PROGRAMU YA WAKULIMA KUPUNGUZA MATUMIZI YA JEMBE LA MKONO INAENDELEA MUSOMA VIJIJINI

Kikundi cha Wakulima¬† wa Kijiji cha Buanga, Kata ya Rusoli, kiitwacho “NGUVUKAZI” kikiwa katika shambalao walilolima kwa kutumia PLAU waliyopewa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

Tarehe, 29.11.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo anaendelea KUGAWA bure PLAU (majembe ya kukokotwa na ng’ombe au punda) kwa VIKUNDI vya WAKULIMA wa Jimbo la Musoma Vijijini. MGAO mwingine utakuwa wa ZAWADI ya KRISMASI & MWAKA MPYA utafanyika tarehe 24 Disemba 2020.
Kikundi kiitwacho, “NGUVUKAZI”, cha Kijiji cha Buanga, Kata ya Rusoli ni moja ya VIKUNDI vilivyokwishapewa PLAU na MBEGU kutoka kwa Mbunge huyo.
Kikundi cha NGUVUKAZI kilianzishwa Mwaka 2015 na kina WANACHAMA 30 wanaolima MAZAO ya CHAKULA na BIASHARA. Kikundi hiki kinagawia SHULE za MSINGI Bwenda A&B 50% ya MAVUNO ya Mazao yake ya CHAKULA.
MWENYEKITI wa Kikundi hicho, Ndugu Tore Masamaki anasema MISAADA ya NYEZO zao za Kilimo imetolewa na PCI (Tanzania) na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo.
PCI (Tanzania) imewapatiwa MASHINE ya UMWAGILIAJI, MBEGU za Viazi Lishe, Mahindi na Alizeti.
Mbunge Prof Muhongo amewapatia PLAU 1 na MBEGU za Mihogo, Mtama, Ufuta na Alizeti
Vilevile, kwa Kata ya Rusoli, Mbunge huyo aligawa PLAU 1 kwa Kikundi kingine kiitwacho “MKULIMA JEMBE”.
Ndugu Anna Masange, MWANAKIKUNDI cha NGUVUKAZI amesema kwamba ameweza kujenga NYUMBA, ANASOMESHA WATOTO wake na kufungua BIASHARA ya DUKA dogo kutokana na MAPATO ya Kilimo cha Kikundi chao. Kwa hiyo, anawashawishi WANAWAKE na VIJANA wajiunge kwenye VIKUNDI vya KILIMO vina manufaa sana.
AFISA KILIMO wa Kata ya Rusoli, Ndugu Gervas Ngova. amesema WANAVIJIJI wa Kata hiyo wamechangamkia fursa za kuanzisha VIKUNDI vya KILIMO kwani vinawarahisishia kupata MAFUNZO na MISAADA ya Kilimo kutoka kwa WADAU wa MAENDELEO ikiwemo SERIKALI yetu.
Vilevile, hapo shambani, Afisa Kilimo wa Kata hiyo anatoa MAELEKEZO ya Kilimo bora kwa Kikundi cha “NGUVUKAZI”.
KILIMO NI UHAI
KILIMO NI AJIRA
KILIMO NI UCHUMI
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini