MBUNGE WA JIMBO AWATOA WANAFUNZI WANAOJIFUNZIA MCHANGANI NA AKODISHIA NYUMBA KIJIJINI ITUMIWE NA WALIMU WA SEKONDARI MPYA

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, alipokuwa Kigera Sekondari (Kata ya Nyakatende) na Shule Shikizi Egenge (Kata ya Etaro)

 

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo anakagua ujenzi unaoendelea kwenye SHULE za MSINGI na SEKONDARI za Jimbo hilo.

SHULE SHIKIZI EGENGE

Shule hii iko kwenye Kitongoji cha Egenge, Kijiji cha Busamba, Kata ya Etaro.

IDADI ya WANAFUNZI wa Shule hii ni kama ifuatavyo: 60 Awali, 30 Darasa la I na 60 Darasa la II.

Prof Sospeter MUHONGO ameamua KUNUNUA VIBAO vya KUJIFUNZIA vya Wanafunzi wa DARASA LA AWALI na wa DARASA LA KWANZA baada ya kuambiwa kwamba Wanafunzi hao wanajifunza kwa KUANDIKA MCHANGANI.

Vilevile, Mbunge huyo amekubali KUEZEKA PAA la Vyumba 2 vya Madarasa vinavyojengwa hapo.

Shule ina Vyumba 4 vya Madarasa vilivyojengwa na SERIKALI (Miradi ya EQUIP & EP4R) kwa kushirikiana na WANANCHI wa Kitongoji cha Egenge.

Vilevile, WANANCHI hao hao wanajenga Vyumba vingine 4 kwa kushirikiana na DIWANI na MBUNGE wao wa Jimbo.

LEO KUU ni Shule SHIKIZI EGENGE iwe na MIUNDOMBINU ya Shule kamili ya Msingi kabla ya tarehe 30 Disemba 2021.

SEKONDARI MPYA YAFUNGULIWA KIJIJINI KIGERA

KIGERA Sekondari imefunguliwa Jumatatu, tarehe 22.2.2021 na tayari WANAFUNZI 103 kati ya 122 wa Kidato cha Kwanza wameanza masomo.

WALIMU 5 ni wa kuajiriwa na Serikali na 1 ni wa kujitolea.

UJENZI unaendelea kwa kasi na MAABARA zitakamilika kabla ya tarehe 1.6.2021.

SEKONDARI hii MPYA ni kati ya Sekondari mpya 5 zinazojengwa Jimboni mwetu, na nyingine 4 zitaanza kujengwa mwaka huu.

MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ametembelea Sekondari hiyo mpya na kutatua tatizo la MAKAZI ya WALIMU hapo Kijijini.

MBUNGE huyo ameamua kulipia PANGO la MIEZI 6 ili WALIMU 2 waweze kupata MAKAZI hapo Kijijini, karibu na Sekondari hiyo.

ELIMU NDIYO INJINI KUU YA MAENDELEO NA USTAWI WA JAMII

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz