JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI – ILANI MPYA YA UCHAGUZI YA CCM (2020-2025) KUANZA KUTEKELEZWA TAREHE 1 NOVEMBA 2020

Prof MUHONGO akiwa na BODABODA wa Kijiji cha Kataryo

WANANCHI wa Kata ya TEGERUKA WAMEAMUA kujenga SEKONDARI ya PILI ili kutatua tatizo la mwendo mrefu wanaotembea WANAFUNZI wa SEKONDARI wa Kata hiyo.
KATA hiyo yenye VIJIJI 3 (Kataryo, Mayani & Tegeruka) vilivyo mbali mbali ina SEKONDARI moja. WANAFUNZI kutoka Vijiji vya Kataryo na Mayani wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya KILOMITA 15 kwenda masomoni TEGERUKA SEKONDARI.
Tarehe 1.11.2020, WANANCHI wanaanza ujenzi wa SEKONDARI ya PILI ya Kata yao itakayojengwa eneo lililo katikati ya Vijiji vya Kataryo na Mayani. WAGOMBEA UBUNGE (Prof S Muhongo) na UDIWANI (Askofu A M Mashauri) WAMEKUBALI KUSHIRIKIANA na WANANCHI hao kujenga Sekondari hiyo.
WANANCHI wa Kata ya Kataryo WAMEFURAHI na KUSHUKURU sana SERIKALI yao baada ya kuambiwa kwamba MRADI wa BOMBA la MAJI kutoka Ziwa Victoria (Mugango) kwenda Kiabakari na Butiama litakuwa na MATOLEO ya MAJI ndani ya VIJIJI vyote VITATU vya Kata hiyo. MRADI huo utagharimu TSH BILIONI 71 (bilioni sabini na moja) ambazo ZIMEISHATOLEWA na Serikali ya SAUDI ARABIA, BADEA na SERIKALI yetu. Utekelezaji wake unaanza hivi karibuni.
Sospeter Muhongo
Jimbo la Musoma Vijijini
19.9.2020