UJENZI WA WODI YA MAMA NA MTOTO KISIWANI RUKUBA

Ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto kwenye Zahanati ya Kisiwa cha Rukuba – hatua hiyo ya ujenzi imefikiwa ndani ya muda wa wiki 2 (kasi kubwa)

Jumamosi, tarehe 4.7.2020, Prof Sospeter Muhongo, alikamilisha AHADI  yake ya KUCHANGIA SARUJI MIFUKO 200 (mia mbili) kwa ajili ya ujenzi wa Wodi ya Mama & Mtoto kwenye Zahanati ya Kisiwa cha Rukuba. Prof Muhongo alitoa AHADI hiyo kabla muda wake wa UBUNGE kufikia tamati.
HALI YA HUDUMA YA AFYA MUSOMA VIJIJINI
* Zahanati 24 za Serikali
* Zahanati 4 za Bunafsi
* Zahanati 14 zinajengwa kwa nguvu za WANANCHI kwa kushirikiana na Serikali
* Wodi za Mama na Mtoto zinajengwa kwenye Zahanati za Bukima, Nyegina na Kisiwa cha Rukuba.
* Vituo vya Afya 2 (Murangi & Mugango)
* Kituo cha Afya Bugwema – Zahanati  ya Kijiji cha Masinono inapanuliwa iwe Kituo cha Afya cha Kata ya Bugwema.
* Hospitali ya Wilaya inajengwa Kijijini Suguti, Kitongoji cha Kwikonero.
MAGARI YA WAGONJWA (Ambulances):
Yapo 5: Kwenye Zahanati za Masinono, Kurugee na Nyakatende, na kwenye Vituo vya Afya vya Murangi na Mugango.
Jimbo la Musoma Vijijini lina Kata 21, Vijiji 68 na Vitongoji 374.
KARIBUNI TUCHANGIE UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA AFYA MUSOMA VIJIJINI