TAARIFA ZA MIRADI MBALIMBALI YA MUSOMA VIJIJINI
1. Barabara ya Musoma-Makojo-Busekera (km 92)
*Ujenzi wa kilomita 5 (Kusenyi hadi Suguti, Kwikonero) umekamilika wiki jana
*Ujenzi wa kilomita 87 zilizosalia:
Ombi liko ndani ya Wizara la kushawishi Mradi huu wa KM 87 uwekwe wote kwenye Bajeti ya Mwaka unaoanza tarehe 1.7.2023, yaani, Mwaka wa Fedha 2023/2024
2. Maombi ya Mikopo ya UVUVI
*Tulituma jumla ya maombi 10 yakiwa ya: (i) boti za uvuvi na (ii) vizimba vya uvuvi.
*Taarifa niliyopewa (Mbunge) ni kwamba sehemu kubwa ya maombi yetu imekubalika.
*Wapo watakaopata mikopo ya boti yenye thamani ya kati ya Tsh Milioni 16 na 72
*Wapo watakaokopeshwa vizimba 8 vyenye thamani ya Tsh Milioni 130
*Orodha na maelekezo ya upokeaji wa mikopo hiyo utatolewa hivi karibuni na Wizara husika.
3. Ujenzi wa VETA Musoma Vijijini
*Serikali imeamua kujenga VETA moja kwa kila Wilaya
*Sisi Wilaya yetu inayo VETA hapo Mwisenge, Musoma Mjini. Hii ilikuwa VETA ya Mkoa wa Mara, sasa inakuwa VETA ya Wilaya ya Musoma.
*Wizara imeshawishiwa na kuona umuhimu wa Musoma Vijijini kupata VETA yake.
Tumeombwa tukabidhi VETA MAKAO MAKUU eneo lililoainishwa kwa ajili ya ujenzi wa VETA tunayoiomba.
Mbali ya ufinyu wa Bajeti, Wizara itajitahidi kutafuta fedha za ujenzi wa VETA ya Musoma Vijijini. Halmashauri itekeleze hili!
4. Minara mipya ya Mawasiliano
Ombi letu linafanyiwa kazi, pamoja na maombi mengine ya nchini kote. Tutajulishwa.
5. Ujenzi wa Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba
*Taarifa ya uamuzi wa Wakazi wa Rukuba kuwa na Sekondari yao hapo Kisiwani imefikishwa kwa Wahusika TAMISEMI, na hakuna kuzuizi cho chote kilichopo.
*Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba waanze matayarisho ya mradi huu. Mbunge wa Jimbo ataenda huko kupiga Harambee ya ujenzi wa Rukuba Sekondari.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Alhamisi, 9.2.2023
Kalamu ya Mh. Mbunge, Prof. Sospeter Muhongo
RUKUBA ISLAND SECONDARY SCHOOL: MABATI YA RANGI 130 KUTOKA NYANSAHO FOUNDATION
Mhe DC Juma Chikoka kukabidhi mabati:
Kesho, Alhamisi, 12 Juni 2025, Saa 5 asubuhi, Mhe Juma Chikoka, Mkuu wa Wilaya Musoma, atakabadhi Mabati 130 ya rangi kwa ajili ya ujenzi wa "Rukuba Island Secondary School"
Nyansaho Foundation:
Ofisi ya Kanda ya Foundation hii ya Mjini Mugumu imenunua mabati hayo ikiwa ni mchango wake kwenye ujenzi wa sekondari hiyo.
Kata ya Etaro yenye sekondari moja ya Kata, kwa sasa inajenga sekondari mbili - ya Kijijini Mmahare na ya Kisiwani Rukuba.
SHUKRANI
Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba na Viongozi wao akiwemo Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini wanatoa shukrani nyingi kwa Dr Rimo Nyansaho kwa mchango huu muhimu sana uliotolewa na Foundation yake - Ahsante sana!
ELIMU NI UHAI WA KILA TAIFA
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumatano, 11 Juni 2025
BREAKING NEWS: MUSOMA VIJIJINI - HIGH SCHOOLS ZA SCIENCE KUANZA TAREHE 1.7.2025
Suguti High School: Wanafunzi 158
Mugango High School: Wanafunzi 62
Prof Sospeter Muhongo anaahidi:
*Kutembelea High Schools hizo na kuongea na wanafunzi hao
*Kuwapatia vitabu vya Maktaba vya Masomo ya Sayansi (reference books)
Sekondari zinazokaribia kukidhi vigezo vya uwepo wa High Schools za sayansi ni:
(i) Mtiro Secondari, Kata ya Bukumi
(ii) Makojo Sekondari, Kata ya Makojo
(iii) Bugwema Sekondari, Kata ya Bugwema
(iv) Kiriba Sekondari, Kata ya Kiriba
(v) Nyakatende Sekondari, Kata ya Nyakatende
(vi) Etaro Sekondari, Kata ya Etaro
Vigezo (matakwa) muhimu ni:
*Maabara 3 za masomo ya sayansi
*Bweni
*Bwalo la chakula
*Maji ya bomba
*Umeme
(v) Sekondari mpya zote zilizopata uwekezaji mkubwa kutoka Serikalini zina maabara tatu za masomo ya sayansi. Jumla ni: sekondari 5 zilizoko vijijini Kabegi (Kata ya Ifulifu), Kurwaki (Kata ya Mugango), Wanyere (Kata ya Suguti), Kasoma (Kata ya Nyamrandirira), na Butata (Kata ya Bukima)
Tuendelee kuongeza High Schools za Masomo ya Sayansi Jimboni mwetu!
Tunafanikiwa, tuongeze bidii, maarifa na ubunifu kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya vijijini mwetu!
Sospeter Muhongo (Mb)
Jimbo la Musoma Vijijini
8.6.2025
SHEREHE ZA UZINDUZI WA SEKONDARI MPYA MUSOMA VIJIJINI
Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa sekondari mpya nne Jimboni mwetu. Wanavijiji na Viongozi wao, kwa njia mbalimbali, wameshiriki vizuri kwenye uchangiaji wa ujenzi huu.
Sherehe za uzinduzi wa sekondari mpya:
(i) Butata Sekondari, Kijijini Butata
Hii ni sekondari ya pili ya Kata ya Bukima. Kata hii ina vijiji vitatu.
Sherehe za ufunguzi zimeishafanyika
(ii) David Massamba Memorial Secondary School, Kijijini Kurwaki
Hii ni sekondari ya pili ya Kata ya Mugango. Kata hii ina vijiji vitatu.
Sherehe za ufunguzi zimeishafanyika
(iii) SEKONDARI YA AMALI YA NYAMRANDIRIRA, Kijijini Kasoma
Hii ni sekondari ya tatu ya Kata hii. Kata ina vijiji vitano.
Tarehe ya Sherehe:
Jumamosi, 7 Juni 2025
Saa 4 asubuhi
Mgeni Rasmi: DC Wilaya ya Musoma
(iv) MUHOJI SEKONDARI, Kijijini Muhoji
Hii ni sekondari ya pili ya Kati hii. Kata ina vijiji vinne.
Tarehe ya Sherehe:
Jumatatu, 9 Juni 2025
Saa 4 asubuhi
Mgeni Rasmi: RC Mkoa wa Mara
KARIBUNI NYOTE TUSHEREHEKEE ONGEZEKO KUBWA LA SEKONDARI JIMBONI MWETU
Lengo letu kuu:
Sekondari moja kila kijiji - Wana-Musoma Vijijini mnakaribishwa kuchangia, kwa vitendo, maendeleo ya vijijini mwetu!
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Ijumaa, 6 Juni 2025
LEO BUNGENI DODOMA (Bajeti ya Wizara ya Afya)
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ametoa mchango wake Bungeni akielezea mengi yakiwemo:
*Musoma Vijijini wameamua kujenga zahanati moja kila kijiji. Jumla ya vijiji ni 68
*Taifa lisomeshe vijana wengi kwenye eneo la "radiology" ili matumizi ya vifaa tiba kama CT scan, MRI, X-ray na Ultrasound machine yapate wataalamu wa kutosha.
Taafadhali sikiliza mchango wa Prof Muhongo kutoka kwenye CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumatatu, 2 Juni 2025
Alhuda Newspaper 28/05/2025, PROFESA MUHONGO ANG'ARA UTEKELEZAJI ILANI MUSOMA VIJIJINI
Alhuda Newspaper 28/05/2025
Profesa Muhongo ang'ara utekelezaji ilani Musoma vijijini
Na. Mwandishi Wetu
Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospester Muhongo ametajwa kutekeleza vema aliyoyaahidi jimboni kwake.
Mbunge huyo ambaye pia ni mwanataaluma bobezi ameng'ara kwa namna alivyowatumikia wapiga Kura wake katika kipindi cha miaka mitano inayomalizika.
Utekelezwaji wa ilani ya CCM jimboni Musoma Vijijini umetajwa kuwa wa kitaalamu unaokipa haiba njema Chama cha Mapinduzi kwa Wananchi wa jimbo hilo.
Miradi ya Maji, shule zikijumuisha maabara za masomo ya sayansi, zimempa Mbunge huyo upendo mkubwa miongoni mwa wananchi
Muhongo ambaye Awamu ya Nne mwishoni na Awamu ya tano mwanzoni alikuwa Waziri wa nishati na madini aliyefanya mabadiliko makubwa katika sekta hizo ametajwa kuwa Mbunge aliyetumia wakati mwingine jimboni kwake akishiriki, kusimamia miradi pamoja na kusaidia wananchi wa jimbo hilo katika masuala ya kijamii.
Ili kuweka kumbukumbu, ofisi ya Mbunge huyo, imechapisha vitabu vyenye kuonesha utekelezaji wa ilani ya CCM jimboni humo kwa kipindi cha 20/25.
"Profesa Muhongo ametisha" , ameandika Mwananchi mmoja kwenye ujumbe mfupi akionesha kufurahia kwake kazi nzuri iliyofanywa na Mbunge huyo wa Musoma Vijijini.
Profesa Muhongo aliingia Bungeni mwaka 2015, akachaguliwa kwa kura za kishindo mwaka 2020, utekelezaji wake wa ilani jimboni Musoma Vijijini, umeliweka jimbo hilo kuwa moja ya ngome imara ya Chama hicho katika chaguzi zote.
MATOKEO YA MJADALA WA UBORESHAJI WA UFUNDISHAJI, UJIFUNZAJI, UELEWA NA UFAULU WA SHULE ZA MUSOMA VIJIJINI
Mgeni Rasmi: Ripoti & Zawadi za Ufaulu
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mhe Juma Chikoka alikabidhiwa Ripoti ya Matokeo ya Mjadala huo.
Vilevile, Mkuu huyo wa Wilaya alikabidhi zawadi za ufaulu za aina zifuatazo:
(i) Shule za Msingi na Sekondari zilizofanya vizuri kwenye mitihani ya mwaka jana, 2024
(ii) Shule za Msingi na Sekondari zilizofanya vibaya kwenye mitihani ya mwaka jana (2024) zilipewa "tuzo" ya kuonyesha ufaulu huo mbaya! Lengo ni mwaka huu waachane na "tuzo" hiyo kwa kufanya vizuri.
(iii) Zawadi za utunzaji mzuri wa mazingira zilizotolwa kwa shule za Msingi na Sekondari
Mjadala (The Dialogue):
Timu ya Wataalamu watatu iliendesha Mjadala huo na baadae kutayarisha Ripoti iliyokabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, imeambatanishwa hapa.
Majina ya Wataalamu:
1. Dr. Zablon Kengera, UDSM
2. Dr. George Kahangwa, UDSM
3. Mr Japhet Makongo, Ubunifu Associates
Washiriki:
1. Walimu Viongozi Shule za Msingi (120), wakiwemo Walimu wa Taaluma
2. Walimu Viongozi Shule za Sekondari (32), wakiwemo Walimu wa Taaluma
3. Madiwani 28 wa Musoma Vijijini
4. Viongozi mbalimbali wa Halmashauri wakiwemo Mkurugenzi na Afisa Elimu wa shule za Msingi na Sekondari
Wafadhili wa Mjadala:
1. Prof Sospeter Muhongo, Mbunge
2. Halmashauri ya Wilaya ya Musoma
Muda wa Mjadala:
Siku tatu, tarehe 25-27 Machi 2025
Mijadala ya awali ya aina hiyo:
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, ameishawahi kufadhili mijadali ya aina hii. Hiyo ilikuwa:
(i) 20 Feb 2020: Mjadala wa Mkoa wa Mara
(ii) 3 Feb 2023: Mjadala wa Mbunge na Wakuu wa Sekondari (Headmasters)
Mijadala hii, endelevu, inasaidia wahusika kufanya maboresho stahiki!
Kiambatanisho cha hapa:
Ripoti ya Matokeo ya Mjadala ulioelezewa hapo juu
Mawasiliano:
Dr Zablon Kengera
zkengera@yahoo.com
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumatatu, 19 May 2025


