OFISI YA CCM YA WILAYA YA MUSOMA YAANZA KUJENGWA

Uanzaji wa ujenzi wa OFISI YA CCM ya Wilaya ya Musoma Vijijini, yaani UCHIMBAJI wa MSINGI na UFYATUAJI wa MATOFALI.

OFISI YA MUDA ya CCM ya Wilaya ya Musoma Vijijini iko kwenye Kijiji cha Chumwi, Kata ya Nyamrandirira.
Wana-CCM wa Musoma Vijijini (kwenye Vitongoji 374, Vijiji 68, Kata 21) wakiongozwa na KAMATI YA UJENZI wameanza rasmi kujenga OFISI YA CCM ya Wilaya yao.
MWENYEKITI wa KAMATI ya Ujenzi ni Dr Vicent Anney Naano, Mkuu wa Wilaya (DC) ya Musoma na MAKAMU MWENYEKITI ni Mhe Diwani Charles Magoma Nyambita, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.
Ndugu John Lipesi Kayombo, Mkurugenzi Mtendaji (DED) wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ANASHIRIKI vizuri sana kwenye UTEKELEZAJI wa MRADI huu.
HATUA ZA AWALI ZA UJENZI
Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi amewezesha upatikanaji wa MAWE na MCHANGA wa kuanzia ujenzi. FUNDI ameanza kuchimba MSINGI.
AHADI ZA MICHANGO ILIYOTOLEWA KWENYE HARAMBEE YA UJENZI
KAMATI ya ujenzi INASUBIRI WALIOTOA AHADI za VIFAA VYA UJENZI na FEDHA TASLIMU watimize AHADI zao ili ujenzi uende kwa kasi kubwa.
AHADI YA MBUNGE WA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo alihaidi kutoa MCHANGO wa awali wa MATOFALI 5,000 (elfu tano). Alianza kwa kununua MATOFALI 1,000 kutoka Kanisa Katoliki Nyegina.
KAMATI YA UJENZI imependekeza MATOFALI yatengenezewe karibu na eneo la ujenzi ili kuachana kabisa na GHARAMA za kusafirisha MATOFALI. Kwa hiyo, Mbunge huyo ameanza kununua SARUJI hapo hapo Kijijini (Murangi) ya kutengenezea MATOFALI 5,000.
Vilevile, Mbunge huyo atachangia FEDHA za kumlipa FUNDI ujenzi.
Diwani wa Kata ya Murangi, Mwenyeji wa MRADI huu, Mhe Simion Kujerwa ANAFANYA KAZI NZURI ya kusimamia ujenzi wa OFISI hii  ya CCM Wilaya.