PLAU NYINGINE 50 KUGAWIWA KWA VIKUNDI VINGINE 50 VYA WAKULIMA WA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Wakulima wakitumia PLAU walizopewa bure na Prof Sospeter Muhongo

Jumatatu, tarehe 13 Julai 2020, Prof Sospeter Muhongo alinunua PLAU 50 (majembe ya kukokotwa na ng’ombe) kwa ajili ya kuzigawa siku ya Sherehe za WAKULIMA (8.8.2020, NANENANE).
Prof Muhongo amefanya hivyo kwa kuzingatia TARATIBU za UCHAGUZI ambapo ltarehe 13 Julai 2020 ndiyo siku ya mwisho ya kutekeleza AHADI za waliokuwa WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. PLAU hizo zitagawiwa tarehe 8.8.2020 (NANENANE) na Mkuu wa Wilaya (DC) ya Musoma.
PROGRAMU YA KUPUNGUZA MATUMIZI MAKUBWA YA JEMBE LA MKONO
Prof Muhongo AMEANZISHA PROGRAMU hiyo ikiwa ni sehemu ya  LENGO kuu la KUBORESHA KILIMO ndani ya VIJIJI 68 vya Jimbo la Musoma Vijijini.
JUMLA YA PLAU 85 zimeishagawiwa kwa VIKUNDI 85 vya WAKULIMA wa Jimbo la Musoma Vijijini. LENGO KUU ni kuwa na angalau  PLAU 20 kwa kila Kijiji.
WAKULIMA wameelezwa mara kadhaa namna ya kupata MIKOPO ya KUNUNUA MATREKITA. Ofisi ya Kilimo ya HALMASHAURI yetu (Musoma DC) ipo tayari kuwasaidia kutuma MAOMBI ya MIKOPO yao.
MBEGU BORA zimeishagawiwa kwa WAKULIMA wa Jimbo la Musoma Vijijini. Hizo ni: Mbegu za ALIZETI (tani 20), MIHOGO, MTAMA na UFUTA.
KARIBUNI TUCHANGIE UBORESHAJI wa KILIMO ndani ya VIJIJI 68 vya Jimbo la Musoma Vijijini.