MAAZIMIO YA KONGAMANO (23.3.2020) LA UBORESHAJI WA KIWANGO CHA ELIMU NDANI YA MKOA WA MARA

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo akiwa kwenye KIKAO na WANANCHI wa Kijiji cha Butata (Kata ya Bukima) wanaojenga Vyumba Vipya 2 vya Madarasa ya S/M Butata iliyoanzishwa Mwaka 1942 na ina UPUNGUFU wa Vyumba 6 vya Madarasa. Mbunge huyo alichangia SARUJI MIFUKO 100.

(1) Uboreshaji wa MIUNDOMBINU ya ELIMU ya aina zote katika Shule za Msingi na Sekondari.
(2) Kuthibiti UTORO wa WANAFUNZI kwa kuweka utaratibu wa KISHERIA wa kuthibiti tatizo hilo.
(3) Utoaji wa huduma ya CHAKULA cha MCHANA Shuleni (Msingi na Sekondari) ni LAZIMA. WAZAZI na JAMII nzima ya Mkoa wa Mara watengenezewe utaratibu wa kuchangia CHAKULA katika SHULE zao.
(4) Kuimarisha MAHUSIANO ya WALIMU na JAMII na NIDHAMU ya WANAFUNZI.
(5) Kuthibiti MIMBA kwa WATOTO wa KIKE na UKATILI wa WANAFUNZI.
(6) Kuimarisha USHIRIKI na USHIRIKISHWAJI wa JAMII katika MAENDELEO ya SHULE.
*WARATIBU na WASIMAMIZI wa UTEKELEZAJI wa MAAZIMIO hayo sita (6) ni Wakuu wa Wilaya (DCs) na Wakurugenzi Watendaji (DEDs) chini ya UONGOZI wa Mkuu wa Mkoa (RC) wa Mara
* Tarehe ya KUTATHMINI maendeleo ya UTEKELEZAJI wa MAAZIMIO hayo ni 30 AGOSTI 2020 (Kongamano la pili)
* HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA na Jimbo lake la Musoma Vijijini ILIANZA MUDA mrefu kuboresha MIUNDOMBINU ya ELIMU kwa MALENGO ya kuinua UBORA wa ELIMU kwenye SHULE zake za MSINGI (111 za Serikali & 3 za Binafsi) na SEKONDARI (20 za Serikali & 2 za Binafsi). Shule SHIKIZI 11 zinajengwa kwa kiwango kizuri.
* CHAKULA cha MCHANA Shuleni (Msingi & Sekondari) – shule chache zinatoa CHAKULA kwa Wanafunzi wawapo masomoni. Viongozi wa ngazi mbalimbali wanaendelea kuwashawishi WAZAZI wakubali kuchangia CHAKULA cha WANAFUNZI wawapo masomoni Shuleni.
OMBI
Tafadhali ungana na WANANCHI wa Jimbo la Musoma Vijijini KUTEKELEZA MAAZIMIO ya UBORESHAJI wa kiwango cha ELIMU kwenye SHULE zetu.
MATUMAINI YAPO
Hatimae MWANGA unaanza kuchomoza. Mwaka jana (2019) HALMASHAURI YETU imekuwa ya KWANZA Mkoani mwetu kwenye MITIHANI YA DARASA LA NNE. Tuongeze juhudi kwani ni muhimu kushindana na Halmashauri na WILAYA zote za nchini mwetu. TUTAFANIKIWA!