WANANCHI KISIWANI RUKUBA  WAJENGA MSINGI WA JENGO LA WODI YA MAMA NA MTOTO LENYE VYUMBA 13 KWA MUDA WA WIKI MOJA 

ujenzi wa WODI ya MAMA na MTOTO kwenye ZAHANATI ya KISIWA cha RUKUBA, Kata ya Etaro. WODI hiyo itakamilika na kutumika kabla ya tarehe 1 Disemba 2020.

KISIWA cha RUKUBA kimo ndani ya Kata ya Etaro ambayo ni moja ya Kata 21 za Jimbo la Musoma Vijijini.
Baadhi ya MAFANIKIO makubwa ya KISIWA cha RUKUBA ni haya hapa:
SHULE YA MSINGI RUKUBA ina:
* Wanafunzi 434
* Walimu 7
* Maktaba yenye Vitabu mbalimbali
* Vyumba vya Madarasa 10 – Vyumba 2 vinahitaji matengenezo
* Nyumba za Walimu 8 – Nyumba 2 zinahitaji matengenezo
* Wanafunzi na Walimu wanapata chakula cha mchana hapo Shuleni
UMEMEJUA (SOLAR):
Umeanza kufungwa hapo Kisiwani. Wakazi wanaomba kasi iongezeke.
MAJI YA BOMBA:
Kisiwa cha Rukuba ni moja kati ya VIJIJI 33 vilivyoko kwenye MRADI wa MAZIWA MAKUU. Serikali inajitayarisha kuanza kuutekeleza Mradi huu.
ZAHANATI YA KISIWA CHA RUKUBA
* Wafanyakazi 4
* Nyumba 1 ya Wafanyakazi (two in one)
* Maabara yenye Darubini 1
UJENZI WA WODI YA MAMA NA MTOTO
WANANCHI wa Kisiwa cha Rukuba wameamua kuongeza HUDUMA za AFYA kwenye ZAHANATI yao kwa kujenga WODI ya MAMA na MTOTO. Jengo hill lina Jumla ya VYUMBA 13 na MSINGI wake umejengwa kwa KASI KUBWA sana na kukamilika ndani ya muda wa WIKI MOJA!
WANANCHI hao wanachangia NGUVUKAZI (kusomba mawe, mchanga na maji). FEDHA zinazotumika kwa sasa ni zile za MAKUSANYO yao (20%) zinazorudishwa na HALMASHAURI yetu (Musoma DC).
MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo atachangia SARUJI MIFUKO 200 kulingana na KASI ya ujenzi wa WODI hiyo na tayari ameishachangia Saruji Mifuko 100 kufikia leo (13.6.2020).