BENKI YA CRDB YACHANGIA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA S/M MURUNYIGO

Mkuu wa Wilaya (DC) ya Musoma, Dr Vicent Naano Anney (pichani – mwenye Kaunda Suti ya kijivu) akipokea VIFAA VYA UJENZI kutoka Benki ya CRDB kwa ajili ya S/M Murunyigo ya Kijiji cha Kiemba, Kata ya Ifulifu.

Jumamosi, 4.4.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
AZIMIO LA MKOA WA MARA la kujenga na kuboresha MIUNDOMBINU YA ELIMU kwenye Shule zake za MSINGI na SEKONDARI unaendelea kutekelezwa kwa kasi ya kuridhisha ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma yenye Jimbo la MUSOMA VIJIJINI.
Jana, Ijumaa, 3.4.2020, Mkuu wa Wilaya (DC) ya Musoma, Dr Vicent Naano Anney alipokea VIFAA VYA UJENZI kutoka Benki ya CRDB, Tawi la Musoma.
Ndugu Solomon Marwa, Meneja wa Benki ya CRDB, Tawi la Musoma alikabidhi VIFAA hivyo ambavyo ni: SARUJI MIFUKO 60 na VIFAA vya kutengeneza MILANGO na MADIRISHA. Vifaa vyote vinagharimu Tsh Milioni 2.
WANANCHI wa Kijiji cha Kiemba chenye S/M Murunyigo na VONGOZI wao wanaishukuru sana Benki ya CRDB kwa MCHANGO huo uliopatikana kwa muda muafaka.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dr Vicent Naano Anney, Mkurugenzi Mtendaji (DED) wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Ndugu John Kayombo na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo WANAISHUKURU sana Benki ya CRDB kwa MCHANGO huo na mingine waliyokwishaitoa ndani ya Wilaya yao.