CRDB YAUNGANA NA WANAKIJIJI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA SHULE YA MSINGI ILIYOFUNGULIWA MWAKA 1956

Baadhi ya MAJENGO yaliyokamilika ujenzi na MADARASA ya S/M MURUNYIGO ya Kijiji cha Kiemba, Kata ya Ifulifu.

Tarehe, 27.11.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
SHULE ya MSINGI MURUNYIGO ya Kijiji cha Kiemba, Kata ya Ifulifu ilianza kutoa ELIMU Mwaka 1956.
SHULE hii ina WANAFUNZI 949 na WALIMU 12. IDADI ya WANAFUNZI kwenye chumba kimoja cha DARASA ni kati ya 80 na 152. Kwa hiyo, MIRUNDIKANO Madarasani ipo!
AFISA MTENDAJI (VEO) wa Kijiji cha Kiemba. Ndugu Regina Chirabo amesema kuwa UBORESHAJI wa MIUNDOMBINU ya S/M MURUNYIGO umefanywa na:
*WANAKIJIJI:
Wamechangia NGUVUKAZI kwa kusomba mawe, mchanga, maji na FEDHA taslimu 2,200,000/= za malipo ya Fundi.
*BENKI YA CRDB
Imechangia Saruji Mifuko 60, Rangi Lita 40, Vifaa vya Mlango 1 na Dirisha 1 – SHUKRANI nyingi sana kwa CRDB.
*PCI (TANZANIA)
Imefadhili ujenzi wa Choo chenye Matundu 10 (Wasichana 5 na Wavulana 5 – kwenye picha zilizoko hapa utaona Jengo la rangi ya “light blue”) – SHUKRANI nyingi sana kwa PCI (Tanzania).
*MBUNGE WA JIMBO
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo amechangia Saruji Mifuko 60 na Mabati 54.
MICHANGO mingine ya MBUNGE huyo kwenye Shule hiyo ni pamoja na: Madawati 150 na Vitabu vya Maktaba zaidi ya 1,000 (elfu moja).
MWALIMU MKUU huyo amesema Jumla vya Vyumba vya Madarasa vinavyohitajika ni 18 na vilivyopo ni 9 tu!Mbali ya UPUNGUFU mkubwa huo WANAFUNZI 59 kati ya 64 wamefaulu kujiunga MASOMO ya KIDATO I mwakani!
MWALIMU MKUU huyo anaendelea KUTOA OMBI kwa WADAU wa MAENDELEO kujitokeza na KUCHANGIA uboreshaji na ujenzi wa MIUNDOMBINU kwenye Shule kongwe ya Msingi ya Kijiji cha Kiemba, S/M MURUNYIGO.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini