WANAKIJIJI WAUNGWA MKONO NA SERIKALI KUJENGA NYUMBA ZA WALIMU

ujenzi wa NYUMBA MOJA ya WALIMU (kuanzia msingi hadi nyumba kukamilika) S/M BUIRA ya Kijiji cha Buira, Kata ya Bukumi.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
7.12.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
MWALIMU MKUU wa SHULE ya MSINGI BUIRA, Mwl Yahya Mgika amesema Shule hiyo iliyoanzishwa Mwaka 1992 ina jumla ya WANAFUNZI 747, WALIMU 8, NYUMBA 5 za Walimu, na ina Vyumba 8 vya Madarasa – bado kuna UPUNGUFU wa Vyumba 9 vya Madarasa.
SERIKALI imetoa SHILINGI MILIONI 25 kuchangia ujenzi wa NYUMBA MOJA ya WALIMU kwenye Shule hii. Fedha hizo zimetoka kwenye MRADI wa SERIKALI uitwao, “Primary Education Development Project (PEDP)”.
WANAKIJIJI wa Kijiji cha BUIRA, Kata ya BUKUMI wanaishukuru sana SERIKALI yetu kwa kutoa FEDHA hizo, na wao wamechangia NGUVUKAZI kuhakikisha kwamba gharama za ujenzi wa nyumba hiyo zinapungua – wamejitolea kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji.
MWENYEKITI wa Kijiji cha BUIRA, Ndugu Donald Mafwere ameeleza kwamba, mbali ya MCHANGO wa NGUVUKAZI, Wanakijiji walichangia SARUJI MIFUKO 70, MBAO vipande 101 na MABATI 52 kwenye ujenzi huu.
MWENYEKITI huyo anawashukuru sana WANAKIJIJI hao kwa kuona umuhimu wa KUJITOLEA kwa ajili ya MAENDELEO yao wenyewe wakisaidiana na SERIKALI yetu. Wanavijiji hawa walishajenga NYUMBA 4 za WALIMU wa Shule hiyo.
MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo anapewa SHUKRANI nyingi kwa kuichangia Shule hiyo MADAWATI 60, VITABU zaidi ya 1,000 vya Maktaba, SARUJI MIFUKO 60, na MABATI 54.
VIONGOZI 2 hao, yaani Mwenyekiti wa Kijiji na Mwalimu Mkuu, kwa pamoja wanaomba WADAU wa MAENDELEO wakiwemo WAZALIWA wa Kata ya BUKUMI wajitokeze kuchangia ujenzi wa Vyumba Vipya vya Madarasa, Nyumba Mpya za Walimu na Maktaba – MPANGOKAZI wa ujenzi umeishatayarishwa.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini