VIKUNDI VYA WANAVIJIJI VYA KUKUZA UCHUMI VINAZIDI KUSHAMIRI MUSOMA VIJIJINI

baadhi ya Wanachama wa Kikundi cha TUMETAMBUA wakipalilia MIHOGO shambani mwao, Kijijini KASTAM, Kata ya Bukima.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge

WANAVIJIJI ndani ya VIJIJI 68 vya Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kuanzisha VIKUNDI vya kustawisha na kukuza UCHUMI wao. VIKUNDI hivyo ni vya KILIMO, UVUVI, UFUGAJI na VICOBA.

KIKUNDI cha TUMETAMBUA kilichopo Kijiji cha Kastam, Kata ya Bukima kilianzishwa Mwaka 2017 na kina Wanachama 29.

KIKUNDI hiki kinajishughulisha na KILIMO, uoteshaji wa MITI, na KUKOPESHANA fedha.

MWENYEKITI wa Kikundi hiki, Ndugu Nyamisi Daniel anasema wao wamejikita zaidi kwenye KILIMO cha mihogo, mahindi, maharage na viazi lishe. Kwa hiyo, WANACHAMA wote wanacho CHAKULA cha kutosha kwa familia zao, na wanapeleka 20% ya MAVUNO yao ya mazao ya chakula kwenye S/M Mkapa ya Kijijini mwao.

Vilevile, Kikundi hiki chenye MAFANIKIO makubwa kinatoa msaada wa VIFAA vya SHULE kwa Wanafunzi wanaosoma wakiwa kwenye mazingira magumu.

MBEGU YA MIHOGO YA AINA YA MKOMBOZI YATOA MAVUNO MAZURI

MZALISHAJI MBEGU za MIHOGO, Ndugu Festo Obed ambae pia ni Mwanachama wa Kikundi cha TUMETAMBUA amepata MAFUNZO ya kuzalisha mbegu bora za mihogo kutoka Shirika la MEDA ambalo kwa sasa linafanya kazi kwenye Kata za Bugoji, Bukima, Kiriba, Murangi, Nyamrandirira, Rusoli na Suguti.

Ndugu Obed anasema alipanda VIJITI 4,000 vya mbegu ya MKOMBOZI akafanikiwa kuvuna VIJITI 38,400 ndani ya Miezi 12. Kwa sasa, yeye amekuwa Mfanyabiashara wa MBEGU (Vijiti) ya MIhogo ya aina ya MKOMBOZI ambapo kila KIJITI anauza Shilingi 30.

MTAALAMU wa MEDA, Ndugu Isaack Musa amesema lengo kuu la Shirika lao ni kuendeleza mbegu bora za mihogo zinazostahimili magonjwa. Baada ya kupata MAFANIKIO kwa Mbegu ya MKOMBOZI, MEDA imeanzisha MASHAMBA DARASA ya mbegu nyingine za mihogo za aina ya MKUMBA, MKURANGA 1, T130, ORERA, KIROBA, EYOPE na F-10-30R katika Kata za Ifulifu, Mugango, Nyambono na Rusoli.

KIKUNDI cha TUMETAMBUA kinasudia kupanua MASHAMBA yake ya MIHOGO ili wapate MAVUNO ya ziada ya biashara.

Aidha, mbali na MAFANIKIO hayo KIKUNDI hiki kinatarajia kuanzisha Mradi wa MASHINE ya KUSAGA, kununua CHAREHANI za kushona nguo, na kununua VIFAA vya USEREMALA.

WANACHAMA wa Kikundi cha TUMETAMBUA wanatoa SHUKRANI kwa WADAU wa MAFANIKIO yao ambao ni:

*PCI Tanzania kwa kuwapatia Mbegu za Mahindi, Maharage, Alizeti na magunia ya kuhifadhia chakula.

*Jamii Impact kwa kuwapatia MKOPO wa Shilingi Million 5 (awamu ya kwanza), na awamu ya pili walikopeshwa Shilingi Million 8.

*SHIMAKIUMU kwa kuwapatia Mbegu za Mahindi, Dawa za Mimea na Viroba vya kupandia miche.

*MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo kuwapatia Mbegu za Mihogo, Mtama na Alizeti.

Prof Muhongo aligawa bure Jimboni mwao MAGUNIA 796 ya MBEGU (Vijiti) ya mihogo aina ya MKOMBOZI kama ifuatavyo:

Mwaka 2016/2017: MAgunia 446

Mwaka 2017 /2018: Magunia 350

MFUKO wa JIMBO kwa kuwapatia mashine na mipira ya umwagiliaji, na mbegu za bustani za mbogamboga.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Attachments area