SERIKALI YASHIRIKIANA NA WANAKIJIJI KUTATUA MATATIZO YA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA

Ujenzi unaondelea (Vyumba vya Madarasa & Vyoo) kwenye S/M BUSEKERA ya Kijijini Busekera, Kata ya Bukumi.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge

SHULE YA MSINGI BUSEKERA ilifunguliwa Mwaka 1954. Shule hii iko Kijijini Busekera, Kata ya Bukumi.

MWALIMU MKUU wa Shule hii, Mwl Kevin Majogoro amesema kwamba Shule ina jumla ya WANAFUNZI 1,271.

MAHITAJI ya Madarasa ni Vyumba 24, vilivyopo ni 10!

MIRUNDIKANO ya WANAFUNZI madarasana ni mikubwa. Kwa mfano, Darasa la AWALI lina Wanafunzi 234 kwenye chumba kimoja na Darasa la VII lina Wanafunzi 111 ndani ya chumba kimoja!

SERIKALI YATOA MCHANGO WA KUJENGA MADARASA NA VYOO

SERIKALI kupitia MRADI wake wa EP4R imetoa Tsh MILIONI 47.7 kwa ajili ya ujenzi wa VYUMBA 2 vya MADARASA na CHOO chenye MATUNDU 7 ya S/M Busekera.

MICHANGO YA WANAKIJIJI

MTENDAJI wa Kijiji cha Busekera, Ndugu Faustine Majura amesema WANAKIJIJI wameshirikishwa kwa:

*kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji

*kuchimba shimo la choo

*kuchimba msingi wa Vyumba 2 vya madarasa.

SHUKRANI KWA SERIKALI YETU

Wananchi na Viongozi wa Kijiji cha Busekera WANAISHUKURU sana SERIKALI kwa kuwachangia Tsh Milioni 47.7.

MICHANGO YA MBUNGE WA JIMBO

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo amekuwa akihamasisha na kuchangia uboreshaji wa MAZINGIRA ya KUJIFUNZA na KUFUNDISHIA kwenye SHULE zote za Jimboni mwao.

MICHANGO ya Mbunge huyo kwenye S/M Busekera ni:

*Saruji Mifuko 60
*Mabati 54
*Madawati 94
*Vitabu vingi vya Maktaba

TUCHANGIE KUBORESHA UFAULU WA S/M BUSEKERA

MATOKEO ya DARASA la IV (2020):

*Watahiniwa 123
*Waliofaulu 120

MATOKEO ya DARASA la VII (2020):

*Watahiniwa 69
*Waliofaulu 45

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijni. or. tz