SEKONDARI NYINGINE MPYA INAYOJENGWA KWA NGUVU ZA WANANCHI NA MBUNGE WAO KUFUNGULIWA JANUARI 2021

ukamilishaji wa MIUNDOMBINU ya KIGERA SECONDARY SCHOOL itakayofunguliwa Januari 2021.

Tarehe 29.12.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
JIMBO la MUSOMA VIJIJINI lenye Kata 21na Vijiji 68 linajenga SEKONDARI MPYA 5 ili kutatua MATATIZO sugu mawili – mirundikano madarasani na umbali mrefu wanaotembea baadhi ya Wanafunzi.
Kwa hiyo, idadi ya SEKONDARI za Serikali Jimboni humo zitaongezeka kutoka 20 hadi 25. Vilevile, zipo Sekondari 2 za Madhehebu ya Dini.
MWAKA MPYA (2021): Kata nyingine 6 zitaanza ujenzi wa Sekondari ya pili ya Kata zao.
KATA ya NYAKATENDE yenye Vijiji 4 (Kakisheri, Kamguruki, Kigera na Nyakatende) ina Sekondari moja tu (NYAKATENDE SEKONDARI) ambayo imeelemewa na wingi wa Wanafunzi kutoka Vijiji 4 na wengine wanatoka Kata jirani ya Ifulifu.
Kwa hiyo, UJENZI wa SEKONDARI ya PILI ya Kata hiyo ni muhimu sana.
KIGERA SEKONDARI ITAFUNGULIWA JANUARI 2021
Vijiji 2 (Kakisheri na Kigera) vya Kata hiyo VIMEAMUA kujenga SEKONDARI yao ili watoto wao waachane kabisa na mirundikano madarasani na kutembea mwendo wa zaidi ya kilomita 10 kwenda masomoni.
WANAOCHANGIA UJENZI WA KIGERA SEKONDARI
(i) WANAVIJIJI wa Vijiji viwili wanachangia NGUVUKAZI zao – kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji.
 (ii) WANAVIJIJI hao hao wanachangia FEDHA taslimu: Shilingi 2,000 (elfu mbili) kwa kila mkazi mwenye umri wa kuanzia miaka 18.
(iii) WAZALIWA wa Vijiji hivyo viwili: wanalipa GHARAMA zote za MAFUNDI na wananunua baadhi ya VIFAA vya ujenzi.
(iv) DIWANI wa Kata ya Nyakatende, Mhe Marere J. Kisha ambae ni mmoja wa WAZALIWA na Vijiji 2 nae anachangia kama Wazaliwa wenzake.
*Vilevile, DIWANI huyu anatengeneza MADAWATI 130 ya WANAFUNZI watakaoanza Kidato cha kwanza shuleni hapo Januari 2021.
(v) MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo amekwishachangia:
*Saruji Mifuko 150
 *Mabati 108
MFUKO wa JIMBO
*Saruji Mifuko 100
*Mbunge huyo atachangia, Januari 2021, zaidi ya VITABU 1,000 (elfu moja) vya SAYANSI vya Maktaba ya Sekondari hiyo mpya.
MAJENGO YANAYOKAMILISHWA UJENZI
*VYUMBA 2 vya Madarasa vimeishaezekwa, frame za milango na madirisha zimewekwa, sasa wanapiga jamvi kwa ajili ya kuweka sakafu.
*JENGO la Utawala lenye Ofisi 9 limeezekwa na madirisha yamewekwa.
*BOMA la CHOO cha Matundu 11 limeishaezekwa . Tundu 1 la Choo ni kwa ajili ya Wanafunzi wenye mahitaji maalum.
*Boma la Maabara linajengwa
*Boma la Nyumba ya Mwalimu linajengwa
WANAFUNZI 191 WA KATA WAMEFAULU
Wanafunzi 191 wa Kata ya Nyakatende wamefaulu kujiunga na Kidato cha Kwanza Januari 2021.
Kwa hiyo, WANAFUNZI hao 191 watagawanywa kwenye SEKONDARI 2 za Kata – Nyakatende & Kigera Secondary Schools.
MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha Kigera, Ndugu Magafu Katura anatoa maombi yafuatayo ya  kuchangia ujenzi huu  kwa hatua waliyoifikia:
*Saruji Mifuko 100
*Topu 31 za Milango
*Frame 21 za Milango ya Choo na ya Jengo la Utawala
*Vitasa 31vya Milango
*Bawaba 31 (pair) za Milango
*Masinki 15 ya Choo
*Mabomba piece 5 ya Choo
*Rangi Lita 80
HALMASHAURI ya Wilaya ya Musoma IMECHANGIA Shilingi MILIONI TANO (5M) kwenye ukamilishaji wa ujenzi wa Miundombinu ya Sekondari hii mpya.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini