MATATIZO YA UMBALI MREFU WA KUTEMBEA NA MIRUNDIKANO YA WANAFUNZI MADARASANI YAENDELEA KUTATULIWA

Ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa unaoendelea kwenye SHULE SHIKIZI BURAGA MWALONI inayojengwa kwenye Kitongoji cha Mwaloni, Kijijini Buraga, Kata ya Bukumi.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
AZIMIO NA. 1 LA UBORESHAJI WA KIWANGO CHA ELIMU NDANI YA MKOA WA MARA
(1) Uboreshaji wa MIUNDOMBINU ya ELIMU ya aina zote katika Shule za Msingi na Sekondari
JIMBO la Musoma Vijijini LINATEKELEZA AZIMIO hilo na mengine matano (5) kwa USHIRIKA wa WANANCHI, VIONGOZI na SERIKALI yao – MATUNDA MAZURI yameanza kuonekana.
SHULE ZA MSINGI JIMBONI
* 111 za Serikali
* 3 za Binafsi
UJENZI unaendelea kwenye SHULE zote za MSINGI ili kuboresha MIUNDOMBINU yao ya ELIMU.
MATUNDA YA AWALI yaliyopatikana tokea UBORESHAJI wa MIUNDOMBINU ya SHULE ZA MSINGI uanze, miaka minne (4) iliyopita ni HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA (yenye Jimbo la Musoma Vijijini) kuwa ya KWANZA MKOANI MARA Mwaka jana (2019) kwenye MITIHANI YA DARASA LA NNE (IV).
SHULE SHIKIZI JIMBONI
* 11 zinaendelea kujengwa na baadhi tayari zina WANAFUNZI wa Darasa la AWALI na la kwanza (Std I).
Ujenzi wa SHULE MPYA hizi unazingatia UBORA unaotakiwa kwa MIUNDOMBINU yake.
UJENZI WA SHULE SHIKIZI BURAGA MWALONI
SHULE MPYA hii inajengwa na WAKAZI wa Kitongoji cha Buraga Mwaloni ili KUTATUA TATIZO la WATOTO wao wenye UMRI wa chini ya MIAKA 10 kutembea umbali wa kilometa 5-7 kwenda masomoni kwenye SHULE za MSINGI za vitongoji jirani.
MWALIMU WA KUJITOLEA, Ndugu Dickson Maregesi ndie MSIMAMIZI wa SHULE SHIKIZI Buraga Mwaloni. Amesema SHULE hiyo ilianza rasmi Mwaka 2015 ikiwa na jumla ya WANAFUNZI 117 waliokuwa wanasomea CHINI YA MTI na baada ya kuhitimu hapo WALIENDA kuanza MASOMO ya Darasa la kwanza (Std I) kwenye SHULE ZA MSINGI za Buraga na Chitare ambazo ziko mbali na Kitongoji cha Mwaloni.
Kwa wakati huu, WANAFUNZI 41 wa Darasa la Awali wa SHULE SHIKIZI hiyo wanasomea chini ya MTI.
Ndugu Nyajoge Wanjara, Mwenyekiti wa KAMATI ya ujenzi wa Shule hiyo amesema WANA-KITONGOJI wameanza KUCHANGIA UJENZI wa Shule yao kwa kutoa NGUVUKAZI na Fedha taslimu kiasi cha Tsh 5,000/= kutoka kila KAYA. Kiongozi huyo amesisitiza kwamba  SHULE yao hiyo ujenzi utakamilika na kufunguliwa Januari 2021.
MICHANGO MINGINE
* Saruji Mifuko 50 kutoka MFUKO wa JIMBO
* Saruji Mifuko 100 kutoka kwa Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo
WAZALIWA wa Kata ya Bukumi na hasa wa Kijiji cha Buraga wanaombwa KUTOA MICHAGO ya ujenzi wa Shule hiyo ambayo inahitaji VYUMBA vipya vya Madarasa, Ofisi ya Walimu, Vyoo na Nyumba ya Walimu.
WADAU wengine wa Maendeleo nao wanaombwa KUCHANGIA.