KILIMO CHA MIHOGO CHAENDELEA KUBORESHWA MUSOMA VIJIJINI

WANACHAMA wa  Kikundi cha KILIMO cha TUMEJITAMBUA wakiwa kwenye kazi za UOTESHAJI wa MITI na kwenye mashamba yao ya MIHOGO. Hapo ni Kijijini Bwenda, Kata ya Rusoli 

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
MAZAO MAKUU ya CHAKULA yalimwayo Jimboni mwetu ni: Mihogo, Mahindi, Viazi Vitamu, Mtama,  Mpunga, Maharage na Kunde.
MBOGAMBOGA (k.m., mchicha, kabechi, nyanya, vitunguu) na MATUNDA (matikiti, maembe na machungwa) navyo vinalimwa Vijijini mwetu.
KIKUNDI cha KILIMO kiitwacho TUMEJITAMBUA cha Kijijini Bwenda, Kata ya Rusoli kinajishughulisha na UBORESHAJI wa KILIMO cha MIHOGO.
KIKUNDI hiki kilianzishwa Mwaka 2018 na kina WANACHAMA 31.
Mbali ya kilimo cha MIHOGO, KIKUNDI hiki nacho kiko kwenye Kilimo cha Mahindi, Maharage, Viazi Lishe, Uoteshaji wa Miti, na WANACHAMA wake wanakopeshana fedha.
UBORESHAJI WA KILIMO CHA MIHOGO
KIKUNDI cha TUMEJITAMBUA kimeanzisha SHAMBA DARASA la   kilimo cha MIHOGO ambalo limekuwa kivutio kikubwa kwa wakulima wa eneo hilo na Vijiji vingine.
LENGO KUU la KIKUNDI hiki cha KILIMO ni:
*Kufanya biashara ya mazao ya chakula, ikiwemo biashara ya  VIJITI vya MIHOGO
*Kuanzisha KIWANDA kitakachozalisha bidhaa zitokanzo na ZAO LA la MIHOGO kama vile, unga, wanga na biskuti.
KATIBU wa KIKUNDI hicho, Ndugu Festo Obed ameeleza jinsi KIKUNDI hicho kilivyopata mafunzo ya uzalishaji wa MBEGU za MIHOGO kutoka Shirika la MEDA (Mennonite Economic Development Associate)
KIKUNDI hicho kimelima aina mbili za Mbegu za Mihogo, yaani wamepanda Vijiti 4,000 vya Mbegu ya TARICAS 4 (Tz 130) na wanategemea kuvuna Vijiti 48,000 ya aina hii ya Mbegu.
Vilevile, kwa Mbegu ya pili ya MKURANGA 1, wamepanda Vijiti 7,000 na wanategemea kuvuna Vijiti 42,000.
MBEGU zote hizi zinachukua muda wa MIEZI 9 kupata mavuno mazuri ya  MIHOGO.
Baada ya Mbegu mbili hizo kutoa MAFANIKIO mazuri,
Mtaalam wa MEDA, Ndugu Isaack Musa ameshawishi KIKUNDI hicho kuchukua MBEGU nyingine ambazo nazo zinastahimili magonjwa ya mimea na mabadiliko ya tabianchi.
MBEGU nyingine za MIHOGO zilizotolewa na MEDA ni aina ya Mkuranga, Mkumba, Kizimbani, Taricas 2 (F10) na Kiroba.
MIKOPO NA MISAADA ILIYOTOLEWA KWA KIKUNDI CHA KILIMO CHA TUMEJITAMBUA
MAFANIKIO ya Kikundi cha KILIMO cha TUMEJITAMBUA
yanatolewa shukrani nyingi kwa wafuatao:
*MEDA kwa kuwapatia MBEGU mbalimbali za MIHOGO.
*JAMII IMPACT kwa kuwapatia Mkopo wa SHILINGI MILIONI 5 (awamu ya kwanza) na SHILINGI MILIONI 10 (awamu ya pili), na  hivi karibuni watapokea mkopo mwingine.
*PCI Tanzania kwa kuwapatia Mbegu za Mahindi, Maharage, Alizeti na magunia ya kuhifadhia chakula
*SHIMAKIUMU kwa kuwapatia Mbegu za Mahindi, Dawa za Mimea na Viroba vya kupandia miche
*MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo kwa kuwapatia Mbegu za Mihogo, Mtama na Alizeti
MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo alishagawa bure Mbegu (Vijiti) aina ya Mkombozi kwa Wakulima wa Jimboni mwetu kama ifuatavyo:
*MSIMU wa Kilimo wa Mwaka 2016/2017:
Magunia 446
*MSIMU wa Kilimo wa Mwaka 2017/2018:
Magunia 350
KARIBUNI KIJIJINI BWENDA (Kata ya Rusoli) MNUNUE VIJITI VYA MBEGU ZA MIHOGO
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini