ARI KUBWA YA WANAVIJIJI KUCHANGIA MAENDELEO YAO WAIWEKA PAZURI KATA YA MUGANGO – WANAANZA UJENZI WA MABWENI WAWE NA “HIGH SCHOOL” MWAKANI

Tarehe 8.10.2020, MGOMBEA UBUNGE wa CCM wa Jimbo la Musoma Vijijini, PROF MUHONGO, alifanya MIKUTANO 2 ya KAMPENI ndani ya Kata ya Mugango.
Mbali ya kunadi SERA za CCM, Prof Muhongo alijadili UTEKELEZAJI wa MIRADI ya KIPAUMBELE ya Kata hiyo – hii ikiwa ni sehemu ya matayarisho ya UTEKELEZAJI wa ILANI MPYA ya CCM baada ya UCHAGUZI wa tarehe 28.10.2020.
KIPAUMBELE CHA ELIMU:
KATA ya MUGANGO yenye Vijiji 3 (Kwibara, Kurwaki, Nyang’oma) inaanza KUTEKELEZA ILANI MPYA ya CCM (2020-2025) kwa KUJENGA MABWENI 3 ili mwakani (Julai 2021) iwe na Kidato cha V & VI.
Vilevile, Kata hiyo imeamua kujenga SEKONDARI ya PILI kwenye eneo la katikati ya Vijiji vya Kurwaki na Nyang’oma.
MAFANIKIO makubwa ya WANANCHI kukubali  KUCHANGIA MAENDELEO YAO (nguvukazi & michango ya fedha taslimu) yako dhahiri:
* Vyumba vya Madarasa ya Shule zao za Msingi  na Sekondari ya Mugango havina mirundikano ya Wanafunzi.
* MAABARA za Mugango Sekondari zinajengwa
* Vyoo vya kutosha vipo mashuleni
* Bustani za shule zipo
KIPAUMBELE CHA AFYA:
* KITUO cha AFYA cha Mugango tayari kimekamilika kwa USHIRIKIANO MZURI wa WANANCHI na SERIKALI yao ya CCM
* ZAHANATI ya Kijiji cha Kurwaki itakamilishwa ikiwa ni moja ya MAFANIKIO ya UTEKELEZAJI wa ILANI MPYA ya CCM.
* VITENDO KWANZA
* MAENDELEO KWANZA
ILANI MPYA YA CCM YAKUBALIKA SANA
* MAJI VIJIJINI – Kata ya Mugango yenye CHANZO (Ziwa Victoria) cha BOMBA la MAJI ya Kiabakari na Butiama, itaendelea kupata MAJI kutoka kwenye BOMBA hilo la zamani ambalo limechakaa!
MRADI mkubwa wa Tsh Bilioni 70 wa BOMBA la MAJI la Mugango – Kiabakari – Butiama utaanza kutekelezwa hivi karibuni na VIJIJI vya Kata za MUGANGO na TEGERUKA vitapewa MAJI safi na salama kutoka kwenye BOMBA hili jipya.
* UMEME VIJIJINI – Kama ilivyoandikwa ndani ya ILANI MPYA ya CCM, WANANCHI wa Kata ya Mugango wana imani kubwa sana na SERIKALI ya CCM kukamilisha USAMBAZAJI wa UMEME kwenye Vitongoji vilivyosalia.
IDADI YA KURA KUTOKA KATA YA MUGANGO
* Dkt Magufuli: 100%
* Prof Muhongo: 100%
* Ndg Charles Magoma: 100%
VIAMBATANISHO vya hapa:
* Kwaya ya Mugango
* Matukio mengine ya Mikutano 2 ya Kampeni
“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA”
Sospeter Muhongo
Jimbo la Musoma Vijijini
9 Oktoba 2020