ELIMU MUSOMA VIJIJINI: LENGO JIPYA NI KUWA NA “HIGH SCHOOLS” ZA MASOMO YA SAYANSI KUANZIA MWAKANI (2022)

MAABARA ya Chumba kimoja (Kemia) inayokamilishwa hapo MAKOJO SEKONDARI ya Kata ya Makojo.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
JIMBO la Musoma Vijijini lina VIPAUMBELE 5 ambavyo vinatokana na ILANI za UCHAGUZI za CCM (2020-2025, 2015-2020 & 2010-2015)
VIPAUMBELE hivyo vitano (5) ni:
*Elimu
*Afya
*Kilimo, Uvuvi na Ufugaji
*Mazingira
*Michezo na Utamaduni
KIPAUMBELE CHA ELIMU
JIMBO linaendelea kujenga na kuboresha MIUNDOMBIMU ya ELIMU kwenye Shule za Msingi na Sekondari.
Tunazo Kata 21 zenye jumla ya Vijiji 68 na Vitongoji 374.
IDADI YA SHULE ZA SEKONDARI
“SECONDARY SCHOOLS¬† (Form I – IV)”
*Sekondari za Kata/Serikali: 21
*Sekondari za Binafsi: 2
*Sekondari Mpya zinazojengwa: 10
“HIGH SCHOOLS (Form V – VI)”
*Tunayo moja tu, Kasoma High School, yenye michepuo (combinations) za HGK, HGL na HKL.
UJENZI NA UBORESHAJI WA MAABARA KWENYE SEKONDARI ZETU
SEKONDARI 21 za Kata za Jimboni mwetu zinaendelea na ujenzi na uboreshaji wa MAABARA zinazohitajika kwenye Masomo ya Sayansi. MAABARA hizo ni za masomo ya Fizikia, Kemia na Biolojia.
Vilevile, MAABARA za Masomo ya Sayansi zinajengwa kwenye Sekondari zetu mpya.
KUANZISHWA “HIGH SCHOOLS” ZA MASOMO YA SAYANSI
LENGO letu jipya ni mwakani (2022) kuwa na “High Schools” za Masomo ya Sayansi yenye michepuo (combinations) iliyowekwa na Serikali.
Kwa hiyo, WANAVIJIJI kwa kushirikiana na SERIKALI, na WADAU wengine MAENDELEO, wanaendelea KUJITOLEA kujenga MAABARA za SAYANSI za KISASA kwenye Sekondari zao za Kata.
MFANO WA MAABARA ZINAZOJENGWA MUSOMA VIJIJINI
*MAKOJO SEKONDARI
SEKONDARI hii ni ya Kata ya Makojo. Ilifunguliwa Mwaka 2006 na ina Wanafunzi 423. Kata ya Makojo ina Vijiji 3, ambavyo ni Chimati, Chitare na Makojo
*WANAKIJIJI wamechangia Matofali 1,300; na wamesomba mawe, kokoto, mchanga na maji ya ujenzi (NGUVUKAZI)
DIWANI VITI MAALUM, Mhe Tabu Machumu anafanya kazi nzuri ya kuchangia na kuhamasisha ujenzi huu akishirikiana na Mtendaji Kata, Ndugu Peresi Mgaya.
MKUU wa Makojo Sekondari, Mwl Emmanuel Daghau, amesimamia vizuri matumizi ya Tsh MILIONI 30 zilizotolewa na SERIKALI kwa ajili ya ukamilishaji wa CHUMBA 1 cha MAABARA ya Kemia.
MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ameahidi kuchangia MABATI 53 yatakapohitajika kuezeka Chumba cha Maabara ya pili.
*VITABU vya Masomo ya SAYANSI: Mbunge wa Jimbo ataendelea kuleta VITABU vingi vya masomo ya SAYANSI kutoka USA na UK, na kuvigawa bure mashuleni mwetu.
KARIBUNI tuchangie ujenzi na uboreshaji wa MAABARA za Sekondari zetu ikiwa ni MAANDALIZI ya kuwa na “HIGH SCHOOLS” za masomo ya SAYANSI Jimboni mwetu.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini