KITONGOJI CHA NYASAENGE CHAAMUA KUJENGA SHULE YAKE YA MSINGI

MIUNDOMBINU ya  SHULE SHIKIZI NYASAENGE inayojengwa ndani ya Kitongoji cha Nyasaenge, Kijiji cha Kataryo, Kata ya Tegeruka.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
WATOTO wa Kitongoji cha NYASAENGE wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya KILOMITA 10 kwenda masomoni kwenye SHULE ya Msingi KATARYO.
Kitongoji cha NYASAENGE ni moja kati ya VITONGOJI 6 (sita) vya Kijiji cha KATARYO. Kijiji hiki ni moja ya Vijiji 3 (Kataryo, Mayani na Tegeruka)  vya Kata ya TEGERUKA
Kijiji cha KATARYO kina SHULE 2 za MSINGI, yaani KATARYO na KATARYO B.
WANANCHI wa Kitongoji cha NYASAENGE wameamua kutatuta tatizo la umbali mrefu unaotembewa na WATOTO wao kwenda masomoni kwa KUJENGA SHULE yao ya MSINGI, ambayo itaanza ikiwa SHULE SHIKIZI NYASAENGE.
MIUNDOMBINU ya SHULE SHIKIZI hiyo inayokamilishwa ni:
*Vyumba 2 vya Madarasa
*Ofisi 1 ya Walimu
*Choo chenye Matundu 8
Kwa hiyo, WANANCHI wa KITONGOJI cha MYASAENGE wanaomba WATATO wao waanze MASOMO yao ya AWALI kwenye Shule Shikizi yao itakayotambuliwa na Halmashauri yetu.
MRATIBU wa Elimu Kata ya Tegeruka, Ndugu Modest Fadhili amesema kuwa jumla ya WANAFUNZI 149 wa Darasa la Awali wanasomea CHINI ya MTI hapo hapo Kitongojini Nyasaenge wakifundishwa na MWALIMU wa KUJITOLEA, Ndugu Mauna Rugeye.
KITONGOJI CHA NYASAENGE CHAFANYA VIZURI MASOMONI
Mbali ya umbali mrefu wa kutembea, WANAFUNZI wa kutoka Kitongoji cha NYASAENGE, wamefaulu vizuri Mitihani ya Darasa la VII (2020) wakishinda Vitongoji vingine vitano (5).
Matokeo ya Darasa la VII (2020) ni haya hapa:
*S/M Kataryo:*
Kati ya Wanafunzi 16 waliofaulu, jumla ya Wanafunzi 11 (Wasichana 6 na Wavulana 5) wametoka Kitongoji cha Nyasaenge
*S/M Kataryo B*
Kati ya Wanafunzi 37 waliofaulu, jumla ya Wanafunzi 13 (Wasichana 8 na Wavulana 5) wametoka Kitongoji cha Nyasaenge
WACHANGIAJI WA UJENZI HUU
(i) WANANCHI
*NGUVUKAZI  – kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji
*FEDHA taslimu – kila KAYA inachangia Tsh 30,000/=
(ii) WAZALIWA WA KITONGOJI CHA NYASAENGE
Fedha taslimu zimechangwa kutoka kwa:
*Saguda Paliga 100,000/=
*Madete Washuli 100,000/=
*Gubi Gong’oma 100,000/=
*Maiku Lyangeni 100,000/=
(ii) MBUNGE WA JIMBO
*Prof Sospeter Muhongo atachangia MABATI 54.
MBUNGE huyo ametoa MICHANGO mingi kwa SHULE 2 za Kijiji cha KATARYO ambayo ni:
S/M KATARYO
*Madawati 76
*Vitabu vya Maktaba
S/M KATARYO B
*Saruji Mifuko 60
*Mabati 108
*Madawati 73
*Vitabu vya Maktaba S/M
MFUKO WA JIMBO
*Mabati 54
(S/M Kataryo B)
MWENYEKITI wa Kitongoji cha Nyasaenge, Ndugu Kabole Mesogachura ametoa SHUKRANI nyingi kwa WACHANGIAJI wote wakiwemo WANANCHI wa Kitongoji cha NYASAENGE.
KIONGOZI huyo anaomba WADAU wa MAENDELEO waendelee kuwachangia VIFAA ZA UJENZI ili wakamilishe ujenzi wa SHULE SHIKIZI NYASAENGE ambayo itapanuliwa na kuwa SHULE YA MSINGI NYASAENGE.
WANAFUNZI 149 wa ELIMU ya AWALI wa Kitongoji cha NYASAENGE wataacha kusomea CHINI ya MTI baada ya kupata VYUMBA 2 vya Madarasa ya SHULE SHIKIZI NYASAENGE.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini