KAMPENI ZA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI NI KAMPENI ZA UCHUMI & MAENDELEO – KATA YA BUGWEMA ITAENDELEA KUPANUA KILIMO CHA ALIZETI

KATA ya BUGWEMA yenye VIJIJI 4 (Bugwema, Masinono, Muhoji na Kinyang’erere) ndiyo inayoongoza kwenye KILIMO cha MAZAO MCHANGANYIKO (alizeti, pamba, mahindi, mihogo, mpunga, mtama, dengu, vitunguu, nyanya, viazi, n.k.) ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.

Jana, wakati wa KAMPENI za CCM kwenye Vijiji vya Bugwema na Masinono, KILIMO kiliwekewa mkazo sana.

Matayarisho ya MRADI mkubwa wa KILIMO cha UMWAGILIAJI kwenye BONDE LA BUGWEMA unaendelea ndani ya SERIKALI yetu.

ELIMU & MAFUNZO ni KIPAUMBELE kingine cha Kata hii ambayo VIJIJI vyake 4 viko mbalimbali. Kwa mfano, kutoka Muhoji hadi Masinono (kwenye SEKONDARI yao ya Kata) ni mwendo usiopungua kilomita 11. Kwa hiyo, SEKONDARI MOJA haitoshi. WANANCHI wamependekeza SEKONDARI 2 MPYA zijengwe kwenye VIJIJI vya Muhoji na Bugwema ndani ya MIAKA 5 ya UTEKELEZAJI wa ILANI MPYA ya CCM (2020-2025).

BARAZA LA MADIWANI liliishaamua kupanua BUGWEMA SEKONDARI na kuwa na “HIGH SCHOOL” ya Wasichana (Bugwema Girls High School). Uamuzi huu UTATEKELEZWA ndani ya MIAKA 5 ya UTEKELEZAJI wa ILANI MPYA ya CCM.

WANANCHI wanayo imani kubwa na SERIKALI ya CCM kuendelea kusambaza UMEME kwenye Vitongoji vilivyosalia.

Ndani ya MIAKA 5 (2020-2025), RUWASA imeahaidi kusambaza MAJI kutoka Ziwa Victoria kwenda kwenye VIJIJI 4 vya Kata hii.

ZAHANATI ya Masinono, yenye GARI la WAGONJWA (Ambulance) walilopewa na Prof Muhongo, IMEPOKEA Tsh MILIONI 400 kutoka SERIKALINI kwa ajili ya upanuzi wake wa kuwa KITUO cha AFYA  – KURA za DKT MAGUFULI ni NYINGI kweli kweli!

MASUALA ya UKABILA yamekewa sana na WANANCHI wa KATA ya BUGWEMA wamehaidi kutoa KURA zaidi ya 98% kwa WAGOMBEA wa CCM kwenye nafasi za URAIS (Dkt Magufuli), UBUNGE (Prof Muhongo) na UDIWANI (Ndugu Clifford Machumu).

UTAMADUNI, MICHEZO & SANAA – ILANI MPYA CCM – Kata ya Bugwema iko tayari kwenye UTEKELEZAJI wake

“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA”

Sospeter Muhongo

Jimbo la Musoma Vijijini

4 Oktoba 2020