WATOTO CHINI YA MIAKA 6 WAJENGEWA SHULE VIJIJINI MWAO

WANAVIJIJI wakiwa kwenye ujenzi wa Shule SHIKIZI KARUSENYI, Kijijini Mikuyu, Kata ya Nyamrandirira, na Jengo lilokamilishwa la Shule SHIKIZI EGENGE, Kijijini Busamba, Kata ya Etaro

Prof Sospeter Muhongo ameendelea KUCHANGIA UJENZI wa SHULE SHIKIZI ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
Leo, Ijumaa, tarehe 10 Julai 2020, Prof Muhongo AMETOA MICHANGO ifuatayo:
* MABATI 54 ya Geji 28 ya kuezekea Darasa moja kwenye Shule SHIKIZI KARUSENYI ya Kitongoji cha Mtakuja, Kijiji cha Mikuyu, Kata ya Nyamrandirira
* SARUJI MIFUKO 100 kwa ujenzi wa Vyumba bora vya Madarasa ya Shule SHIKIZI KIUNDA ya Kijijini Kamuguruki, Kata ya Nyakatende. Darasa linalotumiwa ni la matofali ya tope.
JIMBO la Musoma Vijijini linajenga SHULE SHIKIZI 11 kwa ajili ya kutatua MATATIZO sugu ya:
* Wanafunzi wa Madarasa ya Awali (chini ya miaka 6) kusomea chini ya miti.
* Wanafunzi chini ya umri wa miaka 6 kutembea umbali mrefu kwenda masomoni
* Mirundikano madarasani
IDADI YA SHULE ZA MSINGI MUSOMA VIJIJINI (Vijiji 68)
* Shule SHIKIZI 11 zinajengwa, zikiwemo hizo zilizochangiwa leo vifaa vya ujenzi. Nyingine zimeanza kupokea Wanafunzi.
* Shule za Msingi za SERIKALI ni 111
* Shule za Msingi za BINAFSI ni 3
UJENZI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU & VIFAA VYA SHULE KWENYE SHULE ZA MSINGI
* MADAWATI zaidi 10,000 yalishagawiwa mashuleni
* VITABU vingi vya Maktaba vilishagawiwa
* VYUMBA vipya zaidi ya 450 vya Madarasa vilishajengwa
* PCI (USA) na WADAU wengine wa Maendeleo wanaendelea kuchangia ujenzi MAKTABA na VYOO kwenye baadhi ya Shule za Msingi
MATOKEO MAZURI YAANZA KUPATIKANA
* Uboreshaji wa MIUNDOMBINU & VIFAA vya Shule kwenye Shule za Msingi za Musoma Vijijini UMEANZA KUZAA MATUNDA MAZURI kwa mfano:
Mwaka jana (2019), Shule za Msingi za MUSOMA VIJIJINI zilishika NAMBA ya KWANZA kwenye MITIHANI ya DARASA LA NNE (IV) ndani ya Mkoa wa Mara – huko nyuma nafasi yao ilikuwa mkiani!
KARIBUNI TUJENGE SHULE ZA MSINGI zenye MIUNDOMBINU mizuri & VIFAA vizuri vya Shule vijijini mwetu.