MUSOMA VIJIJINI IMEAMUA KUWA NA “HIGH SCHOOLS” ZA MASOMO YA SAYANSI – KIRIBA SEKONDARI YAKAMILISHA UJENZI WA MAABARA TATU

MAABARA 3 za Physics, Chemistry na Biology za KIRIBA SEKONDARI iliyoko Kijijini Bwai Kwitururu, Kata ya Kiriba zimekamilika.

 

SEKONDARI zetu zote (21) za Kata, na za Binafsi (2) zitakamilisha ujenzi wa MAABARA 3 (Physics, Chemistry and Biology) mwakani (2022).

SEKONDARI mpya (10) zinazojengwa Jimboni mwetu lazima nazo zitajenga MAABARA hizo tatu.
UAMUZI WA KUWA NA “HIGH SCHOOLS” JIMBONI MWETU
WANANCHI wa Musoma Vijijini wameamua kuwa na “High Schools” za Masomo ya Sayansi ili kupandisha kiwango cha ELIMU kitolewacho Jimboni mwetu.
Vilevile, maombi ya kujenga CHUO cha UFUNDI (VETA) tayari yameishawasilishwa kwenye Wizara ya Elimu.
VIJANA wanaomaliza Darasa la Saba, na Kidato cha Nne wanazidi KUONGEZEKA Jimboni mwetu. Kwa hiyo, FURSA za KUJIENDELEZA kwa VIJANA hao zinapaswa kuwepo ndani na nje ya Jimbo letu.
KIRIBA SEKONDARI IMEKAMILISHA UJENZI WA MAABARA TATU ZA SAYANSI
KIRIBA SEKONDARI ya Kata ya Kiriba yenye Vijiji 3 (Bwai Kumsoma, Bwai Kwitururu na Kiriba) tayari imekamilisha ujenzi wa MAABARA 3 za Physics, Chemistry na Biology.
SEKONDARI hii ilifunguliwa Mwaka 2006 na ina jumla ya Wanafunzi 731 (Form I – IV). Kata ya Kiriba imeanza ujenzi wa Sekondari yake ya pili.
MATAYARISHO ya kuwa na “High School” ya michepuo (combinations) za PCM na PCB yanaendelea kwa kuanza ujenzi wa:
*Bweni la Wanafunzi 70
*Bwalo la Chakula
*Jiko
*Maktaba yenye Kompyuta
MICHANGO YA UJENZI WA MAABARA HIZO
*MTENDAJI KATA, Ndugu Pendo Isaac Mwita, MRATIBU ELIMU KATA, Ndugu Beatrice Ndosi, MKUU WA SEKONDARI, Mwl Mtani Paul na VIONGOZI wengine wa Kata na Vijiji vyote 3 wamefanikiwa kuhamasisha na kushawishi WANAVIJIJI kuchangia ujenzi huu.
*WANAVIJIJI
Wamechangia NGUVUKAZI zao kwa kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji ya kujengea.
*MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo, mbali ya MICHANGO yake yeye mwenyewe, amefanikiwa kushawishi baadhi ya WAZALIWA wa Kata ya Kiriba kuchangia ujenzi huu.
*BENKI ya CRDB imechangia Tsh MILIONI 20 – Ahsante sana CRDB!
MICHANGO inaombwa ya kuchangia ujenzi ulioelezwa hapo juu kwa lengo la kuwa na “HIGH SCHOOL” ya michepuo ya   PCM na PCB mwakani (Julai 2022). MICHANGO ipelekwe kwa Mkuu wa Shule au Mtendaji Kata.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini