UBORESHAJI WA MAZINGIRA YA KUJIFUNZA NA KUFUNDISHIA – MAKTABA ZAENDELEA KUJENGWA KWENYE SHULE ZA MSINGI

 

Katika MATUKIO mbalimbali kwenye S/M KARUBUGU ya Kijijini Kurwaki, Kata ya Mugango, Prof Sospeter Muhongo alitembelea Darasa la III la Shule hiyo kushuhudia Mirundikano ya Wanafunzi madarasani.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge

WANANCHI wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kushirikiana na SERIKALI kuboresha mazingira ya KUJIFUNZA na KUFUNDISHIA kwenye SHULE za MSINGI na SEKONDARI za Jimboni mwetu.

UJENZI WA MAKTABA KWENYE S/M KARUBUGU

KIJIJI cha KURWAKI kimeamua kujenga MAKTABA kwenye Shule yao ya Msingi, S/M KARUBUGU, iliyofunguliwa Mwaka 1963.

MWALIMU MKUU wa Shule hii, Mwl Rehema Ramadhan amesema kwamba Shule ina jumla ya WANAFUNZI 830 na WALIMU 5.

UFAULU WA MITIHANI YA MWAKA JANA (2020)

MWALIMU MKUU huyo ameeleza UFAULU huo kama ifuatavyo:

STD IV (2020)
*Watahiniwa: 82
*Waliofaulu: 82

STD VII (2020)
*Watahiniwa: 73
*Waliofaulu: 60

UJENZI WA MAKTABA YA KISASA

MTENDAJI wa Kijiji cha Kurwaki, Ndugu Abeid Makamba Ndagala amesema kwamba ujenzi wa MAKTABA ya S/M KARUBUGU ulianza Jumatatu, 8.3.2021 na wanakusudia kukamilisha ujenzi wa BOMA la MAKTABA kabla ya tarehe 30.3.2021.

WACHANGIAJI WA UJENZI HUU

*WANAKIJIJI:
Wanachangia NGUVUKAZI kwa kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji.

*WANAKIJIJI wanachangia FEDHA taslimu Tsh. 5,000/= kwa kila KAYA.

*MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo anachangia SARUJI ya UJENZI wa BOMA la MAKTABA hii. Leo,16.3.2021 amechangia SARUJI MIFUKO 50 ataendelea kuchangia hadi Boma likamilike.

*PCI (TANZANIA) itafadhili umaliziaji wa ujenzi wa MAKTABA hiyo baada ya kukabidhiwa BOMA linalojengwa na WANAKIJIJI. Aidha, PCI (TANZANIA) itaweka SAMANI zinazohitajika kwenye MAKTABA hiyo.

VITABU VYA MAKTABA YA S/M KARUBUGU

Wachangiaji wa VITABU vya MAKTABA hiyo ni:

*PCI (Tanzania)
*MBUNGE wa Jimbo

MATUKIO mbalimbali kwenye S/M KARUBUGU ya Kijijini Kurwaki, Kata ya Mugango.

*Ufyatuaji wa matofali ya ujenzi wa Maktaba.
*Uchimbaji wa Msingi wa Boma la Maktaba
*Ujenzi wa Msingi wa Boma la Maktaba
*Mirundikano ya Wanafunzi madarasani. Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo alitembelea Darasa la III la Shule hiyo kushuhudia Mirundikano ya Wanafunzi madarasani.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz