WANAKIJIJI  WASHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA VYUMBA VIPYA VYA MADARASA

WANAKIJIJI wakiwa kwenye ujenzi wa Vyumba vipya 2 vya Madarasa na Ofisi 1 ya Walimu wa S/M Nyamwiru ya Kijijini Maneke, Kata ya Busambara.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
SHULE ya MSINGI NYAMWIRU yenye WANAFUNZI 886 inaupungufu mkubwa wa MIUNDOMBINU ya ELIMU.
SHULE hii iko Kijijini Maneke, Kata ya Busambara. Kijiji hiki kina Shule za Msingi mbili (S/M Maneke & S/M Nyamwiru).
MWALIMU MKUU, Mwl Masilingi Maira ameleza yafuatayo kuhusu S/M Nyamwiru iliyoanzishwa Mwaka 1997:
*Mahitaji ya Vyumba vya Madarasa ni 17, vilivyopo ni vyumba 10.
*Darasa la Awali ndilo lenye Wanafunzi wengi ndani ya chumba kimoja cha Darasa –  wako 185
*Mahitaji ya Vyoo vya Wanafunzi ni Matundu 24, yaliyopo ni 12
*Matundu 4 yanahitajika kwa Vyoo vya Walimu, hakuna tundu hata moja.
*Mahitaji ya Walimu ni 17, waliopo ni 8
*Mahitaji ya Nyumba za Walimu ni 17, ipo nyumba moja tu.
SERIKALI YATOA SHILINGI MILIONI 40
SERIKALI kupitia Mradi wake wa EP4R imetoa Tsh Milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa:
*Vyumba vipya Viwili (2) vya Madarasa
*Ofisi moja (1) ya Walimu
MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha Maneke, Ndugu Rupago Loya, kwa niaba ya WANAKIJIJI wa MANEKE, ameishukuru sana SERIKALI kwa kutoa MCHANGO huo na amesema kwamba WANAKIJIJI watachangia NGUVUKAZI zao (kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji ya ujenzi) kukamilisha ujenzi huo.
MICHANGO MINGINE ILIYOTOLEWA KWENYE S/M NYAMWIRU
*KIKUNDI cha BUSARA
Kinachangia chakula cha Wanafunzi
*MBUNGE wa JIMBO
Prof Sospeter Muhongo amechangia:
(i) Madawati 115
(ii) Vitabu zaidi ya 1,000 vya Maktaba
MATOKEO YA MITIHANI YA TAIFA YA S/M NYAMWIRU
DARASA la IV (2020)
*Watahiniwa: 127
*Waliofaulu: 127
DARASA la VII (2020)
*Watahiniwa: 101
*Waliofaulu: 67
OMBI KUTOKA KIJIJINI MANEKE
*WAZALIWA wa Kijiji cha Maneke wanaombwa sana WAJITOKEZE kuchangia MAENDELEO ya nyumbani kwao, ikiwemo ujenzi wa Miundombinu ya ELIMU ya S/M Nyamwiru.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini