WANAFUNZI WASIOJUA KUSOMA, KUANDIKA NA KUHESABU (KKK) WAPUNGUA KWA KASI KUBWA NA UTORO WATOWEKA BAADA YA KITONGOJI CHA MWIKOKO KUJENGA SHULE YAKE

Ujenzi unavyoendelea kwenye Shule Shikizi MWIKOKO ya Kitongoji cha Mwikoko, Kijijini Chitare, Kata ya Makojo.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge

WANAVIJIJI wa JIMBO la Musoma Vijijini wanaendelea KUSHIRIKIANA na SERIKALI kuboresha MAZINGIRA ya kujifunzia na kufundishia WANAFUNZI wa SHULE za Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) yenye Jimbo la Musoma Vijijini.

UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA
ELIMU YA MSINGI

*VYUMBA vipya 395 vya Madarasa vimejengwa kwenye Shule za Msingi za Serikali (111) ndani ya Miaka 5 (2015-2020)

MICHANGO ya ujenzi huo imetolewa na Wanavijiji, Serikali, Madiwani, Mbunge wa Jimbo na baadhi ya Wazaliwa wa Vijiji husika.

*SHULE SHIKIZI 12 zinajengwa na kupanuliwa kuwa Shule za Msingi kamili

MICHANGO ya ujenzi huo inatolewa na Wanavijiji, Serikali, Madiwani, Mbunge wa Jimbo na baadhi ya Wazaliwa wa Vijiji husika.

*MAKTABA za Shule za Msingi zinaendelea kujengwa na kufunguliwa

MICHANGO ya ujenzi wa MAKTABA inatolewa na Wanavijiji, PCI TANZANIA, Madiwani, Mbunge wa Jimbo na baadhi ya Wazaliwa wa Vijiji husika.

*VYOO vya kutosha vimejengwa kwa wingi kwenye Shule za Msingi – ahsante sana PCI TANZANIA kwa mchango wenu mkubwa kwenye ujenzi wa vyoo mashuleni. Wanavijiji wamechangia nguvukazi.

SHULE SHIKIZI MWIKOKO

Shule Shikizi Mwikoko ipo kwenye Kitongoji cha Mwikoko, Kijijini Chitare, Kata ya Makojo

WANAFUNZI 299 wa chini ya miaka minane (8), yaani Darasa la CHEKECHEA hadi la PILI wameacha kutembea umbali wa zaidi ya KILOMITA 4 kwenda masomoni kwenye Shule za Msingi za CHITARE A & B.

MWALIMU Magige Simon, Msimamizi na Mlezi wa Shule Shikizi Mwikoko amesema uwepo wa Shule hiyo kwenye Kitongoji hicho, umezaa matunda mazuri:

(i) UTORO unatoweka na Wanafunzi wanazidi kupenda shule

(ii) IDADI ya WANAFUNZI wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) INAPUNGUA kwa kasi kubwa mno kwa Wanafunzi wa Darasa la I & II wa Kitongoji hicho

MWENYEKITI wa Kitongoji cha Mwikoko, Ndugu Athuman Mtembela anawashukuru wale wote wanaochangia ujenzi wa shule yao.

MICHANGO YA UJENZI WA SHULE SHIKIZI MWIKOKO

(i) WANAKIJIJI – nguvukazi (kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji) na fedha taslimu Tsh 10,300 kutoka kwa kila KAYA.

(ii) SERIKALI kupitia Mradi wake wa EQUIP umechangia Tsh Milioni 60.

(iii) DIWANI wa Kata, Mhe Kuyenga Masatu amechangia Tsh 500,000

(iv) MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo amechangia SARUJI MIFUKO 100.

(v) MFUKO wa JIMBO umechangia SARUJI MIFUKO 80 na MABATI 108.

MALENGO ya Wakazi wa Mwikoko ni kwamba ifikapo Mwakani (2022) Shule Shikizi yao iwe Shule kamili ya Msingi yenye MADARASA 7.

KUMBUKA:
Kwa miaka 2 mfululizo (2019 & 2020) WANAFUNZI wa Darasa la IV wa Musoma Vijijini WAMEONGOZA Mkoa wa Mara kwenye MITIHANI ya Darasa la IV.

*Tuendelee kuboresha MAZINGIRA ya kujifunzia na kufundishia WANAFUNZI wetu – TUTAFANIKIWA!

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz