MIKUTANO 3 YA KAMPENI NDANI YA KATA YA NYAMBONO YAMKUBALI SANA DKT MAGUFULI

Leo, Jumanne, 6.10.2020 MGOMBEA UBUNGE wa CCM wa Jimbo la Musoma Vijijini, PROF MUHONGO ameenda Kijijini Nyambono, Kijijini Saragana na kwenye Kitongoji cha Nyabherango KUOMBA KURA za WAGOMBEA  wa CCM wa nafasi za Urais, Ubunge na Udiwani.

DKT MAGUFULI anakubalika kwa Asilimia Miamoja  (100%). SABABU KUU zikiwa:

(i) MAJI ya ZIWA VICTORIA

Vijiji 2 vya Kata ya Nyambono (Saragana & Nyambono) viko mbali na Ziwa Victoria na hivi karibuni vitapata MAJI ya Ziwa hilo kupitia MRADI wa BOMBA la MAJI wa Suguti-Wanyere/Chirorwe ambapo BOMBA hilo litapaleka MAJI kwenye Vijiji hivyo. Ujenzi wa TENKI kubwa la MAJI kwenye Mlima Nyabherango utaanza hivi karibuni (Bajeti ya Mwaka huu).

(ii) UMEME wa REA:

Vitongoji vya Kata hiyo vilivyosalia vitapewa umeme – ILANI MPYA ya CCM (2020-2025) imebainisha hivyo.

VIPAUMBELE MAALUM

* KIJIJI CHA NYAMBONO

WANANCHI wa Kijiji hiki WAMEAMUA kwa KAULI moja kwamba kwa MIAKA 5 ya UTEKELEZAJI wa ILANI ya CCM (2020-2025) watajenga SEKONDARI yao. Kwa sasa WATOTO wao wanatembea umbali wa zaidi ya KILOMITA 6 kwenda  masomoni kwenye SEKONDARI ya NYAMBONO iliyoko Kijijini Saragana.

Vilevile, WANANCHI hawa  na WADAU  wao wa MAENDELEO watakamilisha ujenzi wa ZAHANATI ya Kijiji chao.

WATOTO wa Kitongoji cha Nyabherango wanaenda  masomoni kwenye SHULE za MSINGI za mbali na kwao (zaidi ya kilomita 5).  Kitongoji hicho kinatafuta ardhi kianze kujenga SHULE SHIKIZI.

* KIJIJI CHA SARAGANA

Kitongoji cha Kabise kitajenga SHULE SHIKIZI kutatua tatizo sugu la mwendo mrefu ambao WATOTO wao wanatembea kwenda masomoni kwenye SHULE za MSINGI za Vitongoji vingine.

* MIRADI MINGINE ni kama ilivyoainishwa kwenye ILANI MPYA ya CCM ya 2020-2025.

“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA”

Sospeter Muhongo

Jimbo la Musoma Vijijini

6 Oktoba 2020