PROGRAMU YA KUBORESHA KILIMO NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

UGAWAJI WA PLAU kwa VIKUNDI 25 kutoka VIJIJI 25 vya JIMBO la Musoma Vijijini.

ZAWADI YA PASAKA
JIMBO la Musoma Vijijini HUSHEREHEKEA Sikukuu za PASAKA, EID AL FITR na KRISMASI kwa  NGAZI ya JIMBO kwa WANAVIJIJI kuwa na TAFRIJA za CHAKULA cha PAMOJA wakiwa na Mbunge wao wa Jimbo.
HADHARI ZA VIRUSI VYA KORONA zinazuia TAFRIJA hizi kufanyika kwa WAKATI HUU na badala yake PROGRAMU YA KUONDOA JEMBE LA MKONO VIJIJINI mwetu inaendelea KUTEKELEZWA.
UBORESHAJI WA KILIMO JIMBONI MWETU
Tunaendelea KUTEKELEZA PROGRAMU hii kwa kufanya yafuatayo:
(1) KUONDOA JEMBE LA MKONO: Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ANAENDELEA KUGAWA PLAU (jembe la kukokotwa na ng’ombe au punda) kwenye VIKUNDI VYA KILIMO.
PASAKA (12.4.2020) Mbunge huyo amegawa PLAU 25 kwa VIKUNDI 25 kutoka VIJIJI 25.
Mbunge huyo aligawa PLAU 20 kutoka VIJIJI 20 ikiwa ni ZAWADI ya Mwaka Mpya (2020).
ZAWADI YA EID AL FITR (2020) itakuwa ya kugawa PLAU 40 kutoka VIKUNDI 40 vya VIJIJI 40.
Hatua kwa hatua PLAU zitatumika kwa wingi zaidi VIJIJINI mwetu badala ya JEMBE LA MKONO
(2) KUONGEZA IDADI YA MAZAO YA BIASHARA
Mbunge huyo wa Jimbo la Musoma Vijijini kwa MISIMU 3 mfululizo AMEGAWA BURE Tani 9.66 za MBEGU za ALIZETI ikiwa ni MPANGO wa kuongeza IDADI ya MAZAO ya BIASHARA Jimboni humo. SERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo ilichangia Tani 10 za MBEGU za ALIZETI
Prof Muhongo, Mbunge wa JIMBO la Musoma ameendelea KUWASHAWISHI Wakulima wa Jimboni humo KUPANUA KILIMO cha MAZAO ya CHAKULA ili KUJITOSHELEZA kwa CHAKULA na kuyafanya MAZAO hayo nayo kuwa sehemu ya MAZAO ya BIASHARA. Mbunge huyo AMEGAWA BURE Mbegu bora za MIHOGO, MTAMA na ULEZI.
(3) KILIMO CHA UMWAGILIAJI
MFUKO wa JIMBO ulitoa FEDHA, Mwaka 2016, za kununua VIFAA vya UMWAGILIAJI kwa baadhi ya VIKUNDI vya KILIMO. Kilimo hiki kinawekewa MKAZO na MRADI mkubwa wa KILIMO cha UMWAGILIAJI kwenye Bonde la BUGWEMA uko kwenye matayarisho.
VIPAUMBELE VYA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM (2015-2020)
JIMBO la Musoma Vijijini na Halmashauri yake ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) limechagua VIPAUMBELE 5 kwenye UTEKELEZAJI wa ILANI hiyo.
VIPAUMBELE Vikuu vitano ni: (i) ELIMU, (ii) AFYA, (iii) KILIMO (+ Uvuvi na Ufugaji), (iv) MAZINGIRA, na (v) MICHEZO na UTAMADUNI. Maji, Umeme, Barabara, Vyombo vya Usafirishaji na Mawasiliano ni NYENZO MUHIMU za kufanikisha UTEKELEZAJI wa MIRADI ya VIPAUMBELE hivyo vitano.
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM
Tarehe 7 Julai 2019, KITABU cha Kurasa 110 (cha rangi) cha TAARIFA ya UTEKELEZAJI WA ILANI hiyo kati ya Mwezi Januari 2016 na Juni 2019 kilichapishwa na NAKALA 5,000 kusambazwa VIJIJINI (Jimboni) na kwingineko ndani ya CHAMA na SERIKALI.
Tarehe 7 Julai 2020, KITABU kidogo kinachotoa TAARIFA ya UTEKELEZAJI wa ILANI  wa 1 Julai 2019 – 30 Julai 2020 (kikiwa na MIRADI inayoendelea hadi tarehe 30 Disemba 2020) kitachapishwa na kusambazwa.
Vilevile, KITABU chenye TAARIFA ya UTEKELEZAJI wa ILANI ya CCM ndani ya JIMBO la Musoma Vijijini, kimeambatanishwa hapa.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini