WANAVIJIJI WAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI, PCI NA CRDB KUBORESHA MIUNDOMBINU YA SHULE ILIYOFUNGULIWA MWAKA 1956

baadhi ya WANANCHI wa KIJIJI cha KIEMBA, Kata ya Ifulifu wakiwa kwenye kazi za ujenzi wa MIUNDOMBINU ya S/M MURUNYIGO

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
WANAKIJIJI cha Kijiji cha Kiemba, Kata ya Ifulifu wameendelea kushirikiana na WADAU wa MAENDELEO kuboresha MIUNDOMBINU ya SHULE YA MSINGI MURUNYIGO iliyofunguliwa Mwaka 1956.
Hivi karibuni BENKI ya CRDB imechangia ukamilishaji wa ujenzi wa chumba kimoja cha DARASA kwenye Shule hiyo.
MWALIMU MKUU wa Shule hiyo, Mwl Grace Majinge amesema kwamba jumla ya WANAFUNZI Shuleni hapo ni 846, na mahitaji ya VYUMBA vya MADARASA ni 21, vilivyopo ni 9 na UPUNGUFU ni 12.
BENKI ya CRDB imechangia kupunguza UPUNGUFU huo kwa kutoa VIFAA vya UJENZI vya kukamilisha CHUMBA kimoja (1) cha DARASA.
AFISA MTENDAJI wa Kijiji hicho, Ndugu Regina Mafuru Chirabo ameorodhesha VIFAA vilivyochangwa na CRDB kuwa ni: SARUJI MIFUKO 60, RANGI NDOO 2 na KOPO 1, SQUARE PIPE 5, FLAT BAR 10, SHEET 1, KOMEO na BAWABA.
AFISA MTENDAJI huyo na WANANCHI wa Kijiji cha Kiemba na VIONGOZI wengine, wakiwemo DC, DED na MBUNGE wa Jimbo WAMEISHUKURU sana BENKI ya CRDB kwa MCHANGO huo na kwa pamoja wameahidi kukamilisha ujenzi huo kabla ya tarehe 30 Mei 2020.
MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha  Kiemba, Ndugu  Rocket Mauna Rukiko ameungana na WANAKIJIJI wenzake KUSHUKURU WADAU wengine wa MAENDELEO waliokwishachangia UJENZI kwenye Shule hiyo, ambao ni: SERIKALI, PCI na MBUNGE wa JIMBO lao.
SERIKALI inaendelea kugharamia UBORESHAJI wa Elimu kwenye Shule hiyo. MRADI wa EQUIP wa SERIKALI yetu nao umechangia sana UBORESHAJI wa Elimu Shuleni hapo.
PROJECT CONCERN INTERNATIONAL (PCI) imejenga VYOO vya S/M Murunyigo. Imetoa CHAKULA cha WANAFUNZI, VITABU, ELIMU ya AFYA na inaendelea kuchangia UBORESHAJI wa ELIMU kwenye Shule hiyo.
MBUNGE wa JIMBO la Musoma Vijijini,  Prof Sospeter Muhongo amechangia Shule hiyo ifuatavyo: SARUJI MIFUKO 60, MADAWATI 106 na VITABU vingi vya MAKTABA.
OMBI KUTOKA KWA WANAVIJIJI
KIJIJI cha Kiemba, Kata ya Ifulifu kinawaomba WADAU wa MAENDELEO wakiwemo WAZALIWA wa Kijiji na Kata hiyo KUCHANGIA ujenzi wa Miundombinu ya Shule yao ya Msingi iliyoanzishwa Mwaka  1956.