UHURU NA KAZI – DHAMIRA YA KIJIJI CHA MUHOJI KUFUNGUA SEKONDARI YAKE MWAKANI IKO PALE PALE

Wanakijiji wakilima barabara ya kuingia shuleni (Muhoji Sekondari)

UHURU NA KAZI - DHAMIRA YA KIJIJI CHA MUHOJI KUFUNGUA SEKONDARI YAKE MWAKANI IKO PALE PALE

Wananchi wa Kijiji cha Muhoji, Kata ya Bugwema wameamua kujenga Sekondari yao (Muhoji Sekondari) na dhamira ya kuifungua shule hiyo Januari 2024 iko pale pale.

Ujenzi wa awali unaokamilishwa ni:
*Vyumba 2 vya madarasa
*Ofisi 1 ya walimu
*Vyoo:
matundu 12 ya wasichana
matundu 12 ya wavulana
matundu 2 ya walimu
*Barabara ya kuingia shuleni kutoka barabara kuu (nguvukazi za wanakijiji)

Wachangiaji wakuu wa ujenzi wa Muhoji Sekondari ni:
*Wananchi wa Kijiji cha Muhoji
*Mbunge wa Jimbo
*Mfuko wa Jimbo
*Wazaliwa watatu (3) wa Kijiji cha Muhoji

Halmashauri yetu (Musoma DC) bado haijachangia cho chote!

TARURA imeombwa isaidie ukamilishaji wa ujenzi wa barabara linaloingia Muhoji Sekondari likitokea barabara kuu la Murangi- Masinono-Manyamanyama (Bunda).

Muhoji Sekondari itakuwa ni Sekondari ya pili ya Kata ya Bugwema yenye vijiji vinne (Bugwema, Kinyang'erere, Masinono na Muhoji).

Sekondari moja (Bugwema Sekondari) kwa Kata hii haitoshi, matatizo makuu yakiwa ni umbali mrefu wa kutembea kwa baadhi ya wanafunzi, na mirundikano madarasani!

Ombi kutoka Kijijini Muhoji:
*Wazaliwa au watu wenye chimbuko la Kata ya Bugwema wanaombwa waungane na ndugu zao kukamilisha ujenzi wa Muhoji Sekondari.

*Wadau wengine wa maendeleo wanaombwa sana wachangie ujenzi wa shule hii.

Michango ya fedha ipelekwe:
Benki: NMB
Akaunti Na: 30302301062
Jina la Akaunti: Serikali ya Kijiji cha Muhoji

Picha zilizoambatanishwa hapa:
*Jengo lenye Vyumba 2 vya madarasa na Ofisi 1 ya walimu
*Wanakijiji wakijenga vyoo vya shule (Muhoji Sekondari)
*Wanakijiji wakilima barabara ya kuingia shuleni (Muhoji Sekondari)

UHURU NA KAZI

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe (Uhuru Day)
Jumamosi, 9.12.2023

Jengo lenye Vyumba 2 vya madarasa na Ofisi 1 ya walimu

Wanakijiji wakijenga vyoo vya shule (Muhoji Sekondari)