UJENZI WA MAABARA TATU ZA MASOMO YA SAYANSI KWENYE SEKONDARI YA MTIRO UNAENDELEA VIZURI

Maendeleo ya ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi kwenye Sekondari ya Mtiro ya Kata ya Bukumi, Musoma Vijijini

Rejea taarifa yetu ya Jumatatu, 6.11.2023 kuhusu umuhimu wa kujenga maabara tatu za masomo ya sayansi kwenye Sekondari ya Mtiro ya Kata ya Bukumi.

Ujenzi wa aina hii unafanyika kwenye Sekondari zote za Jimbo la Musoma Vijijini (25 za Kata/Serikali na 2 za Binafsi za Madhehebu ya Katoliki & SDA)

Ujenzi wa maabara tatu za masomo ya Fizikia, Kemia na Baiolojia unaendelea vizuri kwenye Sekondari ya Makojo.

Wanavijiji wa Kata ya Bukumi (Vijiji vya Buira, Bukumi, Buraga na Busekera) wanaendelea kuchangia ujenzi huu.

Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo nae anaendelea kuchangia ujenzi huu. Juzi ameongeza mchango wake kwa kuwapatia Saruji Mifuko 50 (hamsini).

Matofali ya ujenzi huu yanaendelea kufyatuliwa kwenye eneo la ujenzi na kila mfuko mmoja wa saruji unatoa matofali 25 - ubora unaokubalika!

Wanavijiji wanaomba mchango wako, na tafadhali upeleke kwenye Akaunti ya Benki ya Sekondari hiyo ambayo ni:

Jina la Akaunti:
Mtiro Secondary School

Benki (Musoma):
NMB

Akaunti Namba:
30301200299

Tunatanguliza shukrani zetu za dhati!

Picha  hapo juu inaonesha maendeleo ya ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi kwenye Sekondari ya Mtiro ya Kata ya Bukumi, Musoma Vijijini

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 22.11.2023