WANAVIJIJI WAAMUA KUJENGA VYUMBA VIPYA 5 VYA MADARASA NA SERIKALI YACHANGIA UJENZI HUO

MAFUNDI wakiwa kwenye kazi za ujenzi wa VYUMBA VIPYA vya Madarasa ya S/M BWASI B ya Kijiji cha Bwasi, Kata ya Bwasi.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
UBORESHAJI wa MIUNDOMBINU ya ELIMU umetiliwa MKAZO mkubwa sana Mkoani Mara. UBORESHAJI huu umebainika kuwa njia mojawapo ya KUINUA KIWANGO cha UBORA wa ELIMU ndani ya Mkoa huu.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) imechanga Tsh MILIONI 5 kwa ajili ya ujenzi wa VYUMBA VIPYA 5 kwenye S/M BWASI B.
S/M BWASI B iko Kijijini Bwasi ndani ya Kata ya Bwasi. Shule hii ilianza Mwaka 2015, ina jumla ya WANAFUNZI 512 na WALIMU 7.
MWALIMU MKUU wa Shule hii, Mwl Masilingi Maira amesema Shule ina VYUMBA 4 vya Madarasa huku MAHITAJI ni VYUMBA 8. Kwa hiyo, WANAFUNZI wa Madarasa 3 WANASOMEA chini ya MITI, huku Darasa moja likiwa na MRUNDIKANO wa WANAFUNZI 118.
MTENDAJI wa Kijiji cha Bwasi, Ndugu Gabriel Chacha ameeleza kwamba, kwa sasa, WANAKIJIJI   wamekubali na kuhamasika KUTATUA MATATIZO SUGU la kutokuwepo Vyumba vya Madarasa na Ofisi za Walimu za kutosha Shuleni hapo.
KIONGOZI huyo amesema WANANCHI wameanza ujenzi wa VYUMBA VIPYA 5 vya Madarasa na OFISI 3 za WALIMU. Mbali ya kuchangia NGUVUKAZI zao (kusomba mawe, mchanga na maji ya ujenzi), WANAVIJIJI hao wanachangia Tsh 14,000/= kutoka kila KAYA.
SERIKALI ya Kijiji cha Bwasi IMECHANGIA fedha za kununua MBAO za UPAUAJI wa VYUMBA VIPYA 4 vya Madarasa na HALMASHAURI yetu (Musoma DC) imechangia Tsh MILIONI 5 kwa ajili ya UPAUAJI huo  – HONGERENI sana VIONGOZI wa Serikali ya Kijiji cha Bwasi na VIONGOZI wa HALMASHAURI yetu.
WANANCHI wa KIJIJI cha BWASI na Kata nzima ya Bwasi WANATOA SHUKRANI nyingi sana kwa:
PCI (Project Concern International, USA) kwa kujenga vyoo, tanki la maji na kuwezesha MRADI wa CHAKULA cha Wanafunzi kwenye S/M Bwasi B na nyingine ndani ya Kata ya Bwasi – Ahsante sana PCI.
BMZ (The Federal Ministry of Economic Development and Cooperation, Germany)  – Mradi huu umetoa madaftari, kalamu, mabegi ya kubebea vifaa vya shule, miwani na matibabu maalumu kwa WANAFUNZI wenye ULEMAVU kwa Shule zote za msingi ndani ya Kata ya Bwasi –  Ahsante sana BMZ.
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ametoa MICHANGO ifuatavyo:
(i) S/M BWASI B:
Saruji Mifuko 70, Madawati 36, Vitabu vingi vya Maktaba
(ii) S/M BWASI:
Saruji Mifuko 50, Madawati 39 na Vitabu vingi vya Maktaba.
OMBI KUTOKA KWA WANAKIJIJI wa Kijiji cha Bwasi
WAZALIWA wa  Kijiji cha Bwasi na WADAU wengine wa MAENDELEO wanaombwa kuchangia MABATI 162 ili UPAUAJI wa VYUMBA VIPYA vya Madarasa UKAMILIKE kabla ya WANAFUNZI kurudi Shuleni hapo (S/M Bwasi B) kuendelea na masomo yao.