ZAHANATI KWA KILA KIJIJI – KATA YA NYEGINA YATEKELEZA ILANI YA CCM

MAFUNDI na VONGOZI wa Kata ya Nyegina wakiwa kwenye eneo la Ujenzi wa ZAHANATI ya KIJIJI cha MKIRIRA, Kata ya NYEGINA.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
KATA YA NYEGINA ina Vijiji 3 ambavyo ni Kurukerege, Mkirira na Nyegina.
KIJIJI cha NYEGINA kinayo ZAHANATI ambayo inapanuliwa kwa kuongeza WADI ya MAMA na MTOTO. Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo amechangia SARUJI MIFUKO 200 kwenye ujenzi wa WADI hiyo.
KIJIJI CHA KURUKEREGE kilisimamisha kwa muda ujenzi wa ZAHANATI yake baada ya kupata fedha kutoka PIC kujenga VYOO vya S/M Kurukerege. Kazi hiyo imekamilika na sasa wanaendelea na ujenzi wa ZAHANATI ya Kijiji chao. Mbunge wao wa Jimbo atakagua ujenzi huo na kuchangia ipasavyo.
KIJIJI CHA MKIRIRA
kinajenga ZAHANATI yake kwa kushirikisha WAZALIWA wa Kijiji hicho na WADAU wengine wa MAENDELEO.
UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA MKIRIRA
Afisa Mtendaji wa Serikali ya Kijiji cha Mkirira, Ndugu  Sabina  Chacha amesema kuwa WANAKIJIJI wamekusudia kukamilisha ujenzi wa BOMA la ZAHANATI yao ifikapo mwishoni mwa Mwezi huu (April 2020).
WANAVIJIJI wakiongozwa na DIWANI wao, Mhe Majira Mchele, wanachangia NGUVUKAZI na FEDHA taslimu kwenye ujenzi wa ZAHANATI ya Kijiji cha MKIRIRA.
DIWANI huyo ametoa SHUKRANI nyingi kwa WAZALIWA na Kijiji hicho kwa MICHANGO yao iliyofanikisha ujenzi kufikia hatua hiyo. Vilevile, amesema baadhi ya WAZALIWA wa Kijiji hicho wameanzisha UMOJA wao uitwao, “MKIRIRA MAENDELEO” kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ZAHATI ya Kijiji chao.
DIWANI huyo ameendelea kutoa SHUKRANI zake kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo kwa kuchangia SARUJI MIFUKO 200 kwenye ujenzi wa ZAHANATI hiyo na kwa MICHANGO yake mingi ndani ya KATA hiyo kwenye SEKTA za Elimu, Afya, Kilimo, Mazingira, Michezo na Utamaduni.
SHUKRANI ZA KIPEKEE zinapelekwa NMB kwa kuchangia MABATI 182. Mhe Amina Makilagi (Mb)  anapewa SHUKRANI nyingi kwa MICHANGO yake.
Aidha, MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji hiki, Ndugu Magogwa Majinge alisema bado kuna UPUNGUFU wa VIFAA VYA UJENZI wa nondo 12 na Saruji Mifuko 40 kukamilisha ujenzi wa BOMA hilo.
UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM (2015-2020) kwenye SEKTA YA AFYA unaendelea vizuri ndani ya JIMBO la Musoma Vijijini kwa USHIRIKA wa SERIKALI na WANANCHI:
* Zahanati Mpya 14
zinajengwa
* Hospitali ya Wilaya moja (1) inajengwa
* Zahanati moja (1) ya Masinono inapanuliwa kuwa Kituo cha Afya
* Zahanati zinazotoa HUDUMA ni 28 (24 za Serikali & 4 za Binafsi)
*Vituo vya Afya vinavyotoa HUDUMA ni viwili (2)
KARIBUNI TUKAMILISHE UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA MKIRIRA NA NYINGINE 13 ZINAZOJENGWA KWENYE VIJIJI VINGINE 13 JIMBONI MWETU