WANANCHI WA KIJIJI CHA NYASAUNGU WASHIRIKIANA NA MBUNGE WAO KUJENGA SEKONDARI YA KIJIJI CHAO

ukamilishaji wa ujenzi wa MIUNDOMBINU ya NYASAUNGU SEKONDARI ya Kijiji cha Nyasaungu, Kata ya Ifulifu. 

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
KATA ya IFULIFU ni Kata pekee kati ya Kata 21 za Jimbo la Musoma Vijijini ambayo HAINA SEKONDARI yake.
WANAFUNZI wa Sekondari kutoka VIJIJI 3 vya Kata hii, yaani, Kabegi, Kiemba na Nyasaungu wanasoma kwenye Sekondari za Kata jirani za Mugango na Nyakatende.
WANAVIJIJI wa Kata ya IFULIFU WAMEAMUA kujenga Sekondari zao za Kata kwa utaratibu huu:
*Kijiji cha Nyasaungu kinajenga Sekondari yake kwa kushirikiana na Mbunge wao wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo
*Vijiji vya Kabegi na Kiemba nao wanajenga  Sekondari yao kwa kushirikiana na Mbunge wao, Prof Muhongo
NYASAUNGU SEKONDARI
Ujenzi wa Sekondari hii ulianza Julai 2019.  WANANCHI wa Kijiji cha Nyasaungu waliamua kujenga Sekondari yao iitwayo NYASAUNGU SEKONDARI ili kutatua kero ya Watoto wao kutembea kilomita 24 kwenda masomoni kwenye Sekondari za Kata jirani.
MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha Nyasaungu, Ndugu Magesa Chacha Marera, amesema kuwa ujenzi huo hadi hapo ulipofikia unaendeshwa kwa NGUVU za WANANCHI wa Kijiji cha Nyasaungu pekee, na michango ya Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo.
MAKUNDI YANAYOCHANGIA UJENZI WA NYASAUNGU SEKONDARI
(i) KAYA zenye NG’OMBE zaidi ya 100, michango yao ni zaidi ya Tshs 200,000 (laki mbili)
(ii) KAYA zenye NG’OMBE kati ya 50 na 99, michango yao ni Tshs 100,000 (laki moja)
(iii) KAYA zenye NG’OMBE chini ya 50, michango yao ni Tshs 40,000 (elfu arobaini).
(iv) NGUVUKAZI za Wanakijiji za kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji.
(v) MICHANGO ya Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo
*MABATI 108
*SARUJI MIFUKO 35
*NONDO 20
MFUKO wa JIMBO
*Mabati 54
MIUNDOMBINU INAYOKAMILISHWA SEKONDARI IFUNGULIWE JANUARI 2021
*VYUMBA 2 vya Madarasa tayari vimeishaezekwa
*CHUMBA 1 cha Darasa tayari kimeishaezekwa na hiki kitatumika kwa muda kama OFISI ya WALIMU
*CHOO chenye MATUNDU 6 kinaezekwa kabla ya tarehe 1.1.2021
WANAFUNZI 124 WA KATA WAMEFAULU
NYASAUNGU Sekondari, yenye VYUMBA 2 vya MADARASA inategemea kupokea baadhi ya WANAFUNZI hao wa Kata
UONGOZI wa KIJIJI cha Nyasaungu unatoa maombi kwa WADAU wa MAENDELEO waungane wao kwenye ujenzi wa SEKONDARI yao – wanaendelea na ujenzi wa Vyumba vya Madarasa, Jengo la Utawala, Maabara, Maktaba, Nyumba za Walimu, Vyoo, n.k.
SEKONDARI hii MPYA itakuwa tayari kupokea Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, Januari 2021.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini