WANAFUNZI 157 WA KIDATO CHA KWANZA  HAWATARUNDIKANA MADARASANI 

Kazi za upauaji na upigaji lipu wa VYUMBA VIPYA vya MADARASA ya KIDATO cha KWANZA (2020) cha BULINGA SEKONDARI ya Kata ya Bulinga.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
BULINGA SEKONDARI ya Kata ya Bulinga ilisajiliwa Mwaka jana (2019) na kabla ya hapo ilikuwa SEKONDARI SHIKIZI ya Nyanja Sekondari ya Kata jirani ya Bwasi.
KATA YA BULINGA yenye Vijiji 3 vya Bujaga, Bulinga na Busungu imekamilisha ujenzi wa VYUMBA 3 VIPYA vya MADARASA kwa ajili ya WANAFUNZI wa KIDATO cha KWANZA (Form I) wa Sekondari yao ya Kata.
MWALIMU MKUU wa Sekondari hiyo, Mwl Nyang’oso Chacha Munyera ameeleza kwamba jumla ya WANAFUNZI waliochaguliwa kujiunga KIDATO cha KWANZA Mwaka huu (Januari 2020) ni 157 na hadi sasa WANAFUNZI 134 ndio WAMEANZA MASOMO Shuleni hapo.
CHUMBA kimoja cha Darasa kilikuwa kinachukua WANAFUNZI 67, na baada ya KUKAMILISHA ujenzi wa VYUMBA 3 VIPYA, sasa kila CHUMBA kimoja cha Darasa kitachukua WANAFUNZI 45 – hakuna mirundikano madarasani!
MTENDAJI KATA hiyo, Ndugu Pima  Mengere amesema upauaji na upigaji lipu VYUMBA VIPYA 2 ulikamilika tarehe 25 Machi 2020 na muda mfupi ujao watakamilisha kazi ya kupiga lipu Chumba cha tatu. Kwa hiyo, WANAFUNZI 134 wa KIDATO cha KWANZA watakaporudi Shuleni (baada ya likizo ya CORONAVIRUS) watakuwa na VYUMBA VIPYA 3 vya Madarasa yao – hakuna mirundikano madarasani.
WANAVIJIJI wamechangia NGUVUKAZI zao na FEDHA taslimu Tsh 10,500 kutoka kila KAYA.
DIWANI wa KATA ya Bulinga, Mhe Mambo Japani (CHADEMA) amesema kwamba kuna MIPANGO imewekwa na WANAVIJIJI ya KUSHIRIKIANA na SERIKALI kupitia HALMASHAURI yao na MBUNGE wao wa Jimbo, KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU kwenye SEKONDARI hiyo na SHULE zote za MSINGI ndani ya Kata yao.
DIWANI huyo amesema ifikapo Januari 2021, MADARASA CHINI YA MITI yatatoweka kabisa. Ameishukuru sana SERIKALI kwa MICHANGO yake kwenye SEKTA YA ELIMU ndani ya Kata yao.
MICHANGO YA MBUNGE WA JIMBO
Mbunge Prof Sospeter Muhongo amechangia:
* MADAWATI, VITABU vingi vya MAKTABA, SARUJI na MABATI kwa Shule zote za Msingi za Kata ya Bulinga.
* BULINGA SEKONDARI: Mbunge huyo amechangia Saruji Mifuko 192 na Vitabu vingi vya Maktaba. MFUKO wa JIMBO umechangia Mabati 108.
WAZALIWA wa KATA ya BULINGA wanaombwa wajitokeze kuchangia MIRADI ya MAENDELEO ya KATA yao ikiwemo ya UBORESHAJI wa Miundombinu ya Elimu kwenye Shule za Msingi na Sekondari.