ILANI MPYA YA CCM INATOA MAJIBU YA KERO & VIPAUMBELE VYA WANANCHI WA KATA YA NYAMRANDIRIRA

Kata ya Nyamrandirira ina Vijiji 5 (Chumwi, Kaboni, Kasoma, Mikuyu na Seka) na kila KIJIJI kinakiri kwamba ILANI MPYA ya UCHAGUZI ya CCM (2020-2025) ndiyo pekee inatoa MAJIBU ya Kero na Vipaumbele vya MAENDELEO na USTAWI wa Vijiji vyao.
Hayo yamebainika wakati wa MIKUTANO 4 ya KAMPENI ya Mgombea Ubunge wa CCM wa Jimbo la Musoma Vijijini, PROF MUHONGO.
* ELIMU – SEKONDARI MPYA YA KATA
Vijiji vyote 5 vinachangia ujenzi wa SEKONDARI ya PILI ya Kata yao. SEKONDARI hii (Seka Secondary School) itafunguliwa Januari 2021.
*KIJIJI CHA MIKUYU
VIPAUMBELE vya Kijiji hiki ni MAJI, UMEME na ZAHANATI.
Ujenzi wa ZAHANATI ya Kijiji chao utaanza  baada ya UCHAGUZI wa tarehe 28.10 2020 kwa kutumia NGUVUKAZI na MICHANGO ya Wanakijiji na Viongozi wao.
MAJI – Kijiji hiki kiko kwenye Mradi wa BOMBA la Maji ya kutoka Ziwa Victoria (Kijijini Chumwi) kwenda Mabui Merafuru na Mikuyu. USANIFU wa awali unapitiwa upya na RUWASA kwani awali Vijiji vya Nyambono na Saragana vilikuwa ndani ya Mradi huu. Kwa sasa vijiji hivyo vimepelekwa kwenye  Mradi wa Suguti – Wanyere/Chirorwe.
UMEME- Miundombinu ya Usambazaji wa UMEME ipo na baadhi ya Wanavijiji tayari wameunganishiwa umeme. Kazi inaendelea na itakamilika kama isemavyo ILANI MPYA ya CCM.
* KIJIJI CHA CHUMWI
VIPAUMBELE vya Kijiji hiki vinafanana na vile vya Kijiji cha Mikuyu kasoro  Zahanati. UTEKELEZAJI wa Miradi yake ya MAJI & UMEME unafana na ule wa Kijiji cha Mikuyu.
* KIJIJI CHA KASOMA
MAJI ya Kijiji hiki yatatolewa Ziwa Victoria. Kijiji hiki kiko kwenye orodha ya Vijiji 33 vya Jimboni mwetu vilivyo kwenye Mradi wa MAZIWA MAKUU.
UMEME – ni kama ilivyoelezwa hapo juu kwenye Kijiji cha Mikuyu.
* VIJIJI VYA KABONI & SEKA
MAJI ya Vijiji hivi yatatolewa kwenye BOMBA la MAJI la MGODI wa SEKA ambalo chanzo chake kiko Kijijini Kaboni. Baadhi ya Wanavijiji tayari wanahudumiwa na Bomba hili.
UMEME – Baadhi ya Wanaviviji ndani ya Vijiji hivi viwili tayari wameunganishiwa umeme. Vitongoji vilivyosalia vitapewa UMEME na kazi ya usambazaji inaendelea.
ELIMU – Kijiji cha KABONI kinashughulikia suala ya ardhi kwa ajili ya ujenzi wa SHULE ya MSINGI yao. Kijiji hakina Shule ya Msingi.
MGOMBEA URAIS WA CCM (DKT MAGUFULI) ameahidiwa KURA ZOTE (100%) kutoka Kata Nyamrandirira
VIAMBATANISHO vya hapa:
Kwaya, Shairi, Igizo kutoka Kata ya Nyamrandirira
“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA”
Sospeter Muhongo
Jimbo la Musoma Vijijini
8 Oktoba 2020