RUWASA YAANZA KUTEKELEZA KWA KASI MRADI WA USAMBAZAJI MAJI KWENYE KATA YA NYAKATENDE

UTEKELEZAJI wa MRADI wa RUWASA wa kusambaza MAJI ya ZIWA VICTORIA kwenye Kata ya Nyakatende. 

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
RUWASA imeanza kujenga MIUNDOMBINU ya USAMBAZAJI wa MAJI ya ZIWA VICTORIA kwa Kata ya NYAKATENDE.
Kata ya NYAKATENDE ina Vijiji 4 ambavyo ni Kakisheri, Kamuguruki, Kigera na Nyakatende. Vijiji 2 (Kigera na Kakisheri) viko kwenye mwambao wa ZIWA VICTORIA na ndivyo vitaanza kusambaziwa MAJI ya Mradi huu, baadae Vijiji vya Kamuguruki na Nyakatende vitafuata.
MITAMBO ya kuvuta na kusafisha MAJI ya ZIWA inajengwa kwenye Kitongoji cha Kusenyi, Kijijini Kigera.
Sehemu ya Kijiji cha KURUKEREGE cha Kata jirani ya NYEGINA itapata MAJI ya Mradi huu, na sehemu nyingine ya Kijiji hicho itapewa MAJI ya MRADI wa MUWASA.
MENEJA wa MRADI huu wa RUWASA, Injinia Mohamed Said Yamlinga amesema MIUNDOMBINU inayojengwa kwa sasa ni:
*TENKI la MAJI lenye ujazo wa LITA 300,000 (laki tatu)
*OFISI ya Mradi
*VIOSKI vya kuzuia maji
*Kutandaza MABOMBA kwenye mitaro inayochimbwa.
MENEJA huyo amesema kuwa MRADI huu utakamilika Januari 2021.
WANANCHI na VIONGOZI wao wa Kata ya Nyakatende WANAISHUKURU sana SERIKALI yao kwa kutekeleza AHADI yake ya usambazaji wa MAJI SAFI na SALAMA Vijijini mwao.
Kata za jirani za ETARO, NYEGINA na IFULIFU zitapewa MAJI ya kutoka kwenye Mitambo ya MUWASA iliyoko Bukanga, Musoma Mjini. MRADI umeanza kutekelezwa.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini