WASAIDIZI 6 WA MBUNGE WA JIMBO WANUNULIWA PIKIPIKI MPYA 6

Tukio la ununuaji na upokeaji wa PIKIPIKI MPYA 6 za Wasaidizi wa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

Leo, Jumatano, tarehe 3 Machi 2021, MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo AMEWANUNULIA WASAIDIZI wake PIKIPIKI MPYA 6 na kuwazawadia PIKIPIKI za ZAMANI walizokuwa wanazitumia.

JIMBO la Musoma Vijijini lina KATA 21 zenye VIJIJI 68 na VITONGOJI 374.

WASAIDIZI wa MBUNGE wamegawiwa maeneo yao ya kazi na KILA JUMAMOSI Ripoti za kazi zao za wiki lazima Mbunge huyo apewe.

Kwa hiyo, WANAVIJIJI wanafuatwa huko huko VIJIJINI mwao na hawana sababu ya KUFUNGA SAFARI kwenda kumtafuta Mbunge, badala yake wao (wanavijiji) ndio wanatembelewa kwenye makazi yao au sehemu zao za kazi za kiuchumi na kwenye miradi ya maendeleo.

Mbunge huyo ametoa VITENDEA KAZI vifuatavyo:

*Pikipiki tokea Mwaka 2015
*Mafuta ya Pikipiki kila wiki
*Smartphone & Bando
*Laptop
*GPS

Vilevile, Wasaidizi wa Mbunge huyo wanapewa BONUS ya kila mwisho wa Mwaka.

KARIBUNI TUJENGE MUSOMA VIJIJINI

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz