SIKU YA WANAWAKE DUNIANI: MIKOPO ISIYOKUWA NA RIBA YAENDELEA KUTOLEWA

Halmashauri ya Wilaya ya Musoma IMEFANIKIWA, kwa Mwaka huu wa Fedha (2019/2020) kutoa MIKOPO MARA MBILI.

HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA, yenye Jimbo la Musoma Vijijini INAENDELEZA UTARATIBU WAKE wa kushiriki SHEREHE za SIKU YA WANAWAKE DUNIANI kwa kutoa MIKOPO isiyokuwa na RIBA kwa Vikundi vya WANAWAKE, VIJANA na WATU WENYE ULEMAVU.
MWAKA HUU (2020) Sherehe za SIKU YA WANAWAKE DUNIANI zilifanyika juzi Kijijini CHIRORWE, Kata ya SUGUTI.
MGENI RASMI alikuwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini. VIONGOZI wa Wilaya, ukiacha waliokuwa safarini kikazi, waliongozwa na Afisa Utawala wa Wilaya (DAS).
MIKOPO ISIYOKUWA NA RIBA
Halmashauri ya Wilaya ya Musoma IMEFANIKIWA, kwa Mwaka huu wa Fedha (2019/2020) kutoa MIKOPO MARA MBILI.
DISEMBA 2019, HALMASHAURI yetu ILITOA Mikopo ya Jumla ya Tsh MILIONI 116.5 kwenye VIKUNDI 23 vya Jimboni mwetu.
MACHI 2020, kwenye Sherehe za SIKU YA WANAWAKE DUNIANI iliyofanyika juzi Kijijini Chirorwe,  HALMASHAURI yetu ilitoa MIKOPO kama ifuatavyo:
*WANAWAKE, Vikundi 16, jumla ya Tsh MILIONI 98.0
* VIJANA, Vikundi 2, jumla ya Tsh MILIONI 11.0
* WATU WENYE ULEMAVU, Vikundi 3, jumla ya Tsh MILIONI 9.4
PLAU – ZAWADI YA PASAKA KUTOKA KWA MBUNGE WA JIMBO
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ATATOA ZAWADI YA PLAU (Jembe la kukokotwa na ng’ombe/punda) kwenye SIKUKUU YA PASAKA ya Mwaka huu. VIKUNDI VYA PCI na VIKUNDI vyenye  Mikopo kutoka Halmashauri yetu  VINAVYOJISHUGHULISHA NA KILIMO ni miongoni mwa VIKUNDI vinavyotathminiwa kwa ajili ya kupewa ZAWADI YA PLAU kutoka kwa Mbunge wao.
MAFANIKIO YOTE haya na mengine mengi Jimboni mwetu ni MATUNDA ya UONGOZI mzuri wenye UBUNIFU mzuri wa DC wa Wilaya, Dr Vicent Naano Anney, DED wa Halmashauri, Ndugu John Kayombo na TIMU zao za Wafanyakazi makini.