MAJI SAFI NA SALAMA YA BOMBA NA SHEREHE ZA PASAKA NDANI YA VIJIJI VITATU

WANANCHI wa Vijiji vya Busungu (Kata ya Bulinga) na Kwikerege (Kata ya Rusoli) wakiteka MAJI ya BOMBA kutoka Ziwa Victoria.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge

WANANCHI wa Vijiji vya Busungu (Kata ya Bulinga), Bukima (Kata ya Bukima) na Kwikerege (Kata ya Rusoli) WAMEFURAHI sana kuanza kupata MAJI ya BOMBA ya Ziwa Victoria.

WANANCHI hao, hasa akina MAMA na WATOTO wamefurahishwa sana na upatikanaji wa maji katika maeneo yao, kwani hapo awali walilazimika kutembea umbali mrefu na kutumia muda mwingi kutafuta maji kutoka kwenye visima vya asili.

Mama Nyamburi Mafuru, Mkazi wa Kijiji cha Busungu amesema kuwa amefurahishwa sana na neema ya upatikanaji wa maji kijijini mwao maana walitumia muda mwingi kutafuta maji na kupelekea shughuli za kujitafutia kipato kuzorota.

Mama huyo amesema, “Tunaishukuru sana Serikali yetu kwa kutuondolea kero hii hasa sisi wanawake.”

MKANDARASI wa Mradi huu, EDM NETWORK LTD, Ndugu Adiel Mushi amethibitisha kukamilika kwa mradi huo kwa zaidi ya 90% na VITUO 23 vimeanza kutumika ambavyo ni:
* Vioski 2
*Maltwater 1
*Vituo 2 vya kunyweshea mifugo
*Vituo 18 vya kuchotea maji.

Mkandarasi huyo ameeleza kwamba TANKI la BUSUNGU lina uwezo wa kujaza LITA 225,000 za kuhudumia Vijiji 3 hivyo.

DIWANI wa Kata ya Bulinga, Mhe Abel Mafuru amewataka WANANCHI kutunza vizuri MIUNDOMBINU ya usambazaji wa maji ya bomba kwenye Vijiji vyao.

DIWANI huyo ametoa SHUKRANI nyingi sana kwa SERIKALI yetu kwa kuwapatia MAJI SAFI na SALAMA ya BOMBA, na vilevile amemshukuru Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo kwa UFUATILIAJI mzuri wa Miradi ya Maji na Miradi mingine ndani ya Jimbo lao.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijni.or.tz