SHULE YA MSINGI MURANGI B YAKARIBIA KUACHANA NA DARASA NA OFISI CHINI YA MITI

UPAUAJI wa CHUMBA kimoja cha Darasa S/M MURANGI B ya Kijijini Lyasembe, Kata ya Murangi

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
MWALIMU MKUU wa S/M Murangi B, Mwl Kerango Msakambi ameeleza kwamba SHULE hiyo ina jumla ya WANAFUNZI 544, WALIMU 6. Vyumba vya Madarasa vilivyopo ni 7 na UPUNGUFU ni 9. Shule ilifunguliwa Mwaka 2014 na iko Kijijini Lyasembe, Kata ya Murangi.
Chumba cha Darasa lenye WANAFUNZI WENGI kinao 124 (Std III) na chenye wachache ni 59 (Std II).
WANAFUNZI wa Darasa la II hawana Chumba chao cha Darasa, kwa hiyo WANASOMEA chini ya MTI au ikibidi wanapokezana (kusoma kwa zamu) na Darasa la I lenye Wanafunzi 71.
WALIMU hawana OFISI, wanakaa CHINI YA MITI na mvua ikinyeesha wanahamia MADARASANI.
Diwani wa Kata ya Murangi, Mhe Simion Kujerwa amesema kwamba KATA imedhamiria kutatuta TATIZO SUGU la MIRUNDIKANO YA WANAFUNZI Madarasani. WANAVIJIJI na WAZALIWA wa Kata hiyo wameanza kuchangia ujenzi wa MIUNDOMBINU bora kwenye Shule zilizoko ndani ya Kata yao.
KATA ya Murangi, yenye VIJIJI 2 (Lyasembe na Murangi) inazo SHULE ZA MSINGI 4 na SEKONDARI 1.
DIWANI huyo anaishukuru sana SERIKALI kupitia Halmashauri yao na Mbunge wao, Profesa Sospeter Muhongo kwa  MICHANGO ya MIRADI ya MAENDELEO kwenye Kata yao. Ameeleza kwamba MBUNGE wao wa JIMBO amechangia SARUJI, MADAWATI na VITABU vingi kwa SHULE zote nne (4) za MSINGI. MURANGI SECONDARY School imepewa VITABU VINGI vya MAKTABA
UKAMILISHAJI WA DARASA LA S/M MURANGI B
Njia pekee ya kuwatoa WANAFUNZI (Std II) CHINI ya MTI ni KUKAMILISHA Chumba kimoja cha Darasa kinachoezekwa kwa MABATI 54 yaliyonunuliwa na FEDHA za MFUKO wa JIMBO.
MBUNGO wa Jimbo anachangia SARUJI MIFUKO 50 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Chumba hicho. SARUJI hiyo itachukuliwa tarehe 2.4.2020.
Baada ya JENGO hilo kukamilika, Mbunge wa Jimbo atapiga HARAMBEE ya kujenga VYUMBA 2 VIPYA vya Madarasa vyenye OFISI ya WALIMU katikati.
WAZALIWA wa KATA ya MURANGI wanaombwa wajitokeze KUCHANGIA UJENZI huu na MIRADI mingine ya MAENDELEO inayotekelezwa ndani ya Kata yao.
Kwa muda wa takribani MIAKA MINNE na NUSU (4.5 yrs), JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI limeendelea KUJENGA na KUBORESHA MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye SHULE zake zote za MSINGI (114 – 111 za Serikali na 3 za Binafsi) na SEKONDARI (22 – 20 za Serikali na 2 za Binafsi). MADAWATI na VITABU VINGI vya MAKTABA vimegawiwa. Sekondari Mpya 5 zinajengwa zifunguliwe mwakani  (Januari 2021).
WADAU WA MAENDELEO wakiwemo PCI, NMB, CRDB na baadhi ya WAZALIWA wa Vijiji vya Jimbo hili WANAENDELEA KUCHANGIA MIRADI muhimu kwenye SEKTA YA ELIMU ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini – TUNAWASHUKURU SANA!
Picha zilizoko hapa zinaonesha UPAUAJI wa CHUMBA kimoja cha Darasa ya S/M MURANGI B ya Kijijini Lyasembe, Kata ya Murangi.