KATA YA BWASI YAENDELEA KUBORESHA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

baadhi ya WANAKIKUNDI cha NO SWEAT NO SWEET wakiwa kazini kwenye MASHAMBA yao ya MPUNGA na MATIKITI Kijijini Bugunda, Kata ya Bwasi.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
KATA ya BWASI ina Vijiji 3 ambavyo ni Bugunda, Bwasi na Kome. Vijiji 2 –  Bugunda na Bwasi viko kwenye mwambao wa Ziwa Victoria.
KIKUNDI cha NO SWEAT NO SWEET cha Kijiji cha Bugunda kinajishughulisha na KILIMO cha BUSTANI (nyanya, vitunguu na matikiti)  na KILIMO cha MAZAO ya CHAKULA na BIASHARA (mahindi, maharage, viazi lishe na mpunga)
KATIBU wa KIKUNDI hicho, Ndugu Daudi Silas ameeleza kwamba kwa sasa HAWASUBIRI MVUA KUNYEESHA kwani KILIMO chao ni cha UMWAGILIAJI hata kwenye kilimo cha MPUNGA.
KIKUNDI hiki kina MASHINE 2 za UMWAGILIAJI. Mashine ya kwanza ilinunuliwa kwa kutumia FEDHA za MFUKO wa JIMBO na Mashine ya pili WAMEJINUNULIA WENYEWE  – hongereni sana Wanachama wa NO SWEAT NO SWEET!
Vilevile, KIKUNDI hiki tayari kimenunua NG’OMBE 2 kwa ajili ya KILIMO cha kutumia PLAU. Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo amekubali maombi yao ya kupewa PLAU (jembe la kukokotwa na ng’ombe) ikiwa ni ZAWADI ya EID al FITR
MBUNGE huyo ATAGAWA BURE PLAU 40 ikiwa ni ZAWADI yake ya EID al FITR (2020) kwa VIKUNDI 40 kutoka VIJIJI 40 vya Jimbo la Musoma Vijijini. MGAO huo wa tatu utafikisha jumla ya PLAU 85 ambazo Mbunge huyo atakuwa amegawa bure kwenye VIKUNDI 85 vya Jimbo la Musoma Vijijini lenye Vijiji 68 – PROGRAMU hii ya UBORESHAJI wa KILIMO Jimboni humo ni ENDELEVU!
Kwa sasa, WANACHAMA wa KIKUNDI CHA KILIMO cha NO SWEAT NO SWEET wanasomesha watoto wao bila matatizo na wameanza kujenga bora za kisasa za kuishi – hongereni sana ndugu zetu kwa MAFANIKIO hayo.
KIKUNDI cha KILIMO cha JIPE MOYO cha Kijijini Kome kinaendelea kuboresha kilimo chao kwa kutumia PLAU waliyopewa na Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo.
AFISA KILIMO wa Kata ya Bwasi, Ndugu Alex Mihambo anaendelea KUSHAWISHI na KUHAMASISHA Wanavijiji waunde VIKUNDI vya KILIMO kurahisisha UTOAJI wa MAFUNZO ya KILIMO na utafutaji wa MASOKO ya MAZAO yao.
SHUKRANI kutoka kwa VIKUNDI VYA KILIMO vya Vijiji vya Bugunda na Kome zinapelekwa kwa:
* SERIKALI yetu kwa kuwapatia WATAALAMU wa KILIMO walioko kwenye Halmashauri yetu.
* PCI (Project Concern International, USA) kwa kutoa bure MBEGU za MAHINDI kwa Kikundi cha JIPE MOYO cha Kijijini Kome. PCI imepanga kukipatia Kikundi hiki MASHINE ya UMWAGILIAJI.
* MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo kwa kugawa bure ZANA za KILIMO (plau na mashine ya umwagiliaji) na MBEGU za MIHOGO, MTAMA na ALIZETI kwa Wakulima wa Kata ya Bwasi.