HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA YASHIRIKIANA NA PCI KUSHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 

MGENI RASMI, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo ALICHANGIA Jumla ya MAGUNIA 11 ya mahindi na MAGUNIA 2.75 ya maharage.

SHEREHE ZA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, yenye Jimbo la Musoma Vijijini, zilifanyika jana, Ijumaa, tarehe 13 Machi 2020, kwenye Kijiji cha CHIRORWE, Kata ya SUGUTI. MGENI RASMI alikuwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo.
MATUKIO mawili (2)  MUHIMU sana yalifanyika Kijijini Chirorwe: (i) kuchangia CHAKULA  MASHULENI na (ii) HALMASHAURI yetu kugawa MIKOPO ISIYOKUWA NA RIBA kwa VIKUNDI vya WANAWAKE, VIJANA na Watu wenye ULEMAVU.
SHEREHE hizi hufanyika kila Mwaka kwa mzunguko ndani ya Kata za Halmashauri hii na  WARATIBU wake ni HALMASHAURI yenyewe kwa KUSHIRIKIANA na PCI-WE.
PROJECT CONCERN INTERNATIONAL (PCI) ni SHIRIKA la KIMATAIFA lenye MALENGO ya kuboresha AFYA, kukomesha NJAA, kupambana na ugumu wa MAISHA na kuendeleza  WANAWAKE na WASICHANA. PCI ilianzishwa Mwaka 1961 nchini Marekani (USA).
Project Concern International – Women Empowered (PCI-WE) ni MPANGO MAALUM wa PCI unaolenga KUHAMASISHA na KUWEZESHA WANAWAKE kiuchumi na kijamii kupitia UUNDAJI wa VIKUNDI vya KUWEKA na KUKOPA.
PCI-WE NDANI YA JIMBO LETU
* Inahudumia jumla ya Kata 14 ambazo ni: Bugwema, Bukima, Bukumi, Bulinga, Bwasi, Etaro, Ifulifu, Kiriba, Makojo, Mugango, Nyakatende, Nyegina, Rusoli na Suguti.
* Jumla ya VIKUNDI 169 vimeanzishwa ndani ya Kata hizo 14.
WAKUFUNZI WA PCI WAPEWA BAISKELI
* WAKUFUNZI 47 wa wa PCI ndani ya Jimbo letu wamepewa BAISKELI 47 ili kurahisisha USAFIRI wao kwenye maeneo yao ya kazi. MAKABIDHIANO ya BAISKELI hizo yalifanyika wakati wa SHEREHE za SIKU YA WANAWAKE DUNIANI yaliyofanyika jana Kijijini Chirorwe.
VIKUNDI VYA PCI VYAHAMASISHA WASHIRIKI WA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KUCHANGIA CHAKULA MASHULENI
* VIKUNDI vya PCI vya Kijiji cha Chirorwe, kwa kuungwa mkono na VIKUNDI vingine vya PCI, na WASHIRIKI wa Sherehe za SIKU YA WANAWAKE DUNIANI Kijijini Chirorwe, WALIFANIKIWA kuchangia na kukusanya Jumla ya TANI 5.6 za CHAKULA (mahindi na maharage) kwa ajili ya SHULE ZA MSINGI 2 za Kijiji hicho ambazo ni: S/M SOKOINE na S/M CHIRORWE. Chakula hicho kinatosha kutumiwa kwa muda wa Mwaka mmoja.
* Jumla ya TANI 2.7 nyingine za CHAKULA zilikusanywa kwenye hafla hiyo ikiwa ni mwanzo wa UCHANGIAJI wa CHAKULA kwa ajili ya SHULE NYINGINE ndani ya Kata hiyo. Idadi yake (mbali ya hizo za Kijiji cha Chirorwe) ni SEKONDARI 1 na SHULE ZA MSINGI 7.
MGENI RASMI, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo ALICHANGIA Jumla ya MAGUNIA 11 ya mahindi na MAGUNIA 2.75 ya maharage.
UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA UBORESHAJI WA KIWANGO CHA ELIMU NDANI YA MKOA WA MARA
MAAZIMIO haya yameishasambazwa sana na anayeyahitaji anaweza kuyapata kutoka OFISI Za ELIMU za Halmashauri, Manispaa na Wilaya za Mkoa wa Mara.
MOJA YA MAAZIMIO hayo ni UTOAJI WA CHAKULA kwa WANAFUNZI wawapo masomoni kwenye SHULE ZOTE za Mkoa wa Mara (Msingi na Sekondari).
*Sherehe za SIKU YA WANAWAKE DUNIANI iliyofanyika Kijijini Chirorwe zimetumika KUTEKELEZA KWA VITENDO AZIMIO HILO (Chakula cha Wanafunzi) ndani ya Jimbo letu.