JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI
Mh. Mbunge, Prof. Sospeter Muhongo
Curriculum Vitae (CV)
Curriculum Vitae (CV)
Matukio katika picha - (Toa Maoni Hapa)
-
MBUNGE WA JIMBO, MH. PROF SOSPETER MUHONGO AKITOA ZAWADI YAKE YA EID AL FITR YA PLAU 40 KWA VIKUNDI 40 VYA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI.
-
UTUMIAJI WA MAJEMBE YA KUKOKOTWA NA NG'OMBE (PLAU) WAONGEZA UFANISI KWENYE KILIMO MUSOMA VIJIJINI
-
MBUNGE WA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI, MH. PROF SOSPETER MUHONGO AKIKAGUA UJENZI WA OFISI YA CCM WILAYA YA MUSOMA VIJIJINI INAYOJENGWA KIJIJINI MURANGI.
Habari Mpya Toka Jimboni
HUDUMA ZA BENKI ZAANZA KUSHAMIRI VIJIJINI MWETU
Benki za CRDB na NMB tayari zina MAWAKALA wanaotoa HUDUMA ndani ya VIJIJI vyetu. Hii ni hatua muhimu kabla ya ujenzi wa MATAWI ya BENKI hizo JIMBONI mwetu.
NMB - MAWAKALA
*Bukima (2) na Mugango
CRDB - MAWAKALA
*Bukima, Mugango Saragana na Seka
NBC - itaanzia Murangi
MAWAKALA WAJAO:
CRDB (Bwai Paris), NMB (Busekela, Bwai Paris, Etaro, Nyambono na Seka)
UJENZI WA OFISI YA CCM (W) KIJIJINI MURANGI
MICHANGO ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo YAFIKIA Tsh MILIONI 12.
Mchanganuo ni huu:
(i) Tsh Milion 6 kulipia gharama za ujenzi (FUNDI).
(ii) Ununuzi wa Saruji Mifuko 200
(iii) Kulipia gharama za ufyatuaji na umwagiliaji wa matofali ya Mifuko 200.
KAMATI YA UJENZI itasimamia ujenzi huu (Mwenyekiti: DC Musoma District)
Kalamu ya Mh. Mbunge, Prof. Sospeter Muhongo
KUONGEZA HIGH SCHOOLS MUSOMA VIJIJINI
* Tunazo High Schools 2 (Kasoma- Serikali na Nyegina-Katoliki)
* Halmashauri imeamua kuboresha baadhi ya Sekondari zetu ziwe na High Schools. Sekondari hizo ni:
(1) Bugwema, (2) Mtiro, (3) Mugango na (4) Mkirira
* Bwasi Sekondari (SDA) imeombwa ianzishe High School.
Tunazo Sekondari 20 (Serikali) na 2 (Binafsi). Tunajenga MPYA 5, na nyingine zitajengwa. Tuanze KUONGEZA HIGH SCHOOLS.
Ofisi ya Mbunge
7.6.2020
MAOMBI YA UMEME WA REA
Mbunge wa Jimbo amewasiliana na REA & TANESCO kwa kusudio la kuongeza kasi ya USAMBAZAJI WA UMEME WA REA Vijijini mwetu.
LETA MAOMBI:
yakitaja MTAA, KITONGOJI na KIJIJI ambacho hakijapata UMEME
TAARIFA zipelekwe OFISI ya MBUNGE:
Fedson:
0623 608 686
Hamisa:
0762 626 881
Verediana:
0763 503 033
Jumatatu, 8 Mei 2020, MBUNGE wa Jimbo atawasiliana na REA kuhusu MAOMBI yetu.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
TUMEANZA UJENZI WA WODI ZA MAMA NA MTOTO
ZAHANATI za VIJIJI vya BUKIMA, NYEGINA na RUKUBA KISIWANI zinajenga WADI hizo.
MICHANGO ya UJENZI inatoka kwa WANAVIJIJI, HALMASHAURI yetu na MBUNGE wa Jimbo
Mbunge wetu, Prof Sospeter Muhongo ameanza kuchangia na atatoa SARUJI MIFUKO 200 kwa kila ZAHANATI (jumla atachangia Mifuko 600). SARUJI ya MBUNGE inatolewa kulingana na KASI YA UJENZI.