UJENZI WA SHULE MPYA SHIKIZI KUTATUA MATATIZO YA UMBALI MREFU WA KUTEMBEA NA MIRUNDIKANO   MADARASANI

WANANCHI na VIONGOZI wao wa Kijiji cha Buanga, Kata ya Rusoli wakiendelea na UJENZI wa VYUMBA vya MADARASA ya SHULE SHIKIZI yao.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
KIJIJI cha BUANGA cha Kata ya RUSOLI kina Jumla ya VITONGOJI 9 na SHULE za MSINGI 2 (S/M Bwenda na S/M Bwenda B).
MWALIMU MKUU wa S/M Bwenda B, Mwl Christopher Cosmas  amesema Shule hiyo iliyofunguliwa Mwaka 2015 ina jumla ya WANAFUNZI 482, VYUMBA vya MADARASA 4 na inao UPUNGUFU wa Vyumba 5 vya Madarasa. Kwa hiyo MADARASA 4 yanasomea CHINI ya MITI na kipo Chumba cha Darasa kina WANAFUNZI 99.
MATATIZO ya UMBALI MREFU wa kutembea na MIRUNDIKANO madarasani ya WANAFUNZI wa kutoka VITONGOJI 9 vya Kijiji cha Buanga,  yamewalazimisha WANANCHI WAAMUE kuyatatua kwa kujenga SHULE SHIKIZI MPYA kwenye KITONGOJI cha CHIRUGWE.
MWENYEKITI wa Kijiji cha Buanga, Ndugu Kejile Eyembe amesema WATOTO WAO wanatembea umbali wa KILOMITA 5 kwenda masomoni kwenye Shule Mama ya Bwenda (S/M Bwenda & S/M Bwenda B). Kwa hiyo, WAMEAMUA kujenga Shule MPYA, yaani SHULE SHIKIZI na WANANCHI WAMEKUBALIANA kuchanga Tsh 10,000 (elfu kumi) kutoka kila KAYA, na tayari ujenzi umeanza.
DIWANI wa Kata ya RUSOLI, Mhe Boaz Nyeula amesema UJENZI wa SHULE hiyo unachangiwa na NGUVUKAZI na FEDHA za WANAKIJIJI, na WADAU wengine wa MAENDELEO wakiwemo WAZALIWA wa Kijiji cha Buanga.
MALENGO ya UJENZI ni kukamilisha VYUMBA 7 vya MADARASA, OFISI 1 ya Walimu na VYOO vya Wanafunzi na Walimu.
SHUKRANI KUTOKA KIJIJI CHA BUANGA
Wananchi na Viongozi wa Kijiji cha Buanga wakiongozwa na Diwani wao huyo wanatoa SHUKRANI nyingi kwa:
* SERIKALI na HALMASHAURI yake kwa kushirikiana na WANANCHI kujenga na kuboresha MIUNDOMBINU ya Shule za Msingi za Kijiji cha Buanga na Kata yao yote ya Rusoli.
* PLAN CONCERN INTERNATIONAL (PCI) kwa kujenga VYOO, kugawa VITABU na CHAKULA kwa Wanafunzi.
* MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo kwa MICHANGO yake ya:
(i) S/M Bwenda –
Madawati 92, Saruji Mifuko 60 na Vitabu vingi vya Maktaba
(ii) S/M Bwenda B –
Madawati 70, Saruji Mifuko 60, Mabati 50 na Vitabu vingi vya Maktaba
(iii) Shule SHIKIZI inayojengwa: SARUJI MIFUKO 100.
OMBI KUTOKA KWA WANAKIJIJI
WAZALIWA wa Kijiji cha Buanga na Kata ya RUSOLI wanaombwa WAJITOKEZE KUCHANGIA UJENZI wa SHULE SHIKIZI ya Kijiji cha Buanga iliyopangwa kufunguliwa mwakani (Januari 2021).
SHULE ZA MSINGI NDANI YA JIMBO LETU
HALMASHAURI ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) na JIMBO lake la Musoma Vijijini (Vijiji 68, Kata 21) ina jumla ya:
* Shule za Msingi za Serikali 111
* Shule za Msingi za Binafsi 3
* Shule Shikizi 11 (nyingine zimeishafunguliwa na nyingine zinakamilisha ujenzi)
* MAKTABA kwenye Shule za Msingi zipo chache na ujenzi unaendelea.