KATA YA NYAMRANDIRIRA YADHAMIRIA KUPATA SEKONDARI YAKE YA PILI ITAKAYOFUNGULIWA JANUARI 2021

MIUNDOMBINU ya SEKA SEKONDARI inavyoendelea kujengwa Kijijini Seka, Kata ya Nyamrandirira.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Kata ya Nyamrandirira inaundwa na Vijiji Vitano (5) ambavyo ni: Chumwi, Kaboni, Kasoma, Mikuyu na Seka.
Kata hii ina Sekondari moja tu iliyoko Kijijini Kasoma (KASOMA SECONDARY SCHOOL) yenye Kidato cha kwanza hadi cha sita.
UMBALI MREFU wa zaidi ya km 10 wa kutembea kwa  Wanafunzi walio wengi, na MIRUNDIKANO yao  Madarasani ni sababu zilizowafanya WANANCHI wa Kata hii kuamua kujenga SEKONDARI ya pili Kijijini Seka (SEKA SECONDARY SCHOOL).
Akizungumza na Msaidizi wa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini,  Ndugu Fedson Masawa, DIWANI wa Kata ya Nyamrandirira, Mhe Nyeoja Wanjara amesema kuwa lengo lao ni kukamilisha ujenzi wa VYUMBA 5 vya MADARASA kabla ya tarehe 30 Januari 2021.
MIUNDOMBINU mingine muhimu inayohitajika ili SEKA SEKONDARI ifunguliwe itakamilishwa kabla ya tarehe 30 Januari 2021 ambayo ni:
* Choo chenye Matundu 8
* Jengo la Utawala
MAJENGO mengine yatakayojengwa ni: Maabara, Maktaba, Vyumba zaidi vya Madarasa, Nyumba za Walimu, n.k.
SEKA SEKONDARI ni moja ya Sekondari Mpya 5 zinazojengwa ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini lenye Sekondari 20 za Serikali/Kata na 2 za Binafsi.
*Wachangiaji wa Ujenzi huu ni:*
(i) WANANCHI kwa mpangilio huu:
*Kijiji cha Kaboni –  kila Kaya inachangia Tsh 10,000/=
* Kijiji cha Seka – kila Kaya inachangia kati ya Tsh 20,000/=  na 15,000/=
* Kijiji cha Kasoma – kila Kaya inachangia Tsh 10,000/=
* Kijiji cha Chumwi – kila Kaya inachangia Tsh 6,500/=
* Kijiji cha Mikuyu – kila Kaya inachangiya Tsh 20,000/=
(ii) NGUVUKAZI za Wanavijiji wa Vijiji vyote 5 – kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji.
(iii) MBUNGE WA JIMBO
Prof Sospeter Muhongo tayari amekwishachangia SARUJI MIFUKO 250 (mia mbili hamsini).
MBUNGE huyo ametoa AHADI ya kutoa MICHANGO zaidi iwapo KASI ya UJENZI itaongezeka, na hasa ya ujenzi wa VYOO vya Shule.
(iv) WAZALIWA WA KATA YA SEKA
*Wazaliwa 21 tayari wamechangia jumla ya Tsh 1,884,000/=
(v) WADAU WENGINE WA MAENDELEO
Mgodi wa MMG uliopo Kijijini Seka umechangia:
* Mawe tripu 20
* Molamu tripu 10
* Mchanga tripu 10
Vilevile, MMG imetoa AHADI ya kujenga Jengo moja la Shule.
MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha Seka, Ndugu Damian Mjara, kwa niaba ya Wananchi wa Kata Nyamrandirira, anawaomba WADAU wa MAENDELEO wajitokeze na kuwachangia MABATI, SARUJI, NONDO, MADAWATI, n.k. ili SEKA SEKONDARI ifunguliwe tarehe 30 Januari 2021.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini